Tuesday, November 12, 2013

Dk Mvungi Afariki Dunia

Mkurugenzi wa Katiba, Sheria na Haki za Binadamu wa NCCR-Mageuzi, Dk Sengodo Mvungi amefariki dunia leo alasiri nchini Afrika Kusini alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa na watu wanaosadikiwa ni majambazi.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Mwenyekiti Taifa wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia.

Dk Mvungi ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba alijeruhiwa kwa kukatwa na mapanga kichwani Novemba 13, mwaka huu nyumbani kwake Kibamba Msakuzi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na kulazwa Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (Moi) na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya Milpark, Johannesbarg, Afrika Kusini.

Penzi la Kajala Masanja na Petit Man laota mabawa


 

Habari zilizogazaa mtaani zinasema kuwa  penzi la mwanadada Kajala Masanja na Petit Man Wakuache ambaye ni anafanya kazi na Wema Sepetu kwenye kampuni ya Endless Fame Production limeota mabawa na kwa sasa Petit Man anatoka na mdogo wake Vanessa Mdee.

Kwa mujibu wa The Gossip corp wa clouds FM wawil hao hawapo pamoja tena na mwanadada kajala amejaribu sana kumsihi Petit man wakuache warudiane bila mafanikio

Ray C ajipongeza baada ya kuachana na Mihadarati

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Rehema Chalamila ‘Ray C’ mwishoni mwa wiki aliandaa sherehe kujipongeza kutimiza mwaka mmoja tangu aanze kutumia dawa za ‘methadone’ ambazo zimemsaidia kupona uraibu uliotokana na matumizi ya mihadarati.

Ray C,aliyabainisha hayo Dar es Salaam juzi, alipokuwa akizungumza na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Jumanne Sigini, alipotembelea Kituo cha Tiba cha Dawa za Kulevya (Methadone Wing), kilichopo katika hospitali ya Mwananyamala, Kinondoni.

“Sasa najisikia vizuri na namshukuru baba (Rais Kikwete), kwa kunishauri pamoja na jitihada zake za kuwaleta Wamarekani katika kutupatia tiba hii ambayo imenirudisha katika hali yangu ya kawaida, hadi nikaweza kuingia tena studio kurekodi nyimbo tena, ni jambo kubwa sana na la kujivunia,” alisema Ray C.

HUU NDIO MJENGO ANAOPOROMOSHA MSANII DIAMOND KWA SASA

Kijana anayefanya vizuri kwenye muziki wa Bongo Fleva Diamond Platnumz mambo si mabaya kwake baada ya kuonyesha mjengo wake mwingine wa hatari ambao bado upo katika ujenzi


Kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram,Diamond jana ame-share picha ya nyumba hiyo na chini akatia neno..Shuka nayo.

''Toa kitu weka kitu...! Ndio tulivyo funzwa...stareh tunawaachia wajanja wa mji... #WCB #Wasafi for the Fkn Life!''

Haijajulikana mjengo huu uko maeneo gani wala umegharimu kiasi gani ila inaendelea kudhihirisha mafanikio anayoendelea kuyapata Diamond.
 
 
source dj seki 

TAMKO rasmi la Ndugu Zitto Z. KABWE (MB) kuhusiana na kinachoitwa "Taarifa ya Siri ya Chadema"

NILIPOKUWA katika ziara ya bara la Ulaya kati ya Oktoba 21 mpaka Novemba 2 mwaka huu (2013), nilipokea kwa njia ya barua pepe ripoti inayoitwa "Taarifa ya Siri ya Chadema" ambayo pia ilikuwa imesambazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

“Taarifa ya Chadema inasema kwamba chama hicho (chama changu) kilikuwa kimechunguza mwenendo wangu tangu mwaka 2008 hadi 2010 na kubaini kuwa mimi napokea fedha kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kuivuruga Chadema.


Ripoti hiyo ilinihusisha pia na mwananchi raia wa Ujerumani, Andrea Cordes ambaye, kwa mujibu wa ripoti hiyo, alinisaidia kupokea na kuhifadhi kiasi cha dola 250,000 za Marekani kupitia kwenye akaunti yake binafsi.