Misemo


Misemo na Bervone:
Ø Ukiona darasani natega lakini mtihani nakushinda usikasirike.
Ø Maadui zangu wana kismati cha paka kupendwa na wachawi.
Ø Siyo tabasamu zote za halisi, zingine za bandia
Ø Yatima hadekezwi.
Ø Hata maji machafu yanazima moto.
Ø Aibu ya maiti aijuaye muosha.
Ø Chura anapenda maji lakini siyo ya moto.
Ø Ukiona manyoya ujue kaliwa.
Ø Kobe hapimwi malaria.
Ø Siku zote mwiba hutokea ulipochomea.
Ø Umezoea kusomewa taarifa za habari, hujazoea kusomewa habari za misiba.
Ø Kujitetea kwenye uongo ni sawa na kibaka kutafuta msaada wa polisi.


No comments:

Post a Comment