Thursday, January 10, 2013

Boda boda yaleta timbwili kwa wapendanao MORO

Chanzo chetu hivi karibuni kikiwa kwenye duka la kuuza pikipiki lililopo Mtaa wa Mindu barabara ya kueleka Faya Manispaa ya Morogoro, lilishuhudia pikipiki nyingi zikiwa zimeandikwa ujumbe tofauti.
Kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Sule Manga akiwa juu ya pikipiki yake iliyoandikwa maneno yanayosomeka: “Usijisifu una mimba, msifu aliyekutia mimba hiyo” alipoulizwa sababu ya kuandika hivyo alifunguka:

“Pikipiki hii nimeinunua hivi karibuni na hili pepe nililichora tangu jana nikiwa na sababu maalumu, nilikuwa na demu wangu ambaye nilimtia mimba, juzikati kaniaga anakwenda kwao Tanga, chaajabu aliporudi amekata mawasiliano na mimi huku akijisifu kwa watu kwamba ana mimba bila kunisifu mimi niliyempa mimba hiyo,” alisema Manga na kuongeza:
“Nikimpigia simu hapokei, hivyo kuanzia juzi niliamua kuachana naye kwa sasa naelekea nyumbani kwao na pikipiki hii, nikifika naipaki  jirani na nyumba yao kwa lengo la kutaka yeye na familia yake akiwemo mama yake mzazi wasome meseji hii…nasikia kambambikia mtu mwingine mimba yangu,” alisema.
Hata hivyo,  hakuwa tayari kumtaja mwanamke huyo anayedai kuwa na mimba yake. Pikipiki nyingi mjini hapa zimeandikwa maneno ya mafumbo kama yanayoandikwa kwenye khanga.

No comments:

Post a Comment