Thursday, January 10, 2013

Ni utata mtupu juu ya kifo cha Jackline Musa Matiko aliyekutwa kafia hotelini

                           
UTATA mkubwa umegubika kifo cha mwanafunzi Jackline Musa Matiko (15) aliyekuwa akisoma katika Shule ya Sekondari Juhudi iliyopo Gongo la Mboto Wilaya ya Ilala aliyekutwa amekufa katika Hoteli ya Southern Resort, Kigamboni Dar es Salaam baada ya wazazi wake kudai kuwa hakufa maji bali alinyongwa.

Akizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita, baba wa marehemu, Mussa Matiku alisema baada ya kuikuta maiti ya mtoto wake kando ya bwawa katika hoteli hiyo na kuichunguza shingo yake aliiona imelegea na tumbo lake halikujaa maji kama watu wanaokufa kwa maji wanavyokuwa.
Alisema kwa vigezo hivyo ni wazi kwamba mwanaye hakufa maji na amelitaka jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina ili kuwabaini waliomuua kikatili binti yake.
 Naye mjomba wa marehemu ambaye alikuwa na Jackline kabla ya kifo chake aliyejitambulisha kwa jina moja la Abdul, alisema  binti huyo alitoka nyumbani kwa wazazi wake maeneo ya Mazizini Ukonga kwenda Gongo la Mboto kwa bibi yake kusherehekea Sikukuu ya  Mwaka  Mpya.

“Baada ya kufika pale na kupata chakula cha mchana pamoja  na ndugu zake, Ilipangwa kwenda  kutembea kokote walikohitaji ambapo walichagua  kwenda Quality Centre.

WACHINA WAZUIA UPANUZI WA BANDARI YA DAR

 
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe.  

* Waziri Dk. Mwakyembe, Jaji Werema wageuziwa kibao,washitakiwa
WIKI hii kona ya Fumuafumua ilizama bandarini Dar es Salaam na kugundua kuwa shughuli za upanuzi wa bandari kama serikali ilivyokusudia imekwama na kuwa ni ndoto kwa wakati huu.
 
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema.
Hata hivyo, katika dodosadodosa yetu tumegundua kuwa kuna kesi ambayo imefunguliwa na imezuia muendelezo wowote wa upanuzi wa bandari hiyo ili iwe ya kisasa zaidi.
Imegundulika pia kuwa Kampuni moja ya Kichina iitwayo China Communications and Constraction (CCC) ndiyo iliyoenda Mahakama Kuu, kitengo cha biashara na kuzuia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutangaza zabuni ya upanuzi wa bandari hiyo.

Boda boda yaleta timbwili kwa wapendanao MORO

Chanzo chetu hivi karibuni kikiwa kwenye duka la kuuza pikipiki lililopo Mtaa wa Mindu barabara ya kueleka Faya Manispaa ya Morogoro, lilishuhudia pikipiki nyingi zikiwa zimeandikwa ujumbe tofauti.
Kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Sule Manga akiwa juu ya pikipiki yake iliyoandikwa maneno yanayosomeka: “Usijisifu una mimba, msifu aliyekutia mimba hiyo” alipoulizwa sababu ya kuandika hivyo alifunguka:

Tuesday, January 8, 2013

KANISA LA AJABU LINALOPINGA BIBLIA TAKATIFU LATUA TANZANIA

Kanisa hilo ambalo linajulikana kwa jina la The Pool of Siloam lililoko Mbezi- Makonde, Kinondoni, Dar es Salaam linafanya ibada zake Jumanne badala ya Jumapili wakiamini ndivyo Neno la Mungu linavyotaka.

Jambo lingine ambalo linachagiza u-ajabu wa kanisa hio…

KANISA lingine la ajabu limegunduliwa Bongo ambapo linafanya ibada zake kwa utofauti mkubwa na makanisa yaliyozoeleka na wengi, Uwazi limechimbua.
                        

PICHA ZA WEMA SEPETU ZIMEMAKE HEADLINE MITANDAO YA JAMII

 
Ikiwa ni mda mchache tu baada ya kupost picha zake zenye kuonyesha wazi sehem za tumbo na kifua kupitia Instagram, picha ya wema imeonekana kusambaa kwa haraka zaidi kupitia mtandao wa jamii "facebook" huku kila mmoja akitoa maoni yake kutoka na mtazamo wake.