Friday, June 28, 2013

NDEGE 8 ZA BARACK OBAMA ZATUA DAR ES SALAAM.


DAR ES SALAAM.   MAKACHERO wa Marekani wameendelea na matayarisho ya mwisho ya ziara ya Rais Barack Obama, ambapo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere walikuwa na kazi ya kuunganisha helikopta za doria.
Makachero hao walikuwa wakiunganisha helikopta sita zilizosafirishwa vipande vipande kutoka Marekani, ambapo meli mbili za kivita na ndege moja pia zimewasili.
Rais Obama tayari yuko katika ardhi ya Afrika, ambapo leo anatarajiwa kwenda Afrika Kusini baada ya kumaliza ziara yake ya kwanza Senegal na anatar ajiwa kuwasili nchini Jumatatu.
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa jana na Mwananchi unaonyesha Marekani imeleta helikopta hizo kwa ajili ya ulinzi wa Rais Obama, zikiwemo meli zilizobeba helikopta nyingine mbili na ndege.
Habari zilizopatikana kutoka kwa wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,zinasema kuwa helikopta sita zinaunganishwa katika sehemu ya karakana ya Kikosi cha Anga cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Mpashaji mmoja aliliambia gazeti hili kuwa helikopta hizo zililetwa kama vipande vipande vilivyosafirishwa kama mzigo kwenye meli za kivita zilizotia nanga jijini Dar es Salaam.
“Nilikaribia kwenye eneo la karakana na nikashangaa kuona jinsi jamaa walivyokuwa ‘bize’ wakiunganisha vyuma mbalimbali na kutengeneza helikopta hizo,” aliongeza mpashaji wetu, ambaye alibahatika kusogelea eneo hilo licha ya kuwepo kwa ulinzi mkali.

Thursday, June 27, 2013

UJIO WA OBAMA OMBA OMBA WAHAMISHWA JIJINI DAR...

 
KAMA UONAVYO KATIKA PICHA HIVI NDIVYO OMBAOMBA WAKIHAMISHWA MAENEO MBALIMBALI YA JIJINI
DAR KUPISHA UJIO WA RAIS OBAMA

HUU NDIO MKWANJA DIAOMND PLATINUM ALIOUINGIZA MWEZI JUNE NA JULY


Staa wa Kesho, Diamond ameendelea kupiga hela kwa show nyingi zinazomfuata kila kukicha. Wingi wa show hizi unazidi kumfanya kuwa miongoni mwa wasanii wachache wa Tanzania wenye pesa nyingi zaidi.
Tumejaribu kuangalia baadhi ya show alizofanya mwezi huu, atakazofanya mwishoni mwa mwezi huu na mwezi ujao ili kukadiria ni kiasi gani anaweza kuwa ameingiza. Baadhi ya show tunafahamu ni kiasi gani aliingiza huku zingine tukikadiria kutokana na jinsi anavyochaji.
Show ya nchini Comoro 22 June