Friday, July 27, 2012

Diamond amchana live baba yake na baba nae kumjibu

SIKU chache baada ya kuibuka kwa baba aliyemlea Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’ aitwaye Abdul Juma na kudai kuwa mwanaye huyo amemtelekeza na hamjali, mwanamuziki huyo amemchana mzazi wake huyo, Ijumaa lina kitu kamili.
Akizungumza redioni kupitia Clouds FM, Jumatatu wiki hii, Diamond alidai kushangazwa na mzazi wake huyo huku akimtaka kuacha kusema maneno hayo kwani siyo mazuri.

HOTUBA YA MSEMAJI WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI WIZARA YA NISHATI NA MADINI JOHN JOHN MNYIKA (MB) KUHUSU MAONI YA KAMBI RASMI YA UPINZANI JUU YA MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA MWAKA 2011/2012 NA MAKADIRIO YA MATUMIZI YA WIZARA YA NISHATI NA MADINI KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013


UTANGULIZI Mheshimiwa Spika, awali ya yote niungane na wote wenye mapenzi mapema katika kuomba ulinzi wa Mwenyezi Mungu wakati tukitimiza wajibu wa kibunge kwa mujibu wa ibara ya 63 ya Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania na Kanuni Kudumu za Bunge (Toleo la mwaka 2007) kifungu cha 99 (7) wa kuishauri na kuisimamia serikali; kwa kuwasilisha maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu mapitio ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2011/2012 na makadirio ya matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2012/2013.

Download Kirungu-by Marlaw...HAPA

Listen to Marlaw_-_Kirungu.mp3 on Hulkshare - Free Music Streaming & Download

Wanasayansi nchini Marekani wanasema kuna dalili wamegunduwa njia ya kutibu ugonjwa wa ukimwi.

Virusi vya ukimwi mara nyingi huwa huishi mwilini kwa miaka mingi bila ya kutambulika, hivyo kuifanya kuwa vigumu kutibu ugonjwa huo.
Katika nyaraka zao kwenye jarida la matibabu la Nature, watafiti hao wanasema kuwa wamepata njia ya kuvimulika virusi hivyo mwilini na kuwa baada ya kufanya hivyo wameweza kuviua kutumia dawa za kuongeza nguvu mwilini.
Tayari majaribio kwa wagonjwa wanane zimefanikiwa.
Hata hivyo wamesema kuwa bado kunahitajika utafiti zaidi wa kuwezesha kuundwa dawa marudufu ya kumaliza ugonjwa huo.

Zanzibar yapiga marufuku meli tatu


Serikali ya Zanzibar imefuta usajili wa meli tatu ikiwa ni mojawapo ya jitihada ya serikali hiyo kupunguza visa vya ajali za baharini.
Serikali pia imeliagiza halmashauri ya kusimamia usafiri ,Surface and Marine Regulatory Authority(SUMATRA),kuongeza utenda kazi wake hadi Zanzibar
Hatua hii inakuja wiki moja baada ya meli ya MV Skagit kuzama baharini wakati ikielekea zanzibar.

Thursday, July 26, 2012

Ameshakuambia ana wake, unamng’ang’ania wa nini?

 MAPENZI ni sanaa yenye wigo mpana sana ndugu zangu. Unahitajika uwe mbunifu sana ili uweze kuendelea kuwa bora kwa mpenzi wako kila siku. Lazima uwe mtafutaji wa kitu kipya ili uweze kuwa wa tofauti kwa mwenzako.
Huwezi kuwa yuleyule, ikiwa hivyo maana yake utakinaiwa. Naam! Let’s Talk About Love ni safu nzuri kwako kwa ajili ya kuongeza maarifa na kukufanya uendelee kuwa bora zaidi kwa mpenzi wako.
Rafiki zangu, leo nataka kuzungumzia mada moja muhimu sana. Nazungumza na wale wenzangu ving’ang’anizi. Ni suala linalowasumbua wengi sana. Mtu anajua kabisa kwamba mtu anayemshawishi awe wake, tayari ana mpenzi wake, inakuwaje hapo?
Nimepata kesi nyingi sana za aina hiyo. Mwanamke anamtaka mwanaume ambaye ana mchumba wake au mume kabisa. Upande wa pili nao, mwanaume anamtaka mke wa mtu au mpenzi wa mtu. Maana yake ni nini sasa?
Mbaya zaidi, mwingine anaambiwa wazi kwamba ana mtu wake, lakini bado anang’ang’ania inasababishwa na nini? Haya ndiyo ambayo ninakwenda kuzungumza nanyi wapenzi wasomaji wangu.

LORI LA MCHANGA LAANGUKIA RAV 4 MBEZI BEACH JIJINI DAR

Ajali hii imetokea maeneo ya Mbezi Afrikana jijini Dar es Salaam leo ambapo Lori hili lenye nambari za usajili T 545 BPU lililokuwa likimwaga mchanga na kujikuta likipiga mweleka na kuangukia Gari ndogo aina ya Toyota Rav4 yenye nambari za Usajili T839 BSL iliyokuwa imepaki katika eneo hilo. Hakuna mtu aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa katika ajali hiyo.

Sajuki akutwa na ugonjwa mwingine tofauti na wa mwanzo:

PAMOJA na kwamba afya ya staa wa filamu Bongo, Sadick Juma Kilowoko ‘Sajuki’ inaendelea vizuri, imegundulika kuwa ana ugonjwa mwingine tofauti na ule uliompeleka India kufanyiwa upasuaji, chanzo chetu kinakuwa cha kwanza kukuhabarisha.
Hivi karibuni, Sajuki alirejea kutoka nchini India alipokwenda kwa ajili ya matibabu ambapo alionekana kuwa na mabadiliko makubwa kiafya jambo lililowapa matumaini mashabiki wake.

HABARI MEZANI

Akizungumza na waandishi wetu, juzi, Jumapili nyumbani kwake, Tabata jijini Dar es Salaam, mke wa Sajuki, Wastara Juma alisema mumewe amegundulika kuwa na tatizo lingine walipokuwa nchini India kwa matibabu.
Alisema, hawakutaka kuweka hali hiyo mapema kwa Watanzania kwa kuhofia kusababisha simanzi, lakini sasa wanalazimika kufanya hivyo ili kuwafanya wajue kinachoendelea kwa staa wao.
“Kwa kweli mume wangu bado anaumwa na amegundulika kuwa na tatizo lingine ila tunamshukuru Mungu anaendelea vizuri,” alisema Wastara kwa huzuni nyingi.

Wednesday, July 25, 2012

Scotland yatetea haki ya wasenge


Ndoa za watu wa jinisia moja

Serikali ya Scotland imetangaza kwamba itaruhusu ndoa za watu wa jinsia moja.
Hii inamaanisha kuwa Scotland inakuwa jimbo la kwanza la uingereza kutangaza sheria kama hiyo.
Naibu waziri mkuu wa Scotland Bi Nicola Sturgeon amesema hatua hiyo ni ya maana sana na inastahili hasa kwa vile serikali yake inayoheshimu usawa wa kijinsia.
Huenda Scotland ikajitokeza kuwa sehemu ya kwanza ya Uingereza kukubali ndoa za watu wa jinsia moja baada ya serikali ya SNP kutangaza mipango ya mabadiliko hayo.
Mawaziri wamesema kua muswada huo utajadiliwa mapema ikiashiria kua sherehe za kwanza huenda zikafanyika mwanzoni mwa mwaka 2015.

Tuesday, July 24, 2012

Ukimwi usiosikia dawa waongezeka Afrika ya Mashariki


Dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi
Aina ya ugonjwa wa ukimwi ambao hausikii dawa umekuwa ukiongozeka katika bara la Afrika katika muda wa muongo mmoja uliopita.
Kwa muujibu wa ripoti iliyoandikwa na wataalam katika jarida la kisayansi la Lancet, hali hii imebainika baada ya watu 26,000 walioma virusi hivyo kufanyiwa utafiti.

Sunday, July 22, 2012

UN yatangaza kazi kwa vijana hakuna EXPERIENCE ya kazini


Job Title: 2012 YPP EXAMINATION - ARCHITECTURE, P2
Department/ Office: Department of Management
Duty Station: OTHER; VIENNA; SANTIAGO; ADDIS ABABA; NAIROBI; BANGKOK; NEW
YORK; GENEVA
Posting Period: 13 July 2012-12 September 2012
Job Opening number:12-ENG-DM-24424-E-NEW YORK (O)
United Nations Core Values: Integrity, Professionalism, Respect for Diversity