Thursday, November 22, 2012

Duh! Kama utani vile: Askofu wa kwanza wa Kike ateuliwa


                               Ellinah Wamukoya
                                                             Ellinah Wamukoya
Ellinah Wamukoya ameteuliwa kuwa askofu wa kwanza wa kike wa kanisa la Kianglikana barani Afrika.
Akiongea muda mfupi baada ya kuteuliwa, Bi. Ellinah Wamukoya amesema uamuzi huo heshima kwa kina mama.
Ellinah Wamukoya, 61, sasa atahudumu kama askofu mpya wa kanisa hilo katika ufakme wa Swaziland, moja wapo ya nchi zinazokisiwa kufuata siasaa za kihafidina.
Kutawazwa kwake kumejiri huku kanisa la Kianglikana, likitarajiwa kujadili ikiwa kina mama wataruhusiwa kuapishwa kuwa maaskofu wa kanisa hilo.
Askofu wa jimbo la Capte Town, nchini Afrika Kusini, amesema kuwa wamechukua uamuzi huo ili wawe mfano kwa wengine na pia kuwatakia, viongozi wa kanisa hilo, faraja na hekima ili kujadilia sauala hilo kwa haraka.
Kwa mujibu wa ripoti aliyotuma kwa vyo,bo vya habari, askofu huyo wa jimbo la Cape Town, Revd. Thabo Makgoba, amesema wimbi kwa sasa linavuma na kuwa wameshuhudia tukio la kihistoria ambao ni sawa na bingu kufunguka.
David Dinkebogile aliongoza sherehe hizo na kukariri kuwa nia yao kuwa ilikuwa kumuapisha askofu na wale sio mtu mweusi, muafrika na raia wa Swaziland.
Askofu Wamukoya ni meya wa zamani wa mji mkuu wa Swaziland Manzini.

Shule ya Msingi Ndonga: Mtihani wa Taifa hubebwa kichwani, Haijawahi kukaguliwa tangu mwaka 1995





share
NI safari ya siku mbili  kutoka mjini Songea makao makuu ya mkoa wa Ruvuma hadi kuweza kuifikia shule ya msingi Ndonga iliyopo wilayani Nyasa mwambao mwa ziwa Nyasa.
Basi linaishia katika mji mdogo wa Liuli, Ziwa Nyasa na kutoka hapo inakulazimu kukodi pikipiki hadi katika kijiji cha Njambe kata ya Kihagara ambapo ndiyo mwisho wa usafiri wa pikipiki na kuanzia hapo inakulazimu kutembea kwa miguu kwa takribani saa moja hadi kukifikia kijiji cha Ndonga!
Shule ya msingi Ndonga imejengwa juu ya mlima wa Liwundi, unapofika katika kijiji cha Ndonga inakulazimu kupanda mlima wenye mwinuko mkali wenye makorongo kwa takriban zaidi ya saa moja hadi kufika kileleni ndipo unakutana na shule hii.
Asilimia 90 ya wanafunzi wanaosoma katika shule ya msingi Ndonga wanaishi chini ya mlima hivyo inawalazimu kwa siku tano yaani Jumatatu hadi Ijumaa kupanda  na kushuka mlima kwa saa mbili hali ambayo imesababisha shule hiyo kukabiliwa na utoro uliokithiri wa wanafunzi ambao unafikia kwa siku kati ya asilimia 60 hadi 70.
Wanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi Ndonga wilayani Nyasa mkoani Ruvuma wakisomea darasa ambalo halijaezekwa kwa mwaka mmoja sasa mvua na jua vikiwakabili

Wednesday, November 21, 2012

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam Yatoa Hukumu Ya Kunyogwa Hadi Kufa Watuhumiwa Wa Mauaji ya Swetu Fundikira

 Marehemu Swetu Fundikira enzi za uhai wake.
 
Watuhumiwa waliohukumiwa kifo kutokana na mauaji ya Fundikira MTM 1900 Sajenti Roda Robert(42) wa kikosi cha JKT-Mbweni na MT 75854 Koplo Ally Ngumbe (37) wa JWTZ-Kunduchi
--
 WATUHUMIWA katika mauaji ya Swetu Fundikira,  MTM 1900 Sajenti Roda Robert (42) wa kikosi cha JKT - Mbweni na MT 75854 Koplo Ally Ngumbe (37) wa JWTZ-Kunduchi leo wamehukumiwa kifo baada ya kupatikana na hatia na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.Habari zaidi Baadae

SABABU ZA ZITTO KABWE KUANDIKA KWAMBA “TUSIGEUZWE MAZEZETA, MABWEGE NA MAZEZETA HUIMBA KILA WANACHOAMBIWA” SOMA ZAIDI HAPA

 
.
Mabilioni ya Uswisi – Tusigeuzwe Mazezeta
Jumanne tarehe 20 Novemba 2012, baadhi ya vyombo vya habari vimebeba habari zinazohusu matamshi ya Waziri wa Utawala Bora ndugu George Mkuchika kuhusu sakata ya mabilioni ya Uswisi. Waziri amesema kwamba Serikali ya Uswisi inataka majina ya Watanzania walioficha fedha huko ndio waweze kusaidia uchunguzi. Habari kama Hiyo, yenye maudhui na malengo hayo hayo iliandikwa na Gazeti la The Guardian on Sunday la tarehe 18 Novemba 2012.

KERI HILSON SOON KUPIGA SHOW KALI TANZANIA NA KENYA

Msanii mahiri kutoka pande za state almaarufu kama Keri Hilson anayetamba na ngoma kali kama That way you love me,Pretty girl Rock na ngoma nyinginezo kali,mpaka kupelekea mashabiki kumkubali katika tasnia ya muziki.Sasa latest info ambayo tumeipata kutoka kwa msanii huyu ni kwamba leo asubuhi aliamua kuandika katika ukurasa wake wa twitter kwamba mwezi wa Desemba itakuwa ni mara yake ya kwanza kupiga show kali hapa Tzee na kenya.