Friday, August 3, 2012

BADO SIKU 140 KUFIKIA MWISHO WA DUNIA



Mfuasi wa Freemason.


 
                        Yesu feki.

ZIKIWA zimebaki siku 140 tu kufikia Desemba 21, 2012 ambapo ilitabiriwa kuwa ndiyo mwisho wa dunia, wasiwasi umeongezeka miongoni mwa jamii huku baadhi ya wanasayansi wa Magharibi wakisisitiza kuwa siku hiyo haitapita.
Baadhi ya imani kama ya Kikristo wao wanasikitika kuwa kama ni kweli, basi tukio hilo litatokea siku 4 kabla ya sikukuu ya kuzaliwa mkombozi wao, Yesu Kristo ‘Krismasi’, Desemba 25.
Wengi waliozungumza na chanzo chetu walionesha dhahiri hofu yao juu ya mwisho wa dunia wakisema haiingii akilini wala hawapati picha itakavyokuwa.
MWISHO WA KISAYANSI NA KIIMANI

Malawi yakataa madai ya Tanzania

Tanzania yaitaka Malawi kusitisha utafiti wa gesi na mafuta mpakani
Malawi imekataa kuitikia wito wa Tanzania kutaka isimamishe shughuli za kutafuta mafuta na gesi ziwa Malawi, wakati suluhu ya mvutano wa mpaka ikisubiriwa.
Mvutano wa maneno umezuka kati ya nchi hizo mbili baada ya Malawi kuipa leseni Kampuni ya Uingereza kufanya utafiti katika eneo hilo.
Maafisa nchini Tanzania wanasema mvutano huo uliodumu kwa miaka 50 sasa unaweza kuwa mkubwa iwapo ugunduzi wa mafuta na gesi utatokea kwenye ziwa hilo linalojulikana kama Ziwa Nyasa nchini Tanzania.
Tanzania inasema inaendelea kufanya mazungumzo na Malawi na iko Tayari kulipeleka suala hilo kwenye vyombo vya upatanishi.
"Hili ni suala nyeti sana na tungependa litatuliwe kwa maelewano, tutaendelea na mazungumzo," Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania alisema.

Wednesday, August 1, 2012

AVIMBA MGUU, AENDA KUOMBEWA

 Hujafa hujaumbika, ni kauli iliyotolewa mama aliyejitambulisha kwa jina la Jacqueline Chema ambaye alikutwa hivi karibuni na chanzo chetu katika Kanisa Kuu la Huduma ya Maombezi linaloongozwa na Nabii Flora Peter lililoko Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam.
Jacqueline au Jack, mama mwenye mtoto mmoja alisema tatizo alilonalo lilimuanza mwaka 2004 na kuanza kutafuta msaada katika hospitali mbalimbali ikiwemo ya magonjwa ya saratani, Ocean Road ya jijini Dar es Salaam.
Jack alikuwa na haya ya kusema: “Nimehangaika sana baada ya kuanza kuugua mguu huu mwaka 2004. Nilianza kuumwa homa kali mara kwa mara baadaye ukaanza kuvimba hapa (akaonesha mguu). Sielewi nini kimesababisha tatizo hili.
“Nimekwenda katika hospitali nyingi kupata tiba na nikafika Ocean Road lakini sijapona. Nikaamua kuja kufanyiwa maombi katika kanisa hili. “Kuumwa kwangu kumeniharibia ratiba zote za maisha yangu. Siwezi kufanya kazi yoyote na hata kuzaa.

Dk. Steven Ulimboka sio wa kupona leo wala kesho



Dk. Steven Ulimboka.
Hali ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka, inaendelea vizuri lakini si wa kupona leo wala kesho, imeelezwa na vyanzo vyetu.
Dk.Ulimboka anayetibiwa Afrika Kusini, yupo chini ya uangalizi mkali wa madaktari katika hospitali aliyolazwa na wanafanya kazi kubwa kuhakikisha anapona.
Chanzo chetu kimetoa taarifa kuwa, Dk. Ulimboka anapata matibabu sahihi kwa sababu hospitali aliyolazwa ni ya uhakika.
Awali, kabla ya mazungumzo ya moja kwa moja kwenye simu, ripota wetu alimtumia SMS mtoa habari wetu kumuulizia maendeleo ya daktari huyo naye akajibu: “He’s recovering slowly.” (Anapona taratibu).

China swimmer Ye Shiwen smashes record, draws doping speculation

 

YE Shiwen


When Chinese swimmers started blowing rivals out of the water in London's Olympic pool, whispers quickly followed. Is China cheating the sport again, as it did in the 1990s, when drug-fueled, muscle-bound swimmers emerged from nowhere to beat the world? Alain Bernard, the 2008 Olympic freestyle champion from France, was among those who wondered.

Sunday, July 29, 2012

Jacqueline Patrick atupia tena zingine chafu

 MLIMBWENDE mtata Bongo, Jacqueline Patrick, kama kawa, amedondosha picha nyingine chafu kwenye ‘peji’ yake ya mtandao wa BBM, chanzo chetu kina ‘fulu’ data.
Jack ambaye ni mke wa mfanyabiashara Abdulatif Fundikira alitupia picha hizo Julai 25, mwaka huu huku akizisindikizia na ujumbe usemao ‘sina tatizo na mtu na mwenye macho haambiwi tazama.’

Machangu walambishwa viboko jijini DAR

Machangu wamekiona cha mtemakuni! Wakati Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ukiwa katika chungu cha nane, akina dada wanaofanya biashara haramu ya kuuza miili maarufu kama Machangudoa au Chipsi Funga au Wauza Sukari Tamu, wamekula viboko laivu baada ya kutuhumiwa kuwatega Waislamu.
Tukio hilo lilijiri katikati ya wiki hii ambapo vijana wa Kiislamu waliodai ni wa kikundi cha Jumuiya ya Uamsho Tanzania Bara walizunguka mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam na kuwashushia fimbo machangu ambao kwa sasa wametapakaa kila kona jijini.

WATUMIA BAJAJ
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, waumini hao, wakiwa wamevaa kanzu huku wakitembea na bakora mkononi walichukua jukumu la kukodi Bajaj na kuzunguka maeneo mbalimbali jijini inapofanyika biashara hiyo haramu ya ukahaba.
BARABARA YA SHEKILANGO
Vijana hao waliolenga kukomesha biashara hiyo hasa kipindi hiki cha mfungo walianzia kwenye Barabara ya Shekilango inayokatiza kwenye viunga vya Sinza, Dar ambapo kila kituo cha daladala kuanzia Afrika Sana hadi kwenye mataa ya Shekilango waliwakuta machangu na kuwatandika viboko kabla ya kutua mitaa ya Mwenge.

Chukua Tahadhari mapema Ebola yazuka tena Uganda

Virusi vya EbolaBaada ya tetesi za majuma kadha, serikali ya Uganda na Shirika la Afya Duniani, WHO, wamethibitisha kuwa ugonjwa wa Ebola umeibuka magharibi mwa nchi.
Watu kama 13 wamekufa na wengine kadha wanauguwa ugonjwa huo katika wilaya ya Kibaale.
Chanzo cha ugonjwa huo safari hii kingali kinachunguzwa.
Virusi vya Ebola havina dawa wala chanjo ya kinga, na kati ya ishara zake ni homa, kutapika, na kuhara.
Ugonjwa huo ulizuka Uganda miaka 12 iliyopita, na kuuwa watu zaidi ya 200.