Bw.Anord
Nyabenda akionesha Ulimi wake namna ulivyokatwa kwa meno na mkewe.
Imeelezwa kuwa chanzo ni wivu wa kimapenzi kati yake na mkewe. Hadi sasa
mwanamke hajafika Hospitalini alikolazwa kwa matibabu ili kujulia hali
mwenzake.
Tuesday, July 30, 2013
HIVI NDIVYO KABURI LILIVYO FUKULIWA NA MAITI KUIBIWA
(1) aliyefariki dunia kwa ugonjwa wa malaria, kuibwa na watu wasiojulikana na kaburi lake kuachwa wazi, Uwazi limechimbua.
Kaburi alipozikwa mtoto Sophia Said likiwa wazi.
Tukio hilo la aina yake na lililoacha maswali mengi, lilitokea usiku
wa Julai 20, 2013 kwenye Makaburi ya Buguruni Kwamkanda, Mtaa wa
Mnyamani jijini Dar es Salaam. Marehemu alizikwa Juni 20, 2013.
Uwazi lilifika eneo la tukio na kukuta umati, ikiwemo familia ya Said
ukitokwa machozi huku wakiliangalia kaburi hilo likiwa wazi.
Mbao na miti iliyotumika kwenye mazishi ya mtoto huyo vilikutwa pembeni ya kaburi.
Monday, July 8, 2013
JANUARY MAKAMBA AWATAKA WANANCHI WAWALAUMU WABUNGE WAO KUHUSU KODI YA 1000 KWA KILA LAINI.....ADAI WIZARA YAKE ILIPINGA VIKALI

Haya ni majibu ya Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. January Makamba akijibu maswali katika mtandao wa Twitter kuhusu kodi mpya ya TZS 1000 kwa mwezi kwa kila line ya simu.
- Amesema kwamba Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia iliipinga kodi hiyo.
- Amesema kwamba Hazina (Wizara ya Fedha) walikubaliana na maoni ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kuhusu kodi hiyo.
- Amesema kwamba Bunge ndilo lililopitisha kodi hiyo na si Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.

Friday, June 28, 2013
NDEGE 8 ZA BARACK OBAMA ZATUA DAR ES SALAAM.
DAR ES SALAAM.
MAKACHERO wa Marekani
wameendelea na matayarisho ya mwisho ya ziara ya Rais Barack Obama,
ambapo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere walikuwa na
kazi ya kuunganisha helikopta za doria.
Makachero hao walikuwa wakiunganisha helikopta
sita zilizosafirishwa vipande vipande kutoka Marekani, ambapo meli mbili
za kivita na ndege moja pia zimewasili.
Rais Obama tayari yuko katika ardhi ya Afrika,
ambapo leo anatarajiwa kwenda Afrika Kusini baada ya kumaliza ziara yake
ya kwanza Senegal na anatar
ajiwa kuwasili nchini Jumatatu.
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa jana na
Mwananchi unaonyesha Marekani imeleta helikopta hizo kwa ajili ya ulinzi
wa Rais Obama, zikiwemo meli zilizobeba helikopta nyingine mbili na
ndege.
Habari zilizopatikana kutoka kwa wafanyakazi wa
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,zinasema kuwa helikopta
sita zinaunganishwa katika sehemu ya karakana ya Kikosi cha Anga cha
Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Mpashaji mmoja aliliambia gazeti hili kuwa
helikopta hizo zililetwa kama vipande vipande vilivyosafirishwa kama
mzigo kwenye meli za kivita zilizotia nanga jijini Dar es Salaam.
“Nilikaribia kwenye eneo la karakana na
nikashangaa kuona jinsi jamaa walivyokuwa ‘bize’ wakiunganisha vyuma
mbalimbali na kutengeneza helikopta hizo,” aliongeza mpashaji wetu,
ambaye alibahatika kusogelea eneo hilo licha ya kuwepo kwa ulinzi mkali.
Thursday, June 27, 2013
UJIO WA OBAMA OMBA OMBA WAHAMISHWA JIJINI DAR...
HUU NDIO MKWANJA DIAOMND PLATINUM ALIOUINGIZA MWEZI JUNE NA JULY
Staa
wa Kesho, Diamond ameendelea kupiga hela kwa show nyingi zinazomfuata
kila kukicha. Wingi wa show hizi unazidi kumfanya kuwa miongoni mwa
wasanii wachache wa Tanzania wenye pesa nyingi zaidi.
Tumejaribu kuangalia baadhi ya show alizofanya mwezi huu,
atakazofanya mwishoni mwa mwezi huu na mwezi ujao ili kukadiria ni kiasi
gani anaweza kuwa ameingiza. Baadhi ya show tunafahamu ni kiasi gani
aliingiza huku zingine tukikadiria kutokana na jinsi anavyochaji.
Show ya nchini Comoro 22 June
Friday, June 21, 2013
MABOMU ARUSHA; LEMA NUSURA ATUMBUKIE KWENYE MAFUTA YA KITIMOTO
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.
KUFUATIA mapambano ya raia na Jeshi la Polisi mjini hapa, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), Jumanne wiki hii alilazimika kukimbilia kwa wachoma nyama ya nguruwe karibu na eneo hilo ambapo alidaiwa kunusurika kutumbukia kwenye mafuta ya kiti moto.
Lema aliyenusurika kupigwa na bomu lililoharibu gari lake, alikuwa akijaribu kuwatuliza wananchi walioanza kukusanyika katika vikundi, wakijadili amri ya serikali ya kukataza miili ya watu waliofariki dunia katika shambulio la bomu, isiagwe kwenye Viwanja vya Soweto, mjini hapa.
Kabla ya kupigwa mabomu na kukimbilia kwa wachoma nyama ya nguruwe hao, Lema alikuwa akiwataka wananchi kuwa wavumilivu kwani walikuwa wanawasiliana na serikali ya mkoa ili kupata kibali cha kuaga miili ya wapendwa wao.
Ghafla polisi walifika na kutangaza amri ya watu kutawanyika katika viwanja hivyo ili kuweka hali ya usalama ambapo walisema pasingekuwa na suala la kuaga miili ya watu hao katika eneo hilo. Zoezi hilo lilikwama baada ya mabomu kurindima kwa mara nyingine.
source: Global publishers
Subscribe to:
Posts (Atom)
