Thursday, July 5, 2012

Imezuka tabia ya kuzika watu wakiwa hai mkoani Mbeya

      KUMEZUKA vitendo vya unyama mkoani Mbeya vya kuzika watu wanaotuhumiwa kuwa ni washirikina wakiwa hai ambapo hivi karibuni watu wawili akiwemo mwanamke mmoja wamefanyiwa unyama huo.
Mwanamke aliyezikwa akiwa hai kwa tuhuma za kujihusisha na ushirikina ni Rozina Mwadala (60) ambapo tukio hilo lilitokea Juni 2, mwaka huu.

       Mwanamke huyo alichukuliwa hatua hiyo baada ya kifo cha mmoja wa ndugu yake ambaye alifariki muda mchache baada ya kulalamika kuwa alikuwa akiumwa sikio na kichwa. Hata hivyo, hakukuwa na mtu yeyote aliyekuwa tayari kuhojiwa na mwandishi wetu kwa hofu ya kukamatwa na polisi.
Kufuatia vitendo hivyo kushika kasi mkoani Mbeya, Mwenyekiti wa Muungano wa Jamii Tanzania (Mujata), Chifu Soja Masoko, amewaonya wananchi wa Kijiji cha Malamba, Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya kuacha mara moja tabia za kujichukulia sheria mikononi alipokuwa akiwahutubia katika mkutano wa hadhara Juni 15, mwaka huu.

       “Hasara yake mnaona. Sasa kufuatia kitendo hicho cha kikatili baadhi ya wananchi wamehama kijijini hapa kukwepa mkono wa sheria na shughuli za kiuchumi zimezorota,” alisema.
Mbali na mwanamke huyo kuzikwa hai, hivi karibuni mwanaume mmoja, Nyerere Kombwee naye alizikwa hai baada ya kutokea kifo cha mdogo wake kisha yeye kutohudhuria msibani ndipo wananchi wakamsaka na walipompata wakampiga na yeye akatoa vitisho kuwa damu yake isingeweza kwenda bure ndipo wakaamua kumzika akiwa hai.

Mama Ulimboka asema anamuachia MUNGU

 Mama mzazi wa Dk. Steven Ulimboka.

Dk. Steven Ulimboka.

          KUFUATIA tukio la mwanaye ‘kusulubiwa’ wiki iliyopita, mama mzazi wa Dk. Steven Ulimboka ambaye hakutaka jina lake lipambe ukurasa huu, alisema kuwa anashukuru Mungu kwa kwenda kumuona mtoto wake na kumkuta akiwa hai.
Baada ya kumuona mwanaye akipatiwa matibabu kwenye Taasisi ya Mifupa Moi katika Hospitali ya Muhimbili, Dar, mama huyo alisema tatizo lililompata mwanaye anamwachia Mungu kwani ndiye mwamuzi wa uhai wa kila mtu hapa duniani.
“Namwambia Mungu asante kwa kuwa nimemkuta yupo hai. Kwa jinsi nilivyopata taarifa niliamini mwanangu amefariki dunia japo hali yake si ya kuridhisha,” alisema kwa uchungu.
Jumamosi mchana, Dk. Ulimboka alisafirishwa kupelekwa Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu kufuatia kubainika kuwa ubongo wake ulikuwa umetikisika.
Dk. Ulimboka alitekwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia Jumatano wiki iliyopita katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni ambapo alipigwa vibaya na kwenda kutupwa kwenye msitu wa Pande nje kidogo ya jiji.
Tukio hilo limekuwa ndiyo habari ya mjini kwa sasa kwani lilitokea katika kipindi ambacho madaktari wapo kwenye mgomo huku Dk. Ulimboka akiwa ndiye kiongozi wa jumuiya yao.

Irene Uwoya akiri kuacha gambe baada ya kuona anapoteza muelekeo

 Irene Pancras Uwoya katika picha

      MWIGIZAJI Irene Pancras Uwoya amekula kiapo mbele ya Ijumaa Wikienda kuwa hataki kuonja pombe tena kwani anakiri zimempotezea mwelekeo kwa kumharibia vitu vyake vingi.
Akizungumza na mwandishi wetu jijini Dar juzikati, Uwoya ambaye ni mke wa ndoa wa mwanasoka wa Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Kataut’, alisema amegundua kuwa pombe haina faida kwake.
Tujiunge na Uwoya: “Mbali na kupoteza fedha nyingi lakini wakati mwingine nashindwa kutimiza ratiba yangu na hasa nikiwa na ‘apointimenti’ muhimu nashindwa kuitimiza kwa sababu ya pombe kwa hiyo natangaza rasmi kuacha na nawasihi wasanii wenzangu nao waache.”

Chuzi na mpenzi wake Rose wa Chuz wamwagana

 Chuz mwenyewe katika picha

 Rose wa Chuz katika Picha
 
       HATIMAYE ule uchumba wenye makeke wa Mkurugenzi wa Chuz Entertainment, Tuesday Kihangala ‘Chuz’ na msanii wa kundi hilo, Rose Michael ‘Rose wa Chuz’ umekatika na wawili hao wamemwagana, Risasi Mchanganyiko lina ushahidi mkononi.

        Kwa mujibu wa chanzo chetu, wawili hao wamemwagana kufuatia timbwili zito aliloliangusha Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ nyumbani kwa Chuz hivi karibuni akimtuhumu demu huyo kumtesa mwanaye wakati baba mtu alipokuwa Zanzibar ‘Zenji’ akirekodi filamu ya Dirty Game.
Habari zinasema baada ya Chuz kurejea kutoka Zenji, Rose alitoa dukuduku lake kwamba, hawezi kuendelea kulea ‘toto ambalo’ mama yake hana shukurani.

       “Kisa cha hawa watu kumwangana ni Jini Kabula, Chuz alikwenda Zenji kushuti filamu, aliporudi akakuta Rose amevimba macho kwa kulia, alipoulizwa kasema Jini Kabula alimfanyai fujo akimtuhumu kumtessa mwanaye.
“Chuz alijaribu kumlainisha Rose kwa maneno ‘matamtam’ lakini hakukubali, akaondoka kurudi kwao Arusha, hivi leo (juzi, Jumatatu) ninavyoongea na wewe, Rose yupo Arusha kwa wazazi wake,” kilisema chanzo hicho.
Paparazi wetu alimsaka Chuz kwa simu ya kiganjani na alipopatikana na kusomewa mashitaka yake, alikuwa na haya ya kusema:
Chuz: Aaah! Kifupi ni kwamba, ‘asa hivi mi naangalia kazi bwana. Unajua filamu za Bongo zinauza sana, lakini hata hivyo, tumejitahidi kuwa kama Wanaijeria, si eti?”

      Risasi Mchanganyiko: Jibu swali langu, ni kweli umemwagana na Rose?
Chuz: Rose yupo, unajua yule demu (Rose) atakuja kuwa staa mkubwa sana haba Bongo, mi nakwambia. Anajua kuuvaa uhusika katika filamu. Ha! Ha! Ha! Ha!
Rose alipopigiwa simu siku ya Jumatatu iliyopita hakuweza kupatikana mara moja hewani.
Mapema mwaka huu, moja ya magazeti ya Global Publishers liliripoti Chuz kutangaza hadharani kwamba Rose ni mchumba wake na wangefunga ndoa katikati ya mwaka huu. Aliongeza kuwa msichana huyo ndiye mwanamke wa maisha yake baada ya wote waliopita.

      Hata hivyo, Gazeti la Amani likaja andika habari zilizotoka kinywani mwa Jina Kabula akimuasa Rose kuwa makini na Chuz kwamba katika wanaume waongo ulimwenguni, jamaa huyo anashika nafasi ya pili.
Mbali na Rose, Chuz ameshawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wasanii wa filamu, Jacqueline Pentzel ‘Jack wa Chuz’, Joan Mutovolwa, Leila Ismail ‘Lilly’ (amezaa naye) Miriam Jolwa Jini Kabula (amezaa naye).

Lulu achimba mkwara mzito mahakamani

 
MSANII maarufu wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amechimba mkwara mzito katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu jijini Dar es Salaam. 
       Lulu ambaye ni mshukiwa namba moja wa kifo cha msanii mwenzake, marehemu Steven Kanumba, alichimba mkwara huo, juzi Julai 02, mwaka huu wakati akifikishwa mahakamani hapo, kesi yake inapoendeshwa.

ATEMA CHECHE
Baada ya Lulu kushuka katika gari la Magereza na kusindikizwa kwenda kizimbani na askari Magereza, alianza kumshambulia mwandishi wetu kwa maneno alipomuona amekazana kupata picha zake.
“Hivi hamchoki kunifuatafuata? Kila siku Lulu, Lulu niacheni na maisha yangu! Kwani kuna kitu gani kipya tena?
“Hivi nyie hamna kazi nyingine ya kufanya...baba mzima unahangaika kunifuatilia? Nimechoshwa na tabia yenu bwana,” alibwatuka Lulu bila woga.

ASKARI WAPIGWA NA BUTWAA
Wakati Lulu akitema cheche, askari waliokuwa ‘wakimueskoti’ walibaki wamepigwa na butwaa bila kuamini kama ni kweli Lulu ndiye aliyekuwa akizungumza kwa ujasiri mkubwa kiasi kile.
Mdau mmoja aliyekuwepo mahakamani hapo, alisikika akisema: “Mh! Mwanzoni Lulu alikuwa analia kila siku, lakini sasa naona ameanza kuzoea...amekuwa mbogo huyo!”

KESI YAKE NENDA RUDI
Kesi ya Lulu imeonekana kuwa na mvutano mkubwa huku matumaini ya kuanza kusikilizwa yakionekana kuwa hafifu kutoka na shauri hilo kuendeshwa katika mahakama mbili tofauti.
Awali, Mwendesha Mashitaka wa kesi hiyo, Elizabeth Kaganda, mbele ya Hakimu Agustina Mbando alisoma kesi hiyo lakini kabla ya mtuhumiwa hajajibu chochote, hakimu aliihairisha kesi hiyo.
Hakimu Mbando alisema, analazimika kuhairisha kesi hiyo hadi Julai 16, mwaka huu kwa vile shauri hilo halijakamilika kwa sababu lipo Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam ikijadiliwa suala la umri.
Hata hivyo, mahakama kuu ilipeleka shauri hilo katika mahakama ya rufaa baada ya mawakili upande wa serikali, kupinga suala la umri wa Lulu kujadiliwa mahakamani hapo, badala yake lipelekwe katika mahakama ya rufaa.
Mawakili hao walisema, kwa sasa Lulu atabaki kujulikana kuwa ana umri wa miaka 18, ambao aliandikisha yeye mwenyewe katika Kituo cha Polisi Oysterbay alipokuwa akihojiwa kwa mara ya kwanza baada ya kukamatwa.

NDUGU, WASANII WAMTOSA
Aidha, siku hiyo hakukuwa na ndugu yeyote wa Lulu wakiwemo wazazi wake aliyefika mahakamani hapo kufuatilia shauri hilo.
Ukiachilia mbali hao, hata wasanii wenzake ambao wana jumuiya mbalimbali kama Bongo Movie na Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) pia hawakufika kumuona mwenzao.

KUMBUKUMBU MUHIMU
Lulu alikamatwa Aprili 07, mwaka huu kwa madai ya kuhusika na kifo cha marehemu Kanumba, kilichotokea nyumbani kwake, Sinza - Vatican, jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia siku hiyo.
Kwa sasa yupo katika Gereza la Segerea huku kesi yake ikiendelea kuunguruma katika mahakama mbili tofauti; Hakimu Mkazi, Kisutu na Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam.

Barua aliyoandikiwa Rais Kikwete kutoka Marekani

Dear President Kikwete,
I am writing to express my deep dismay that Tanzania has permitted the National Iranian Tanker Company (NITC), to reflag at least 6 and as many as 10 of its vessels under the Tanzanian ship registry, allowing them to remain under NITC ownership and continuing to transport Iran’s crude oil exports. This action by your government has the effect of assisting the Iranian regime in evading U.S. and EU sanctions and generating additional revenues for its nuclear enrichment and weapons research programs and its support for international terrorism.

It is profoundly disappointing to me to learn that your government has acted in contravention of the broad international coalition that is working together to use peaceful means, including economic sanctions, to change the threatening behavior of the Iranian regime. The decision to accept the re-flagging of NITC vessels casts a shadow over Tanzania’s international reputation.

I respectfully request that Tanzania cancel the re-flagging of the NITC vessels. Given the close and cooperative relationship that our two governments now enjoy, it would be unfortunate if this action were permitted to stand.

It would be preferable that Tanzania take this action of its own accord. However, your government should take note of President Obama’s Executive Order 13608, signed May 1, 2012, which provides for the imposition of sanctions on any entity worldwide, including foreign governments, that assists Iran in evading U.S. sanctions. In my view, reflagging Iranian oil tankers falls within the scope of sanctionable activity under that Executive Order. In addition, if Tanzania were to allow Iranian vessels to remain under Tanzanian registry, we in the Congress would have no choice but to consider whether to continue the range of bi-lateral U.S. programs with Tanzania.

Sincerely,

Howard Berman
Ranking Democrat, House Foreign Affairs Committee