Friday, June 15, 2012

Kwanini uvumilie mateso ukidhani ndio mwisho wa maisha?


Sio lengo langu kuwafundisha wanawake namna ya kuachana na wapenzi au waume zao. Lakini hebu fikiria kwamba kila wakati wanandoa au wapenzi wako kwenye vita. Hakuna amani, hakuna masikilizano. Kutwa nzima mtu anawaza kuhusu uhusiano wake mbaya hadi anashindwa hata kufanya kazi. Je, hali kama hii ina maana kwa mtu kuendelea kuwa kwenye ndoa?

Hapa nazungumzia wale ambao wanashindwa kutoka kwenye uhusiano, ambao wanajua kabisa kwamba, unawatesa na kuwaumiza. Kuna sababu nyingi kwa nini watu hawa wanashindwa, lakini nyingine zinatokana tu na kutojua namna ya kutoka, sio utegemezi wa aina yoyote.
Moja ya sababu, ambazo ninaziona sana hasa kwa wanawake ni kujali jamii itasemaje. Mtu anaona kabisa uhusiano haufai na anatamani kutoka . lakini anajiuliza, hivi watasemaje? Kuna wakati ndugu wanamwambia, yeye ndiye mkorofi. Kama hii ndio sababu anachotakiwa kufanya mwanandoa ni kuhakikisha kwamba anajifunza kuishi kama yeye. Nijuavyo mimi, hata wanandugu au jamii hata ikisema vipi, anayeumia au kuepuka kuumia au kuuawa ni yule aliye kwenye mateso ya ndoa
Jambo la kujiliza hapa ni kama, jamii ndiyo inayopigwa, kutukanwa, kutelekezwa au kudhalilishwa? Lakini jambo kubwa zaidi la kufahamu ni kwamba mtu alishaolewa maana yake ni mtu mzima mwenye haki ya kuamua juu ya maisha yake. Akisubiri ndugu wamwamulie, basi huyo bado ni mtoto..
Jambo lingine ni lile la, je nikimwacha nitapata mwingine? kwani wanaume siku hizi ni shida sana? Ni ujinga unaowafanya wengi kuuliza swali hilo. Unahitaji mwingine wa nini? Unahitaji mwingine ili maisha yako yawe ya maana zaidi au? Kama hakuna mwingine ni vyema kwa sababu maana yake ni kwamba hakuna mwingine wa kukutesa. Lakini wanasaikolojia wanaamini kwamba, ‘kila bidhaa ina mnunuzi.’ Kama unataka mwingine, hata ukiwa na miaka sitini utampata. Huwezi kumpata wakati ukiwa ndani ya tanuru la mateso. Ni lazima utoke kwanza.
Kuna wale wanaoshindwa kutoka kwa sababu wanaamini kwamba mwanamke haruhusiwi kutoa talaka. Hi siyo kweli. Kuna wanaoshindwa kutoka kwa sababu dini zao zinakataza kuachana, hii pia siyo kweli. Mwanamke au mwanaume, yeyote anaweza kuomba talaka na ikatolewa, kama kuna sababu zenye kukidhi haja hiyo. Chombo pekee kinachoweza kutoa talaka au kuidhinisha wanandoa kuachana ni Mahakama, siyo dini au taasisi nyingine. Kinachoitwa ‘talaka tatu’ kwa mfano, ni ushahidi tu, na sio talaka.
Kuna wale ambao hawako tayari kutoka kwenye uhusiano mgumu kwa sababu ya mali. Wanaogopa watagawana mali na wenzao, jambo ambalo hawako tayari kulifanya na mara nyingi hawa ni wanaume. Wapo pia wanawake ambao wao ndio waliokuwa watafutaji wakuu. Swali la kujiuliza ni hili. ‘Ni kipi bora, ni mali au ni amani na utulivu na uhai wako?’ kama ni mali, basi hakuna anayeweza kukuingilia kwenye uamuzi wako.
Lakini, kwa ufahamu tu, ni kwamba, pasipo na amani, mali haina maana na pasipo na amani uhai ni wa kubahatisha pia.
Wengine wanashindwa kutoka kwenye husiano kwa sababu wazazi wa mume na ndugu wanampenda sana. Anaogopa kuwaudhi kwa kuondoka kwenye ndoa ya mateso ya mtoto wao na ndugu yao. Anataka wafurahi, hivyo hawezi kuondoka. Huu nao ni upungufu.
Hivi unakuwa umeolewa na ndugu na wazazi au na mume? Lakini, kwani ukiondoka utashindwa kuwa karibu na watu hawa? Hutashindwa na pengine urafiki wenu utakuwa wa kudumu. Ukiendelea kukaa kwenye ndoa ya mateso kuna siku utakosana hata na hawa, maana unaweza ukalipukwa ukamuuwa mtoto au ndugu yao.
Kuna wale wanaoshindwa kutoka kwenye uhusiano mgumu kwa sababu wana watoto na wanaogopa kwamba, watoto wao watateseka. Hivi ni kuteseka kupi kubaya, kule kwa utotoni au ukubwani? Mtoto anayeishi kwenye ndoa yenye vurugu, anaharibikiwa kuanzia utotoni hadi ukubwani. Lakini, hata hivyo kuachana kwa wazazi, sio lazima kuwe na maana ya watoto kuteseka.
Kuna wakati hata watoto wanamwambia mama atoke kwenye ndoa, halafu mama huyo huyo anadai anakaa kwenye ndoa hiyo kwa sababu ya watoto! Kuna haja ya kujiuliza maswali kwa upana zaidi.
Ukitaka kutoka kwenye ndoa ngumu jiulize maswali haya. Je, ndoa hii ni kwa faida ya nani? Je, niliolewa au kuoa ili kupata shida au amani na upendo? Je, bila ndoa,nisingeweza kuishi mwenyewe? Tafuta mifano ya wasio na ndoa ambao wanafurahia maisha.
Jiulize ni kwa kiasi gani wengine wanasaidia kukusukuma zaidi kwenye ndoa hiyo? Jiulize ukamilifu wako. Je, wewe ni nusu mtu au mtu kamili? Kama ni mtu kamili , basi ishi kama mtu kamili.

Dully Sykes aonyesha dharau live XXL ya Clouds FM

 Dully akiwa katika picha
Nachelea kusema kuwa wanakuwa wanalewa ama sifa au vijisenti ambavyo wanakuwa wamevipata na kusau mashabiki ndio wamewafanya wawe na umaarufu walionao na si tu mashabiki bali vyombo vya habari ndio vimewafikisha hapo walipo.
Binafsi nimekerwa sana na kitendo cha mwanamuziki Dully Sykes kukosa adabu akiwa si tu studio bali akiwa Live kwenye kipindi ambacho mashabiki wake wengi wanamsikiliza. Ndani ya wiki moja msanii huyu ameweza mara mbili kukosa adabu tena kwenye radio moja hiyo hiyo.
Wiki iliyopita akiwa live kwenye kipindi cha XXL Dully Sykes alimjibu fyongo mtangazaji Adam Mchomvu wa kipindi hicho mwanzo nilidhani ilikuwa utani lakini Dully alisisitiza kuwa hawezi kuongea na mtu mchafu kama Adam Mchomvu, “siwezi kuongea na mtu mchafu kama wewe angalia mi nywele yako…. mi naongea na Boss wako biashara si mtu mchafu kama wewe” alisema Dully. Baada ya kuangalia kipindi kile kesho yake kupitia Nyuma ya Lensi kupitia Clouds TV nikaona jinsi ile ilivyomuumiza Adam Mchomvu na alivyokuwa akitulizwa asiendelee kujibishana na Dully kiasi alivua headphones na kukaa pembeni.
Kumbuka Dully alikuwa akifanya mahojiano juu ya wimbo wake mpya ambao ameutoa kwa kumshirikisha Mwana FA. Baaada ya Single hiyo inayokwenda kwa jina la Ameen kupigwa hewani watu wakaanza kusema kuwa Single hiyo imefanyiwa sampling kutoka kwenye wimbo mmoja wa huko Jamaica. Hii ilimpelekea Gossip Cop wa Clouds fm kuruka hewani na kumuuliza kwanza Mwana FA juu ya hiyo ambaye alikiri kwa kiasi fulani midundo imefanana lakini alisema ailizwe Dully Sykes ambaye naye baada ya kupigiwa badala ya kujibu alionyesha kukerwa na swali hilo inawezekana style ya kuulizia ya Gossip Cop lakini Dully alimjibu kuwa haongei na mashoga na kumuonya asipige tena.

Sababu za Dogo Janja kutimuliwa TIPTOP

Dogo Janja akiwa kwenye basi kurudi Arusha
 
Siku moja baada ya Dogo Janja kudaiwa kufukuzwa Tip Top Connection, ukweli halisi kuhusiana na uamuzi huo umewekwa wazi na yeye mwenyewe.Sababu zilizotajwa na Tip Top Connection ni kwamba Dogo Janja alilewa sifa na kuwa mtoro shuleni.

Kwa mujibu wa interview (ya pili kufanyiwa baada ya kipindi cha Amplifaya cha jana) tuliyofanya naye kwa simu saa moja asubuhi leo (June 14) akiwa stand kurejea nyumbani, uonevu na dhuluma ndivyo vilivyomchosha kuishi Dar es Salaam.

Anasema tangu aje Dar es Salaam hajawahi kusaidiwa chochote na Madee zaidi ya mambo ya muziki pekee huku kula, malazi na ada ya shule vikifanywa na rafiki yake Madee aitwaye Abdallah Doka ambaye (Dogo Janja) alikuwa akiishi kwake.

Anasema kutokana na ngoma zake kujipatia umaarufu alikuwa akipata show nyingi nchini na zote alikuwa halipwi chini ya milioni moja.Kilichokuwa kinamsikitisha anasema ni kulipwa hela kidogo isiyozidi laki mbili na hivyo kumfanya aishi kwa tabu licha ya kuingiza hela nyingi za show.

“Nilikuwa navumilia tu bro kwasababu kila nilipolalamika kuhusu mambo ya hela Madee alikuwa mkali sana,” ameongea uchungu.

Dogo anasema ilikuwa inafikia wakati akifanya show za ukumbuni hulipwa elfu hamsini au chini ya hapo na wakati mwingine alikuwa halipwi kabisa.Tamaa ilizidi kumwingia Madee kiasi cha kumnyang’anya kadi yake ya benki na kuanza kuchukua hela bila kujua password aliipata wapi.

“Kuna wakati nilikuwa nataka kumtumia mama laki moja, Madee akanikataza eti kwakuwa watadhani nina hela sana,” anasema.Mpaka tunaongea naye asubuhi hii, anasema kadi yake imebakiwa na shilingi 25,000 tu.

Ameendelea kudai kuwa juzi Madee alimpigia simu na kumwambia kuwa kaka yake wa Kibaha ameandaa show ya CCM na atamlipa shilingi laki moja.

“Hivi kweli bro mimi ni mtu wa kufanya show ya laki moja?”. Hata hivyo aliamua kukubali ili kuepusha lawama.
Baada ya show kumalizika anasema yeye na back up artist wake walirudishwa saa saba usiku wakati asubuhi yake alitakiwa kwenda shuleni kuchukua namba ya mtihani na kuandaa dawati la kukalia.

Dogo Janja anaeleza kuwa inamuuma sana kwakuwa muziki haujampa chochote licha ya Madee ambaye huwa hapati hata show kumtumia kimaslahi na hadi leo hii anamalizia kujenga nyumba yake.

“Ni kama vile Madee alinipanda ili anivune.”
Ameendelea kusema kuwa hiyo juzi sasa hadi kufikia Tip Top watangaze kumfukuza alikuwa kwa Tundaman akipiga story na Madee akamuita kisha kuanza kumpiga. Alichukua simu yake akaondoka nayo. “Jamaa alianza kujitumia meseji kutoka kwenye simu yangu kwenda kwake za matusi ama kuwa nataka kumroga. Jana nimemuonesha Milard hizo meseji na amesikitika sana.” Anasema simu yake alipewa jana.

Kitendo cha kumwambia Madee kuwa amechoka na anataka kurudi nyumbani ndicho kimemfanya amfanyie yote hayo hadi kumwambia kuwa watahakikisha wanambania asifanye vizuri tena kwenye muziki. Pia amedai kuwa Madee aliwapigia simu wazazi wake ili wamkataze Dogo Janja asifanye interview na vyombo vya habari.

“Wanajua nikiongea wataabika sana.”

Tuesday, June 12, 2012

Wawili wapoteza uhai wakati wengine wako mahututi hospitali

                                                           Gari ikiwa imepaki kabla ya ajali

                                               Gari ikiwa kwenye mojawapo ya mashindano

                                    Gari baada ya ajali mbaya iliyosababisha mauaji mabaya sana

Ni ajali mbaya sana iliyowakuta vijana wanne kutoka arusha waliyokwenda kwenye mashindano ya magari huko kenya, wawili wapoteza uhai huku wawili wengine wakiwa na hali mbaya hospitalini. Kwa waliyo hai hospitalini Mungu awasaidie wapone haraka na kwa waliyopoteza uhai hatuna la kusema zaidi ya Mungu azilaze roho zao mahali pema peponi amina. 



Diamond amshukuru Wema kwa english course


"Namshukuru sana mama yangu mzazi kwa elimu aliyonipatia na nashukuru sana Wema Sepetu English Course" Diamond ameyazungumza haya leo ndani ya xxl baada ya nsanii Diamond kupongezwa kwa kujibu vizuri katika interview aliyoifanya (kingereza) baada ya kupiga show  Big brother Africa. kusema ukweli amenisaidia sana kufanikisha kwangu kujua kiingereza maana alikua akinielekeza sana tulivyokuwa inlove, nisipo kuwa na shukrani kwa kidogo basi siwezi kuwa na shukrani hata kwa kikubwa" amesema Diamond.

Mimi nilijua ni toyo tu kumbe hadi baisikeli?

Ajali hizi za hivi nilijua ni boda boda na magari kumbe hadi baiskeli inaweza kuvunja mti? AJABU

Babu wa loliondo baada ya mtaji wa kutosha

Kila mtu mara aaaaah! mziki upo kwenye damu mara sijui nani kwetu alikuwa anaimba kwaya ndiyo maana na mimi naimba hakuna kitu kila kitu mazoezi...NI UTANI NA VICHEKESHO MSIAMINI SWALA HILI

Raha ya teknolojia

Waafrika bado tunachezea kwenye ubao wakati wenzwtu ndio kama hivyo wala hakuna kuchafuka lol! mambo mengine raha jaman