Miongoni mwa vitu vinavyochangia kuharibu uhusiano wa kimapenzi ni
hisia. Wapenzi wengi wameachana kwa sababu si kwamba walithibitisha
ubaya wa wenzao ila walijijaza wenyewe hisia mbaya na kujikuta
wamepoteza thamani ya kupenda. Hebu angalia hisia nane hatari ili
uzikimbie mapema kabla hazijakuharibia penzi lako.
1. NASALITIWA
Kuishi
katika mapenzi huku ukiwa na fikra kwamba mwenza wako anakusaliti ni
jambo baya kwa vile huathiri msukumo wa ndani wa kupenda. Matokeo yake
utajikuta ukishindwa kutimiza wajibu wako kama mke/mume kwa sababu tu ya
kuendekeza hisia mbaya. Acha kuhisi, tafuta ukweli.
2. TUTAACHANA
Kuna
wapenzi ambao wanaishi na mawazo ya “ipo siku tutaachana”. Wanafanya
hivyo eti kwa kutafsiri mwenendo usioridhisha wa mapenzi yao. Kusema
kweli hili ni jambo baya kwani huondoa ari na kujenga ufa wa mapenzi.
Huwafanya wapenzi kubakia na wazo moja tu, la kutafuta sehemu mbadala ya
kwenda baada ya kuachana. Usiwaze kabisa kuachana hata kama mnagombana
na mwenzako kila siku.
3. SIWEZI MAPENZI
Baadhi ya wapenzi
huwa na hisia kwamba hawayawezi mapenzi. Hata kama hawajaambiwa chochote
kuhusu kutowatosheleza wenza wao faragha hukimbilia kujihukumu.
Hujaambiwa kama umecheza chini ya kiwango, hofu ya nini? Usiwaze hivyo,
kama una lolote linalokufanya uwe na hofu muulize mwenzio.