Thursday, November 22, 2012

Duh! Kama utani vile: Askofu wa kwanza wa Kike ateuliwa


                               Ellinah Wamukoya
                                                             Ellinah Wamukoya
Ellinah Wamukoya ameteuliwa kuwa askofu wa kwanza wa kike wa kanisa la Kianglikana barani Afrika.
Akiongea muda mfupi baada ya kuteuliwa, Bi. Ellinah Wamukoya amesema uamuzi huo heshima kwa kina mama.
Ellinah Wamukoya, 61, sasa atahudumu kama askofu mpya wa kanisa hilo katika ufakme wa Swaziland, moja wapo ya nchi zinazokisiwa kufuata siasaa za kihafidina.
Kutawazwa kwake kumejiri huku kanisa la Kianglikana, likitarajiwa kujadili ikiwa kina mama wataruhusiwa kuapishwa kuwa maaskofu wa kanisa hilo.
Askofu wa jimbo la Capte Town, nchini Afrika Kusini, amesema kuwa wamechukua uamuzi huo ili wawe mfano kwa wengine na pia kuwatakia, viongozi wa kanisa hilo, faraja na hekima ili kujadilia sauala hilo kwa haraka.
Kwa mujibu wa ripoti aliyotuma kwa vyo,bo vya habari, askofu huyo wa jimbo la Cape Town, Revd. Thabo Makgoba, amesema wimbi kwa sasa linavuma na kuwa wameshuhudia tukio la kihistoria ambao ni sawa na bingu kufunguka.
David Dinkebogile aliongoza sherehe hizo na kukariri kuwa nia yao kuwa ilikuwa kumuapisha askofu na wale sio mtu mweusi, muafrika na raia wa Swaziland.
Askofu Wamukoya ni meya wa zamani wa mji mkuu wa Swaziland Manzini.

Shule ya Msingi Ndonga: Mtihani wa Taifa hubebwa kichwani, Haijawahi kukaguliwa tangu mwaka 1995





share
NI safari ya siku mbili  kutoka mjini Songea makao makuu ya mkoa wa Ruvuma hadi kuweza kuifikia shule ya msingi Ndonga iliyopo wilayani Nyasa mwambao mwa ziwa Nyasa.
Basi linaishia katika mji mdogo wa Liuli, Ziwa Nyasa na kutoka hapo inakulazimu kukodi pikipiki hadi katika kijiji cha Njambe kata ya Kihagara ambapo ndiyo mwisho wa usafiri wa pikipiki na kuanzia hapo inakulazimu kutembea kwa miguu kwa takribani saa moja hadi kukifikia kijiji cha Ndonga!
Shule ya msingi Ndonga imejengwa juu ya mlima wa Liwundi, unapofika katika kijiji cha Ndonga inakulazimu kupanda mlima wenye mwinuko mkali wenye makorongo kwa takriban zaidi ya saa moja hadi kufika kileleni ndipo unakutana na shule hii.
Asilimia 90 ya wanafunzi wanaosoma katika shule ya msingi Ndonga wanaishi chini ya mlima hivyo inawalazimu kwa siku tano yaani Jumatatu hadi Ijumaa kupanda  na kushuka mlima kwa saa mbili hali ambayo imesababisha shule hiyo kukabiliwa na utoro uliokithiri wa wanafunzi ambao unafikia kwa siku kati ya asilimia 60 hadi 70.
Wanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi Ndonga wilayani Nyasa mkoani Ruvuma wakisomea darasa ambalo halijaezekwa kwa mwaka mmoja sasa mvua na jua vikiwakabili

Wednesday, November 21, 2012

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam Yatoa Hukumu Ya Kunyogwa Hadi Kufa Watuhumiwa Wa Mauaji ya Swetu Fundikira

 Marehemu Swetu Fundikira enzi za uhai wake.
 
Watuhumiwa waliohukumiwa kifo kutokana na mauaji ya Fundikira MTM 1900 Sajenti Roda Robert(42) wa kikosi cha JKT-Mbweni na MT 75854 Koplo Ally Ngumbe (37) wa JWTZ-Kunduchi
--
 WATUHUMIWA katika mauaji ya Swetu Fundikira,  MTM 1900 Sajenti Roda Robert (42) wa kikosi cha JKT - Mbweni na MT 75854 Koplo Ally Ngumbe (37) wa JWTZ-Kunduchi leo wamehukumiwa kifo baada ya kupatikana na hatia na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.Habari zaidi Baadae

SABABU ZA ZITTO KABWE KUANDIKA KWAMBA “TUSIGEUZWE MAZEZETA, MABWEGE NA MAZEZETA HUIMBA KILA WANACHOAMBIWA” SOMA ZAIDI HAPA

 
.
Mabilioni ya Uswisi – Tusigeuzwe Mazezeta
Jumanne tarehe 20 Novemba 2012, baadhi ya vyombo vya habari vimebeba habari zinazohusu matamshi ya Waziri wa Utawala Bora ndugu George Mkuchika kuhusu sakata ya mabilioni ya Uswisi. Waziri amesema kwamba Serikali ya Uswisi inataka majina ya Watanzania walioficha fedha huko ndio waweze kusaidia uchunguzi. Habari kama Hiyo, yenye maudhui na malengo hayo hayo iliandikwa na Gazeti la The Guardian on Sunday la tarehe 18 Novemba 2012.

KERI HILSON SOON KUPIGA SHOW KALI TANZANIA NA KENYA

Msanii mahiri kutoka pande za state almaarufu kama Keri Hilson anayetamba na ngoma kali kama That way you love me,Pretty girl Rock na ngoma nyinginezo kali,mpaka kupelekea mashabiki kumkubali katika tasnia ya muziki.Sasa latest info ambayo tumeipata kutoka kwa msanii huyu ni kwamba leo asubuhi aliamua kuandika katika ukurasa wake wa twitter kwamba mwezi wa Desemba itakuwa ni mara yake ya kwanza kupiga show kali hapa Tzee na kenya.

Wednesday, October 24, 2012

Unapopewa, jiulize unatoa nini? Usiendekeze mapenzi ya kizamani

                          
YACHUKUE mapenzi halafu itazame timu ya mpira wa miguu, kikapu na hata pete (netiboli) inavyocheza. Utaona kwamba ni lazima kupeana pasi mpaka mpira unapomfikia mfungaji. Hakuna mwenye uwezo wa kutoka na mpira golini kwake, akawapita wapinzani 10 na kufunga.
                           
Mpira ni pasi, yaani kushirikiana kutafuta ushindi. Haitakiwi kutegeana. Jinsi unavyoona mpira unavyochezwa, ndivyo na uhusiano wa kimapenzi unavyojengwa. Wewe na mwenzi wako ni timu moja, sasa mnachezaje kutafuta ushindi?
Je, anapokuwa na mpira, nawe unajipanga vizuri ili akupe pasi halafu umrudishie afunge au kazi yako ni wewe kumtazama anavyokatiza na kumshangilia? Anapokabwa na maadui, unakwenda kumsaidia au yako yanabaki macho tu, yaani akidhibitiwa ubaki unasonya, akishinda mshangilie pamoja?

MWANAMME ASHITAKIWA KWA KUMTOBOA, KUMFUNGA KUFULI MKEWE UKENI

 
Mwanamke Sitabai Chouhan akiwa hospitalini.
SIKU ambayo mwanamke Sitabai Chouhan alipolazwa katika Hospitali ya Maharaja Yashwant Raoin huko Indore, India, kwa jaribio la kutaka kujiua kwa kunywa sumu ya panya, ndiyo siku manesi walipogundua kwamba mwanamke huyo alikuwa amefungwa kufuli dogo kwenye mlango wa sehemu zake za siri.
 
Mume wa Sitabai, Sohanial Chouhan.
Mume wake aitwaye Sohanial Chouhan (38) alifikishwa polisi baada ya kugundua kwamba alikuwa ana tabia ya kumfunga kufuli mkewe sehemu hizo kwa muda wa miaka minne kwa madai kwamba asingefanya hivyo angekuwa anatembea nje ya ndoa.

Monday, October 22, 2012

Umetendwa? Futa machozi, tazama mbele, usijilaumu wala usijute

 
Busara, hekima na moyo imara ni vipengele vikuu vitakavyokuwezesha kuvuka changamoto mbalimbali kwenye mapenzi. Fikiria kwamba hata barabara iliyochongwa vema na wahandisi waliobobea, bado milima na mabonde vitakuwepo.
Kama ndivyo, basi inashindikana vipi kutokea kwa hali isiyoeleweka kwenye mapenzi? Ni mambo ya kawaida mno, kwa hiyo busara na hekima viwe ndani yako. Vilevile moyo imara ukupe nguvu ya kuvuka changamoto za hapa na pale.

Wednesday, October 3, 2012

Wachina wanaongoza kwa matukio ila hili limetia fora


WAHIFADHI MWILI WA KIJANA WAO MIAKA 6 KWENYE JOKOFU NCHINI CHINA

 

Tian Xueming akiangalia mwili wa kijana wake katika jokofu.

Nyumba ya Tian Xueming.
NI miaka sita sasa tangu familia ya Tian Xueming raia wa nchini China ianze kuhifadhi mwili wa kijana wao kwenye jokofu.
Mwaka 2006, familia hiyo ilimpoteza kijana wao aliyefariki kwa ugonjwa wa leukemia. Tian Xueming mzazi wa kijana huyo aliamua kuuhifadhi mwili wa kijana wake katika jokofu. Kila mara wanapomkumbuka kijana wao, Tian na mkewe wanakwenda kimyakimya katika jokofu na kuuangalia mwili wa kijana huyo. Tim anasema kuwa "kijana wangu katika jokofu anaonekana kama alivyokuwa enzi za uhai wake. Mwanangu bado yupo pamoja nasi mpaka leo."
Miaka 15 iliyopita, familia ya Tian Xueming ilimpoteza pia binti yao aliyefariki kwa ugonjwa wa moyo. Miaka sita baadaye kijana wao naye akafariki kwa leukemia.


Angalia Rufaa ya LEMA ilivyoahirishwa mahakamani Arusha

DSCN5552 Baadhi ya wananchi waliokusanyika nje ya ofisi za Chadema Mkoa wa Arusha, eneo la Ngarenaro wakimsikiliza Mh Godbless Lema haonekeni pichani mara baada ya kutoka Mahakamani kusikiliza shauri lake kupinga kuvuliwa ubunge. Picha hii ni taswira nusu ya kwanza ya watu
DSCN5541 Mh. GodblessLema akizungumza na kuagana na wananchi waliokuwa nae  Mahakamani, mbele ya ofisi za chama hicho.
DSCN5551 Hii ni nusu nyingine ya taswira halisi za wananchi waliofika ofisini hapo…

Wednesday, September 26, 2012

Ulaya yasitisha msaada kwa Rwanda

                 

                                                        Waasi wa M23  

Muungano wa Ulaya umeamua kusitisha msaada kwa Rwanda.

Uamuzi wa Muungano huo umefikiwa kufuatia ripoti ya baraza la usalama la Umoja huo iliyodai kwamba Rwanda inaunga mkono waasi wa M23 dhidi ya serikali ya Congo.
Waasi hao wanadhibiti kimabavu sehemu kubwa ya Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo na hata kuwatoza kodi wananchi.
Kundi hilo lilianza uasi katika eneo hilo mwezi Aprili na kusababisha takriban watu nusu milioni kukimbilia usalama wao.
Lakini Rwanda imeendelea kukana madai hayo.
Umoja wa Mataifa unafanya mkutano na baadhi ya yatakayopewa kipaombele kwenye mkutano huo ni swala la mgogoro huo Mashariki mwa Congo.
Mapema mwezi Julai Marekani ilizuia dola 200,000 zilizokusudiwa kulisaidia jeshi la Rwanda.

Tuesday, September 25, 2012

Mama Rwakatare na Dk. Cheni Presha juu

Nyumba ya Dk. Cheni.
Nyumba ya Mama Rwakatare.

SAKATA la kutangazwa kubomolewa kwa majumba yao kwa sababu tofauti, Mchungaji wa Kanisa la Assembles of God Mikocheni B ‘Milima ya Moto’ la jijini Dar es Salaam, Dk. Getrude Pangalile Rwakatare na staa wa filamu za Kibongo, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’, sasa presha zao juu.
Kwa upande wa Mama Rwakatare, mjengo wake wa bei chafu aliouzindua hivi karibuni uliopo Mbezi Beach, Dar utavunjwa kwa madai kwamba umejengwa kinyume cha sheria za mazingira kwani upo katika maeneo ya kando mwa mito ya Mbezi Beach, Mndumbwe na eneo maalum la hifadhi ya miti adimu ya Mikoko.

Maaskofu kuwanyima waumini sakramenti


                   
Kanisa katoliki nchini Ujerumani
Sheria kali itakayowashurutisha waumini wa kikatoliki kulipa kodi ya kanisa la sivyo wanyimwe sakramento imepitishwa nchini Ujerumani.
Maaskofu waliopitisha sheria hiyo wamesema kuwa yeyote atakayekosa kulipia kodi ya kanisa ambayo ni asilimia nane ya mapato yao watanyimwa sakramento na kisha kutotambuliwa kama wakatoliki.
Maaskofu hao wameshtushwa na idadi ya watu wanaoendelea kuasi ukatoliki.
Wanasema kuwa hatua kama hii ya kuasi dini itakuwa ni kwenda kinyume kabisa na maadili ya jamii.

Saturday, September 22, 2012

Kuumizwa ni ajali lakini isiwe mazoea

 
KAMA kawaida tumekutana tena kwenye kona yetu ya Mapenzi na Uhusiano, leo nataka nizungumzie maumivu katika mapenzi ambayo unaweza kukutana nayo na kuyavumilia.
Kumekuwa na matukio mengi katika uhusiano yanayosababisha mmoja kuumizwa na mpenzi wake pale anapokosa uaminifu au kutoonyesha kujali hisia za mwenzake.
Ni kweli wanadamu tuna upungufu ambayo huenda ukasababisha maumivu kwa mmoja. Wapo ambao wamekuwa wakivumilia mateso ambayo wamekuwa wakiyapata kwa wenza wao, wakiamini huenda mwenzake atajirekebisha lakini bahati mbaya anayemtegemea hayaoni maumivu ya mwenzake na kuendelea kumtesa.

Waisilamu waandamana kote duniani


 

Mapambano yametokea baina ya polisi na waanda-manaji nchini Pakistan kabla ya sala ya Ijumaa, kulalamika juu ya filamu inayokejeli Uislamu iliyotengenzwa Marekani.

Shirika moja la habari la Pakistan limesema kuwa mfanyakazi wake mmoja ameuwawa mjini Peshawar wakati polisi walipofyatua risasi kutawanya makundi ya watu wenye hasira, waliojaribu kuchoma moto jengo la sinema. 

Ghasia zimeendelea hadi Magharibi, na waandamanaji hasa wakilenga ofisi za balozi wa Marekani katika miji mbali-mbali.
Ulinzi ulidhibitiwa katika nchi nyingi za kiisilamu kama Misri, Libya, Tunisia Morocco na kwingineko huku zikijiandaa kwa maandamano makubwa baada ya maombi ya Ijumaa.

Friday, September 21, 2012

CNN iReport about late Daudi Mwangosi


Petition Goverment of Tanzania 


Petition Goverment of Tanzania

 
Government of Tanzania: Stop police violence against peaceful demonstrators and journalists

PLEASE TAKE TWO MINUTES TO SIGN THIS PETITION. THERE ARE PEOPLE IN TANZANIA WHO WANT TO SIGN, BUT THEY DON'T HAVE A COMPUTER.


http://www.change.org/petitions/government-of-tanzania-stop-police-violence-against-peaceful-demonstrators-and-journalists?utm_source=supporter_message&utm_medium=email
  • TAGS:

What do you think of this story?

Select one of the options below. Your feedback will help tell CNN producers what to do with this iReport. If you'd like, you can explain your choice in the comments below.
    Awesome! Put this on TV!Almost! Needs work.This submission violates iReport's community guidelines.

Comments (10)

Log in to comment
iReport welcomes a lively discussion, so comments on iReports are not pre-screened before they post. See the iReport community guidelines for details about content that is not welcome on iReport.
Click to view bongotz's profile bongotz
3 hours ago
Today is almost two weeks since the Journalist Daudi Mwangosi was killed on the hands of the Tanzanian Government, but has not been a word of condolence or condemnation from the President whose First constitution job is to protect the Constitution of United republic of Tanzania and the lives of every Tanzanian.

BASATA WAMJIA JUU AUNT EZEKIEL

                                     
                                              

SAGA la mwigizaji wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel (pichani) kuvaa nusu utupu na kukaa kihasara huku maungo nyeti yakichungulia, limechukua sura mpya baada ya Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kumjia juu,

Baby Madaha abwaga chakula cha mtoto kwenye kuku wengi

Baby Madaha akiwa jukwaani kuwapa raha mashabiki.
Na Musa Mateja aliyekuwa Morogoro
STAA ‘seksi’ wa filamu na muziki wa Bongo Fleva, Baby Joseph Madaha amejikuta akiumbuka mbele ya mashabiki wake baada ya matiti a.k.a nido zake kuchomoza na kuonekana hadharani akiwa jukwaani na kusababisha midume yenye ukame kumzengea.

PADRI POLAND AWALISHA WANAFUNZI KRIMU ILIPAKWA KWENYE MAGOTI

POLISI nchini Poland wameanzisha uchunguzi dhidi ya Padri Marcin Kozyra wa Poland baada ya kupatikana kwa picha zinazowaonyesha wanafunzi wa kike na kiume wenye umri wa miaka 13 wakilamba krimu iliyopakwa kwenye magoti yake.
Kozyra pia ni mwalimu mkuu wa Salesian High School ambako inasemekana kitendo hicho  ni utamaduni wa ‘sherehe ya kuwapokea wanafunzi wapya’ kila mwaka.


        
Wanafunzi wakijiandaa kumlamba magoti padri huyo.

Picha hizo zinamwonyesha Kozyra akiwa amekaa kitini na akiwa amevaa kaptura na akiwa na fimbo.

Monday, September 17, 2012

LADY GAGA NA STYLE MPYA YA NYWELE NA KUPIGA TATOO KATIKA KICHWA CHAKE

Muonekano wa Lady gaga katika kichwa chake kabla ajaweka tatoo mpya baada ya kunyoa style yake.
                            Lady gaga akipigwa tatoo mpya katika kichwa chake baada ya kunyoa.
        Muonekano mpya wa Lady gaga baada ya kumaliza kupiga tatoo yake mpya katika kichwa chake
                            Lady gaga na muonekano mpya wa tatoo yake katika Fashion week

MUONEKANO MPYA NA BURUDANI ILE ILE SERENGETI FIESTA MOROGORO BHASSSSSSSS


Nyota wa kizazi kipya katika muziki wa bongo fleva huyu si mwingine ni Ben Pol akionyesha vitu vyake katika stage ya Serengeti Fiesta mkoani morogoro usiku wa kuamkia leo katika viwanja vya jamhuri.
Msanii mwenye miondoko ya pwani huyu si mwingine anajulikana kwa jina la AT akionyesha mambo yake katika jukwaa la Serengeti Fiesta mkoani Morogoro katika viwanja vya jamhuri.
Nyota wa kizazi kipya anayefahamika kwa jina Recho kutoka THT naye alikuwa ni moja kati ya wasanii ambao wametoa burudani ya uhakika kabisa katika tamasha la serengeti fiesta mkoani Morogoro usiku wa kuamkia leo katika viwanja vya jamhuri.

Sunday, September 16, 2012

MPYA YA LEO>>>MSAFARA WA MBIO ZA MWENGE WAPATA AJALI RUKWA, KADHAA WAJERUHIWA NA KUKIMBIZWA HOSPITALI


Gari iliyokuwa imewabeba madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga katika msafara wa Mwenge ambayo ilipinduka jana katika kijiji cha Luwa na kujeruhi vibaya zaidi ya Madiwani watatu, hali iliyosababisha madiwani hao kukimbizwa hospitali ya mkoa mjini Sumbawanga. 

Sudan Kusini yazamisha meli yake yenyewe

Wakuu wa Sudan Kusini wanachunguza sababu ya jeshi kushambulia na kuizamisha meli yao wenyewe kwenye Mto Nile.
Msemaji wa jeshi la Sudan Kusini Kanali Philip Aguer
Wanajeshi kumi walifariki na wengine hamsini wametoweka.
Msemaji wa jeshi la Sudan Kusini, Kanali Philip Aguer, amesema meli hiyo ilipita kituo cha ukaguzi usiku bila ya kusimama ingawa ilitakiwa kusimama.
Alisema meli hiyo ilikuwa imebeba wanajeshi kama 170.


ALICHOSEMA MSTAAFU WA FREEMASONS KUHUSU MKAPA NA MWAI KIBAKI KUWEMO NDANI YA HICHO CHAMA.


Sir Andy Chande.

Kwa longtime sasa hivi Tanzania imeshuhudia magazeti mengi pamoja na stori za internet kwenye blogs, website na facebook kuhusu Freemasons, kwa kiasi kikubwa baada ya hizo habari, picha iliyojengeka kuhusu Freemasons ni kwamba ni dini ya kishetani.
Wametajwa mastaa mbalimbali wa Tanzania pamoja na viongozi wa kisiasa kwamba nao wamejiunga na dini hiyo akiwemo rais mstaafu wa Tanzania William Mkapa na Rais Mwai Kibaki wa Kenya.
Exclusive kwenye THE INTERVIEW ya CLOUDS TV Mtangazaji Gerald Hando amefanya interview na Sir Andy Chande ambae alikua freemasons lakini kwa sasa amestaafu.
Moja kati ya mambo aliyoyazungumzia ni pamoja na taarifa za Kibaki na Mkapa kuwemo kwenye hicho chama, hapa namkariri akisema “Hakuna hata mmoja kati ya mkapa wala kibaki ambae ni Freemason, nilipofika hapa mwaka 1950 katika biashara zangu nilikutana na watu wengi katika Nyanja mbalimbali ambao walikuwa wakiandaa chama cha freemasons ambao walinialika kwenye vikao mbalimbali Uganda, Kenya, uingereza na kwingineko kama Ghana na Khumasi ila nikastafu baada ya miaka 19 kufanya kazi na freemasons.
Sihusiki tena na freemasons huku Tanzania, ila kama uingereza naenda mara kwa mara kwa sababu bado kuna baadhi ya mashirika ninayofanyakazi nayo hadi sasa, Freemasons sio kama watu wengi wanavyosikia au kuambiwa.. kuna tofauti”

JUMA NATURE NI BABA YANGU ILA AMENIKATAA

Kijana huyu nimekutana nae mjengoni ambapo alifika na kudai kuwa yeyey ni mtoto wa msanii Juma Nature na kujitambulisha kama Samson Juma Kassim Kiroboto, Samson anatokea Morogoro na kwa maelezo yake yeye amezaliwa mwana 1995.
"mama yangu ameshafariki na nilishawahi kwenda mpaka kwa baba yangu Juma Temeke nikiwa na bibi yangu, lakini aliponiona tu akanifukuza akasema hataki kuniona tena " hayo ndio yalikua maelezo ya Samson.
unaona kuna kufanana na nature katika picha hiyo?

MIMBA YA JINI KABULA IMEBAKI STORI

 
 Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’.

SIKU chache baada ya kuahidi kumzalia mtoto mpenzi wake aliyemtaja kwa jina la Bushoke, mwigizaji wa filamu Bongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ amedaiwa kupata tatizo la mimba yake kuharibika.
Chanzo chetu makini kilitutonya kuwa, kuharibika kwa mimba hiyo kulibainika hivi karibuni huku mwenyewe akieleza kutojua sababu.
“Mwenyewe anadai hata hajui imeharibika kwa sababu gani lakini ukweli ndiyo huo, kwa sasa hana raha kabisa kwani alishaamua kuzaa lakini ndiyo hivyo tena,” kilidai chanzo hicho.
Katika kupata ukweli wa habari hiyo, mwandishi wetu alimtafuta Jini Kabula na alipoulizwa juu ya mimba yake kuchoropoka alisema kwa masikitiko:
“Naomba unipigie baadaye nitakueleza kila kitu lakini ni ukweli kwamba ‘mwanangu’ ametoka.”