MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Rehema Chalamila ‘Ray C’ mwishoni
mwa wiki aliandaa sherehe kujipongeza kutimiza mwaka mmoja tangu aanze
kutumia dawa za ‘methadone’ ambazo zimemsaidia kupona uraibu uliotokana
na matumizi ya mihadarati.
Ray C,aliyabainisha hayo Dar es Salaam juzi, alipokuwa akizungumza
na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (Tamisemi), Jumanne Sigini, alipotembelea Kituo cha Tiba cha Dawa
za Kulevya (Methadone Wing), kilichopo katika hospitali ya
Mwananyamala, Kinondoni.
“Sasa najisikia vizuri na namshukuru baba (Rais Kikwete), kwa
kunishauri pamoja na jitihada zake za kuwaleta Wamarekani katika
kutupatia tiba hii ambayo imenirudisha katika hali yangu ya kawaida,
hadi nikaweza kuingia tena studio kurekodi nyimbo tena, ni jambo kubwa
sana na la kujivunia,” alisema Ray C.