Tuesday, July 30, 2013

MWANAUME AKATWA ULIMI NA MKEWE KISA WIVU WA KIMAPENZI

Bw.Anord Nyabenda akionesha Ulimi wake namna ulivyokatwa kwa meno na mkewe. Imeelezwa kuwa chanzo ni wivu wa kimapenzi kati yake na mkewe. Hadi sasa mwanamke hajafika Hospitalini alikolazwa kwa matibabu ili kujulia hali mwenzake.

HIVI NDIVYO KABURI LILIVYO FUKULIWA NA MAITI KUIBIWA

 
 
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, familia ya Said Abdallah inayoishi Buguruni jijini Dar es Salaam imelazimika kutokwa machozi upya baada ya maiti ya mtoto Sophia Said
(1) aliyefariki dunia kwa ugonjwa wa malaria, kuibwa na watu wasiojulikana na kaburi lake kuachwa wazi, Uwazi limechimbua.
Kaburi alipozikwa mtoto Sophia Said likiwa wazi.
Tukio hilo la aina yake na lililoacha maswali mengi, lilitokea usiku wa Julai 20, 2013 kwenye Makaburi ya Buguruni Kwamkanda, Mtaa wa Mnyamani jijini Dar es Salaam. Marehemu alizikwa Juni 20, 2013. Uwazi lilifika eneo la tukio na kukuta umati, ikiwemo familia ya Said ukitokwa machozi huku wakiliangalia kaburi hilo likiwa wazi. Mbao na miti iliyotumika kwenye mazishi ya mtoto huyo vilikutwa pembeni ya kaburi.