MTOTO Ashura Mustafa mwenye umri wa miaka minne (pichani), mkazi wa
Kijiji cha Mwandege wilayani Mkurunga, Mkoa wa Pwani, yupo katika mateso
makubwa kutokana na vidonda vilivyomtoka mwilini na baba yake hana
uwezo wa kumgharamia matibabu.
Baba wa mtoto huyo, Mustafa Mohamed, ana haya ya kusema: “Mtoto wangu alianza kuumwa akiwa na mwaka mmoja baada ya kuzaliwa mwaka 2007. Vidonda hivi vilianza vikiwa ni malengelenge na nimehangaika naye katika hospitali nyingi mpaka nikafika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
“Madaktari Muhimbili walinipa barua ya kwenda CCBRT ambako wataalamu waliniambia kuwa mtoto wangu huyu ana tatizo la saratani ya ngozi, ‘stage 4’. Nikaambiwa mtu akiwa na saratani hatua hiyo, vidonda vyake huchukua muda mrefu kupona.
“Ilitakiwa afanyiwe upasuaji lakini ikabainika kuwa hana damu ya kutosha, akapewa chupa mbili za damu lakini baada ya miezi miwili akapungukiwa tena. Akaongezewa tena chupa mbili lakini kabla ya kufanyiwa upasuaji, daktari aliyekuwa akimtibu CCBRT tukaambiwa amekwenda likizo, hivyo tukarudi nyumbani ambako yupo hadi sasa.
“Mtoto wangu ana hali mbaya kwa kuwa anakaa ndani tu tena kwenye neti kukwepa vumbi na inzi, anateseka sana. Naomba msaada kutoka kwa wasamaria kwani sina kazi na kila tunapompeleka hospitali ni lazima tukodi gari. Hali aliyonayo hatuwezi kusafiri naye kwa daladala.
“Aliyeguswa na mateso ya mwanangu awasiliane nami kwa simu namba 0769517765, 0715424607,” alisema Mustafa kwa masikitiko.

No comments:
Post a Comment