Wednesday, October 3, 2012

Wachina wanaongoza kwa matukio ila hili limetia fora


WAHIFADHI MWILI WA KIJANA WAO MIAKA 6 KWENYE JOKOFU NCHINI CHINA

 

Tian Xueming akiangalia mwili wa kijana wake katika jokofu.

Nyumba ya Tian Xueming.
NI miaka sita sasa tangu familia ya Tian Xueming raia wa nchini China ianze kuhifadhi mwili wa kijana wao kwenye jokofu.
Mwaka 2006, familia hiyo ilimpoteza kijana wao aliyefariki kwa ugonjwa wa leukemia. Tian Xueming mzazi wa kijana huyo aliamua kuuhifadhi mwili wa kijana wake katika jokofu. Kila mara wanapomkumbuka kijana wao, Tian na mkewe wanakwenda kimyakimya katika jokofu na kuuangalia mwili wa kijana huyo. Tim anasema kuwa "kijana wangu katika jokofu anaonekana kama alivyokuwa enzi za uhai wake. Mwanangu bado yupo pamoja nasi mpaka leo."
Miaka 15 iliyopita, familia ya Tian Xueming ilimpoteza pia binti yao aliyefariki kwa ugonjwa wa moyo. Miaka sita baadaye kijana wao naye akafariki kwa leukemia.


Angalia Rufaa ya LEMA ilivyoahirishwa mahakamani Arusha

DSCN5552 Baadhi ya wananchi waliokusanyika nje ya ofisi za Chadema Mkoa wa Arusha, eneo la Ngarenaro wakimsikiliza Mh Godbless Lema haonekeni pichani mara baada ya kutoka Mahakamani kusikiliza shauri lake kupinga kuvuliwa ubunge. Picha hii ni taswira nusu ya kwanza ya watu
DSCN5541 Mh. GodblessLema akizungumza na kuagana na wananchi waliokuwa nae  Mahakamani, mbele ya ofisi za chama hicho.
DSCN5551 Hii ni nusu nyingine ya taswira halisi za wananchi waliofika ofisini hapo…