UTANGULIZI Mheshimiwa Spika, awali
ya yote niungane na wote wenye mapenzi mapema katika kuomba ulinzi wa
Mwenyezi Mungu wakati tukitimiza wajibu wa kibunge kwa mujibu wa ibara
ya 63 ya Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania na Kanuni Kudumu za
Bunge (Toleo la mwaka 2007) kifungu cha 99 (7) wa kuishauri na
kuisimamia serikali; kwa kuwasilisha maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani
kuhusu mapitio ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2011/2012 na makadirio
ya matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha
2012/2013.
Mheshimiwa Spika, nitumie pia nafasi hii kuwashukuru Watanzania wenzangu wa kada, hadhi na ngazi mbalimbali katika taasisi na maeneo mengi ndani na nje ya nchi waliouniunga mkono kwa hali na mali katika kipindi chote cha misukosuko ya kusimamia ukweli na uwajibikaji: katika kuifuatilia serikali na kuunganisha wadau wengine kuwezesha maendeleo katika jimbo la Ubungo; wakati wa kesi ya kupinga matokeo ya ushindi wetu; wakati wa operesheni za 2
kuhamasisha mabadiliko katika maeneo mengine nchini na katika uwakilishi wa wananchi bungeni. Utaratibu wa kupokea maoni na kutoa taarifa za mara kwa mara za maendeleo kupitia mikutano na wananchi pamoja na katika mtandao wa http://mnyika.blogspot.com tutaendelea nao. Kaulimbiu yetu ni ile ile: AMUA; Maslahi ya Umma Kwanza.
Mheshimiwa Spika, nitumie pia nafasi hii kuwashukuru Watanzania wenzangu wa kada, hadhi na ngazi mbalimbali katika taasisi na maeneo mengi ndani na nje ya nchi waliouniunga mkono kwa hali na mali katika kipindi chote cha misukosuko ya kusimamia ukweli na uwajibikaji: katika kuifuatilia serikali na kuunganisha wadau wengine kuwezesha maendeleo katika jimbo la Ubungo; wakati wa kesi ya kupinga matokeo ya ushindi wetu; wakati wa operesheni za 2
kuhamasisha mabadiliko katika maeneo mengine nchini na katika uwakilishi wa wananchi bungeni. Utaratibu wa kupokea maoni na kutoa taarifa za mara kwa mara za maendeleo kupitia mikutano na wananchi pamoja na katika mtandao wa http://mnyika.blogspot.com tutaendelea nao. Kaulimbiu yetu ni ile ile: AMUA; Maslahi ya Umma Kwanza.
Mheshimiwa Spika; Sekta
za Nishati na Madini zina umuhimu maalum katika uchumi wa nchi na
maisha ya wananchi katika kipindi cha sasa na muda mrefu ujao. Wakati
nishati ikiwa nyenzo ya kuendesha maisha ya kiuchumi, kisiasa na kijamii
ya wananchi na nchi kwa ujumla; madini ni mtaji na ni kati ya mitaji
mikubwa ya kuwezesha maendeleo ya haraka ya taifa. Hata hivyo, pamoja na
Tanzania kujaliwa rasilimali hizi nyingi ikiwemo watu, ardhi yenye
rutuba, maji (bahari, mito na maziwa), kuwa katika eneo la kimkakati la
kijiografia kwa biashara na maliasili, bado takwimu za hali ya uchumi
kwa mwaka 2011 zinaonyesha sehemu kubwa ya Watanzania wako kwenye lindi
la umaskini.
Mheshimiwa Spika, tunajadili
sekta za nishati na madini wakati taifa likiwa kwa mara nyingine tena
kwenye tishio la mgawo wa umeme pamoja na serikali kukanusha kwamba
hakutakuwa na mgawo wa umeme. Tunajadili mapitio ya utekelezaji wa
bajeti ya mwaka 2011/2012 wakati kwa mara nyingine tena kukiwa na
mvutano 3
baina ya watendaji
waandamizi wa Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake wakiwa katika
mvutano ambao umeambatana na kutuhumiana hadharani kupitia vyombo vya
habari juu ya tuhuma za ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka.
Tunajadili makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Nishati na
Madini kwa mwaka 2012/2013 wakati kukiwa na tuhuma za vigogo wa serikali
kuingiziwa fedha kifisadi katika akaunti zao za nchini Uswisi na
makampuni ya nje ya utafutaji na uchimbaji wa madini, mafuta na gesi
asili huku viongozi wa dini wakiwa wamezindua ripoti juu ya ukwepaji
kodi na upotevu wa mapato kwa serikali unaogusa pia makampuni kwenye
sekta za nishati na madini (The One Billion Dollar Question).
Mheshimiwa Spika, namuomba
kila mmoja wetu atafakari kwa ukweli wa nafsi na nafasi yake tumefikaje
hapa kama taifa na kwa pamoja tukubaliane kuwa wabunge tuwajibike
kuisimamia serikali kuhakikisha maazimio yote ya bunge kuhusu sekta za
nishati na madini ya miaka mbalimbali yanatekelezwa kwa haraka na kwa
ukamilifu. Naamini iwapo maazimio ya Bunge juu ya Mkataba baina ya
TANESCO na Kampuni ya Richmond Development Company LLC yangetekelezwa
yote na kwa wakati toka mwaka 2008, maazimio ya bunge juu ya uendeshaji
wa sekta ndogo ya gesi asili ya mwaka 2011 yangezingatiwa yote na kwa
haraka, maazimio kuhusu uhalali wa utaratibu wa Wizara ya Nishati na
Madini kuchangisha fedha kwa ajili ya kupitisha bajeti bungeni ya mwaka
2011 yangechukuliwa 4
kwa uzito
unaostahili; taifa lingeepushwa kurudia mijadala ile ile kuhusu Wizara
hii hii mara kwa mara. Aidha, kambi rasmi ya upinzani inatoa mwito kwa
bunge kupitisha maazimio ya kutaka uwajibikaji wa serikali kwa kushindwa
kutekeleza maazimio ya bunge kwa ukamilifu na kwa wakati.
Mheshimiwa Spika, kwa
mujibu wa Katiba ya Nchi Ibara ya 52 (1) Waziri Mkuu ndiye mwenye
madaraka juu ya udhibiti, usimamiaji, utekelezaji wa siku hata siku wa
kazi na shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano na ndiye kiongozi wa
shughuli za Serikali Bungeni. Ni muhimu basi, badala ya kupokea majibu
ya Wizara ya Nishati na Madini pekee ambayo imeendelea kugubikwa na
lundo la tuhuma mbalimbali, Waziri Mkuu atoe kauli bungeni kuhusu
kujirudia rudia kwa madai ya ufisadi na uzembe katika sekta za nishati
na madini.
Aidha, pamoja na mabadiliko ya Mawaziri,
Manaibu waziri, Makatibu wakuu na Wakurugenzi wa Wizara ya Nishati na
Madini na taasisi zake ya mara kwa mara, Rais ashauriwe kutumia nguvu
zake za kikatiba za ibara ya 33, 34, 35 na 36 kuwezesha hatua za
kisheria kuchukuliwa kwa wote waliotuhumiwa kwa ufisadi, uhujumu uchumi
na matumizi mabaya ya madaraka kwa mujibu wa maazimio ya bunge na
taarifa mbalimbali za serikali ili kurejesha misingi ya uadilifu na
uwajibikaji katika sekta za nishati na madini. 5
Mheshimiwa Spika, hivyo
kwa ujumla mjadala wa mapitio ya utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa
fedha 2011/2012 na makadirio ya matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini
kwa mwaka wa fedha 2012/2013 ulenge katika kuliepusha taifa letu
kuendelea kutumbukia katika ‘laana ya rasilimali’ kama ilivyojitokeza
katika mataifa mengine. Tuhakikishe tunalinda uhuru wa taifa letu dhidi
ya uporaji wa ardhi na rasilimali zake yakiwemo madini, mafuta na gesi
asili ulio katika tishio la ubeberu mamboleo, ufisadi na udhaifu wa
kimifumo. Aidha, kupitia mchakato wa katiba mpya wananchi watoe maoni ya
kuhakikisha kuwa rasilimali za muhimu ikiwa ni pamoja na madini, mafuta
na gesi zinawekewa mfumo wa kunufaisha watanzania wote na pia mikataba
kuhusu rasilimali hizo inaridhiwa na Bunge.
Tuchangie
mjadala wa sekta hizi nyeti tukikumbuka maneno ya hayati Mwalimu
Nyerere katika kitabu chake cha TUJISAHIHISHE cha mwaka 1962, nanukuu:"Lakini
woga unaweza kutokana na tamaa ya kila binadamu kupendwa na binadamu
wenzake. Sisi wote tunayo tamaa hii, au sivyo tusingekuwa binadamu. Woga
huu huweza ukamfanya mtu kuvumilia maovu, hasa kama maovu yale
yanatendwa na walio wengi kwa walio wachache, au yanatendwa na wakubwa
kwa wadogo. Kwa kuogopa kuwaudhi wengi tunawaacha watende makosa bila
kuwasahihisha, wasije wakatuchukia. Huu ni ubinafsi mbaya sana" 6
MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA MWAKA 2011/2012
Mheshimiwa Spika, tarehe 15 Julai 2011 niliwasilisha bungeni maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu mapitio ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2010/2011 na makadirio ya matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2011/2012. Kufuatia maoni hayo, yapo masuala machache ambayo Serikali imeyazingatia kwenye utekelezaji na mengine mengi serikali haikuyazingatia pamoja na umuhimu wake kwa maslahi ya nchi na maisha ya wananchi. Hivyo kupitia mapitio haya ya utekelezaji, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka serikali ieleze hatua ilizochukua juu ya maoni hayo ambayo baadhi yalijitokeza pia kwenye maoni ya Kamati za Kudumu za Bunge na michango ya wabunge kwa nyakati mbalimbali. Hakuna sababu ya kutumia muda mrefu kutoa na kujadili maoni mapya ikiwa hakuna mfumo thabiti wa kuhakikisha maoni na maazimio yanatekelezwa kwa wakati na kwa ukamilifu.
Mheshimiwa Spika, tarehe 15 Julai 2011 niliwasilisha bungeni maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu mapitio ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2010/2011 na makadirio ya matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2011/2012. Kufuatia maoni hayo, yapo masuala machache ambayo Serikali imeyazingatia kwenye utekelezaji na mengine mengi serikali haikuyazingatia pamoja na umuhimu wake kwa maslahi ya nchi na maisha ya wananchi. Hivyo kupitia mapitio haya ya utekelezaji, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka serikali ieleze hatua ilizochukua juu ya maoni hayo ambayo baadhi yalijitokeza pia kwenye maoni ya Kamati za Kudumu za Bunge na michango ya wabunge kwa nyakati mbalimbali. Hakuna sababu ya kutumia muda mrefu kutoa na kujadili maoni mapya ikiwa hakuna mfumo thabiti wa kuhakikisha maoni na maazimio yanatekelezwa kwa wakati na kwa ukamilifu.
Mheshimiwa Spika,
Kambi Rasmi ya Upinzani ilipitia kitabu cha pili cha matumizi ya kawaida
ya Wizara ya Nishati na Madini (Volume II Supply Votes) Fungu la 58 kwa
mwaka wa fedha 2011/2012 na kubaini kwamba ilikuwa ni bajeti ya mgawo
mkubwa wa posho na ufujaji ya zaidi ya shilingi bilioni 7.9 ya posho na
matumizi mengine yasiyo ya lazima. Kambi Rasmi ya Upinzani iliitaka
serikali ifanye marekebisho kwenye bajeti ili fedha hizo zipunguzwe na
kuelekezwa kwenye kuongeza ujenzi wa miundombinu wa Chuo Cha Madini
Dodoma na kuongeza kiwango cha fedha katika mfuko wa 7
wachimbaji
wadogo wa madini. Aidha, yako matumizi mengine ya ujenzi wa maofisi na
gharama kubwa za kisheria yaliyopaswa kuhamishiwa katika miradi muhimu
ya maendeleo ikiwemo ya umeme vijijini. Kwa kuwa Wizara iliahidi
kuufanyia kazi ushauri wa kupunguza matumizi yasiyokuwa ya lazima, Kambi
Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kueleza kiwango cha fedha
kilichookolewa kutokana na kutekeleza ushauri huo na kutoa pia maelezo
ni kwanini katika makadirio ya mwaka 2012/2013 pamejitokeza kwa mara
nyingine tena matumizi yasiyokuwa ya lazima.
Mheshimiwa Spika,
Kambi Rasmi ya Upinzani ilitaka kiwango cha bajeti ya Wizara ya Nishati
na Madini kuongezwa ili vipaumbele vifuatavyo viweze kuzingatiwa kwa
uzito unaostahili: Kuwekeza fedha za kutosha kwenye sekta ya umeme na
Gesi ili kumaliza kabisa tatizo la nishati ya Umeme na kupunguza gharama
za maisha. Hatua hizo ziambatane na kuwekeza katika Bomba la Gesi,
pamoja na ujenzi wa mtambo wa kutengeneza Gesi (LPG extraction Plant)
ili kuwezesha gesi kutumika kwenye magari, viwandani na majumbani;
kuhakikisha tunazalisha 360MW za umeme kila mwaka ili kufikia malengo ya
Mpango wa Maendeleo wa miaka Mitano na kumaliza tatizo la mgawo wa
umeme na mwisho kutenga fedha za kutosha kwa ajili ya usafirishaji na
usambazaji wa umeme vijijini ili kuchangia katika ukuaji wa uchumi
vijijini.
Kusuasua kwa utekelezaji wa mpango wa dharura wa umeme 8
Mheshimiwa Spika, ili
kushinikiza nyongeza hiyo ya bajeti na utekelezaji wa vipaumbele hivyo,
Kambi Rasmi Bungeni ilipendekeza bunge kupitisha azimio la kutangaza
kwamba ukosefu wa nishati ni janga la taifa na kupitisha mpango wa
dharura na maamuzi ya hatua za haraka ambazo serikali inapaswa
kuzichukua kwa uwajibikaji wa pamoja. Tarehe 18 Julai 2011 Waziri Mkuu
Mizengo Pinda alikubaliana na mapendekezo yetu na hivyo wakati anatoa
hoja ya kuahirisha majumuisho ya mjadala wa makadirio ya mapato na
matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini akaahidi kwenda kukata fedha
kwenye posho na matumizi mengine yasiyokuwa ya lazima katika bajeti ya
serikali ili kuelekeza fedha kwenye mradi wa dharura wa umeme.
Mheshimiwa Spika, hata
hivyo inaelekea ahadi hiyo ilikuwa hewa kwani tarehe 13 Agosti 2011
Serikali ikageuka na kuleta mpango wa dharura tofauti ambao ulijikita
katika serikali kuidhamini TANESCO kwenda kukopa kwenye mabenki ya
kibiashara zaidi ya bilioni 400. Pamoja na kuikumbusha serikali bungeni
kutekeleza ahadi hiyo ya Waziri Mkuu, serikali ilipuuzia ushauri
uliotolewa. Matokeo yake mpaka sasa Shirika la Umeme (TANESCO)
halikuwezeshwa kupata kiwango cha fedha kilichopangwa na utekelezaji wa
mipango husika kusuasua.
Mheshimiwa Spika, ikumbukwe kwamba Mpango wa Dharura 9
ulipowasilishwa
bungeni tarehe 13 Agosti 2011 serikali ilieleza kuwa imepanga kuongeza
MW 572 ifikapo mwezi Disemba 2011. Kati ya hizo, MW 150 ilikuwa
zizalishwe kupitia makubaliano baina ya Shirika la Hifadhi ya Jamii
(NSSF) na TANESCO; ilitarajiwa kuzalishwe MW 50 Septemba, MW 50 Oktoba
na MW 50 Novemba 2011. Kimsingi, kauli iliyotolewa bungeni kuwa mitambo
ilikuwa imepatikana haikuwa ya kweli. Hivyo, ahadi ya kupata umeme huo
ilikuwa hewa. Mpaka sasa hakuna hata MW moja ambayo imezalishwa kwa
ushirikiano kati ya NSSF na TANESCO. Ujumbe ulipotumwa Marekani kwenda
kuona mitambo iliyokuwa inaelezwa kwamba ipo haikukuta mitambo yoyote,
walikuta kampuni ambayo haikuwa na uwezo kama ilivyokuwa kwa Richmond
Development LLC; timu hiyo ya wataalamu ilibidi kwenda Ufaransa nako
ikakosa mitambo ya dharura. Hivyo, fedha nyingi za umma zimetumika
kufuatilia ahadi hewa na umeme mpaka sasa haujapatikana na taifa
limerejea kwenye utegemezi wa mitambo ya kukodi ya gharama kubwa ya
umeme kwa sababu ya udhaifu na uzembe wa kiutendaji. Hivyo, si kweli
kwamba mpango wa dharura wa umeme umetekelezwa kwa mafanikio ya asilimia
64.5 kama inavyodaiwa na Serikali kwa kupunguza lengo lilopitishwa
bungeni, bali mpaka sasa umetekelezwa kwa asilimia 47.6 tu; katika
muktadha huo, serikali inabidi ieleze kwa ukweli ni kwa vipi mgawo wa
umeme utaepukwa kwa kuzingatia pia barua ya Mwenyekiti wa Bodi ya
TANESCO kwa Rais yenye kueleza uwepo wa tishio la mgawo wa umeme. 10
Mheshimiwa Spika, kwa
upande mwingine upungufu wa umeme unaojirudia rudia matokeo ya serikali
kushindwa kutekeleza kwa wakati mpango wa kuweka mitambo ya MW 100
Ubungo (Dar es salaam) na MW 60 Nyakato (Mwanza) ambayo iliwekwa kwenye
mpango wa umeme wa mwaka 2009 ambao ulicheleweshwa na hatimaye wakati wa
Bajeti ya mwaka fedha 2010/2011 Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati na
Madini wote waliahidi kukamilisha uwekaji wa mitambo hiyo mapema mwaka
2011. Hata hivyo pamoja na miradi hiyo kuingizwa kwenye mpango wa
dharura tarehe 13 Agosti 2011 hakukuwa na usimamizi thabiti wa kufanya
ikamilike kwa wakati. Kuzinduliwa kwa mtambo wa MW 100 Ubungo katika
mwaka wa fedha 2012/2013 ni hatua ndogo kwa kuzingatia kwamba, ilipaswa
mwaka wa fedha 2011/2012 pekee taifa liongeze jumla ya MW 360 toka
kwenye mitambo ya kununua na si ya kukodi ili kuendana na malengo ya
mpango wa taifa wa miaka mitano. Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka
serikali ieleze sababu za kuchelewa kutekelezwa kwa miradi hiyo na hatua
za uwajibikaji zilizochukuliwa kutokana na udhaifu huo.
Kashfa ya Ununuzi wa mafuta ya kufua umeme
Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani tulitahadharisha kwamba mpango wa dharura wa umeme na ununuzi wa mafuta 11
Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani tulitahadharisha kwamba mpango wa dharura wa umeme na ununuzi wa mafuta 11
kwa
ajili ya kufua umeme isitumike kama mwanya wa ufisadi na kuzalisha
"Richmond nyigine". Inaelekea kansa hii ndani ya Serikali inayoongozwa
na CCM ya kuachia dharura ziendelee kwa manufaa ya wachache imesambaa
kwa kiwango cha kuwa vigumu kutibika isipokuwa kwa mabadiliko ya mfumo
mzima wa utawala. Katika siku za karibuni kumekuwapo na malalamiko
kutoka kwa wazabuni ambao wamekosa zabuni ya kuiuzia TANESCO mafuta ya
kuendeshea mitambo ya kufua umeme ya IPTL kutokana na uamuzi wa Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, wa kuipatia zabuni
kampuni ya PUMA Energy (Tz) Ltd. (zamani ikiitwa BP (Tz) Ltd.) ambayo
inamilikiwa na Serikali kwa asilimia 50. Licha ya malalamiko ya wazabuni
hao, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inafahamu kwamba kuna kampeni
kubwa imefanywa na inaendelea kufanywa ndani na nje ya Bunge hili tukufu
ili uamuzi huu wa Katibu Mkuu Maswi ubatilishwe kwa maslahi ya
makampuni hayo na wapambe wake wa ndani na nje ya Bunge lako tukufu.
Aidha, wanaoendesha kampeni hiyo wanashinikiza Katibu Mkuu Maswi
ajiuzulu kwa kile kinachoitwa kitendo chake cha kukiuka Sheria ya
Manunuzi ya Umma.
Mheshimiwa Spika, kwa
mujibu wa nyaraka ambazo Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inazo, tarehe
10 Juni, 2011 aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO William Mhando
alimwandikia Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufilisi, Vizazi na Vifo (RITA) –
iliyokuwa 12
inasimamia ufilisi wa
IPTL – kumtaka aendeshe mitambo ya IPTL ili kufua MW 100 za umeme ili
kuweza kuondoa mgawo wa umeme uliokuwa unaendelea sehemu mbalimbali
nchini. Nyaraka hizo zinaonyesha kwamba mara baada ya kupata barua hiyo,
tarehe 24 Juni 2011, Mtendaji Mkuu wa RITA alimwandikia barua
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA)
akimwomba mwongozo na ushauri juu ya utaratibu wa manunuzi ya mafuta ya
kuendeshea mitambo ya IPTL kwa dharura.
Mkurugenzi Mkuu wa PPRA alitoa mwongozo kwa RITA kwa barua yake ya tarehe 28 June, 2011 ambapo aliielekeza RITA itumie mamlaka yake chini ya kanuni ya 42 ya Kanuni za Manunuzi ya Umma zinazohusu Bidhaa, Kazi na Huduma zisizokuwa na Ushauri Elekezi na Mauzo ya Mali za Umma kwa Tenda, Gazeti la Serikali Na. 97 la mwaka 2005 (Public Procurement (Goods, Works, Non-Consultant Services and Disposal of Public Assets by Tender) Regulations, Government Notice No. 97 of 2005). Kanuni hiyo inamruhusu Afisa Masuhuli kuamua namna ya kufanya manunuzi kwa dharura bila kujali mipaka ya mamlaka yake endapo kwa kufanya hivyo kutahakikisha uchumi na ufanisi wa manunuzi hayo na endapo ataona ni kwa manufaa ya umma kwamba bidhaa au kazi zenye thamani inayozidi mamlaka yake zinunuliwe kama suala la dharura.13
Mkurugenzi Mkuu wa PPRA alitoa mwongozo kwa RITA kwa barua yake ya tarehe 28 June, 2011 ambapo aliielekeza RITA itumie mamlaka yake chini ya kanuni ya 42 ya Kanuni za Manunuzi ya Umma zinazohusu Bidhaa, Kazi na Huduma zisizokuwa na Ushauri Elekezi na Mauzo ya Mali za Umma kwa Tenda, Gazeti la Serikali Na. 97 la mwaka 2005 (Public Procurement (Goods, Works, Non-Consultant Services and Disposal of Public Assets by Tender) Regulations, Government Notice No. 97 of 2005). Kanuni hiyo inamruhusu Afisa Masuhuli kuamua namna ya kufanya manunuzi kwa dharura bila kujali mipaka ya mamlaka yake endapo kwa kufanya hivyo kutahakikisha uchumi na ufanisi wa manunuzi hayo na endapo ataona ni kwa manufaa ya umma kwamba bidhaa au kazi zenye thamani inayozidi mamlaka yake zinunuliwe kama suala la dharura.13
Mheshimiwa Spika, baada
ya kupata mwongozo huo wa PPRA, Mtendaji Mkuu wa RITA alimwandikia
Katibu Mkuu Maswi barua ya tarehe 18 Julai, 2011 kumweleza kwamba katika
makampuni matano yaliyoonyesha nia ya kuiuzia IPTL tani 500 za mafuta
kwa siku zilizokuwa zinahitajika kuendeshea mitambo yake kwa mwezi
Julai, 2011, kampuni za OilCom na Shell hazikuwa na akiba ya mafuta
wakati ambapo kampuni ya Mogas ilikuwa na lita laki tatu tu. Kwa upande
mwingine, kampuni ya Oryx ilikuwa na tani 6,000 lakini ilikuwa inauza
mafuta hayo kwa dola za Marekani 1,069.30 au shilingi 1,668,456.02 kwa
tani. Aidha, kampuni ya BP (sasa Puma Energy) ilikuwa na tani 9,000 na
ilikuwa tayari kuuza mafuta hayo kwa dola za Marekani 901.02 au shilingi
1,405,864.77 kwa tani. Kwa kuzingatia maelezo hayo, Katibu Mkuu Maswi
alitoa ridhaa kwa RITA kununua mafuta ya kuendeshea mitambo ya IPTL
kutoka kwa kampuni ya BP kwa bei iliyotajwa hapo juu.
Mheshimiwa Spika, licha
ya ukweli kwamba mafuta ya BP yalikuwa na bei ndogo ikilinganishwa na
bei ya Oryx, tarehe 27 Septemba, 2011 Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO
alisaini mkataba wa kununua mafuta kutoka Oryx kwa bei ya dola za
Marekani 926.98 au shilingi 1,501,707.60 kwa tani. Aidha, wiki moja
kabla ya hapo, yaani tarehe 21 Septemba, Mkurugenzi Mtendaji huyo
alikwishasaini mkataba mwingine na kampuni ya Camel Oil kwa bei ya dola
za Marekani 905.24 au shilingi 1,466,488.80 kwa tani. Kama 14
inavyoonekana,
mikataba yote miwili ilikuwa na gharama kubwa zaidi kwa tani kuliko bei
ya BP. Hata hivyo, mkataba wa BP ulikatishwa na TANESCO ikaanza kununua
mafuta ya kuendeshea mitambo ya IPTL kutoka kwa makampuni ya Oryx na
Camel Oil.
Mheshimiwa Spika,
kitu cha ajabu ni kwamba licha ya mikataba ya makampuni ya Oryx na Camel
Oil kuonyesha bei za shilingi 1,501.70. na shilingi 1,466.49 kwa lita,
TANESCO ilianza kununua mafuta ya makampuni hayo kwa shilingi 1,850 kwa
lita! Kwa maana hiyo, kwa mikataba ya kununua jumla ya lita 16,110,000
kwa mwezi kutoka kwenye makampuni hayo, TANESCO ilikuwa inayalipa
makampuni hayo jumla ya shilingi 29,803,500,000 kwa mwezi. Kwa
ulinganisho, mafuta yaliyouzwa na BP kwa mkataba na RITA yaliigharimu
Serikali shilingi bilioni 13,140,000,000 kwa bei ya shilingi 1,460 kwa
lita. Hii ndio kusema kwamba kama TANESCO ingeendeleza mkataba na BP
badala ya kuuvunja, gharama ya mafuta ya kuendeshea mitambo ya IPTL
ingekuwa shilingi 23,520,600,000 na hivyo TANESCO ingeliokolea taifa
shilingi 6,282,900,000 kila mwezi!
Mheshimiwa Spika, kwa
upande mwingine kumekuwa na taarifa nyingi kwenye vyombo vya habari
kwamba Mkurugenzi Mtendaji Mhando hakutendewa haki aliposimamishwa kazi
ili kupisha uchunguzi juu ya utendaji kazi wake. Nyingi ya taarifa hizo
zimetolewa bila kuwa na faida ya kuangalia nyaraka zinazohoji 15
uadilifu na uaminifu wa Mkurugenzi Mtendaji Mhando.
Mheshimiwa Spika, Mkurugenzi
Mkuu Mhando ni mkurugenzi na mwanahisa wa kampuni binafsi inayoitwa
Santa Clara Supplies Co. Ltd. ya Dar es Salaam. Wakurugenzi wengine ni
mke wake Eva Martin William, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji, na watoto
wao. Kwa mujibu wa taarifa ambazo Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inazo,
mnamo tarehe 20 Desemba, 2011, Santa Clara Supplies iliingia mkataba na
TANESCO ambapo Santa Clara Supplies ilikubaliwa kuwa mgavi wa vifaa vya
ofisini vya TANESCO kwa gharama ya shilingi 884,550,000. Mkataba huu
ulisainiwa na Mkurugenzi Mtendaji Mhando kwa niaba ya TANESCO na mkewe
Eva Martin William kwa niaba ya Santa Clara Supplies. Aidha, barua ya
TANESCO iliyoitaarifu Santa Clara Supplies kwamba imepatiwa zabuni hiyo
iliyoandikwa tarehe 24 Novemba, 2011 ilisainiwa na Mkurugenzi Mtendaji
Mhando.
Mheshimiwa Spika, Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma inaelekeza kwamba "… kiongozi wa umma hatajiweka katika hali ambayo maslahi yake binafsi yatagongana na wajibu wake kama kiongozi wa umma." Aidha, "…
kuhusiana na uwazi kwa wananchi, viongozi wa umma watawajibika
kutekeleza wajibu wao kwa umma na kuendesha shughuli zao binafsi kwa
namna ambayo itaonekana na kuthibitika kuwa ni wazi na umma na
haitatosheleza kwao 16
kutekeleza wajibu wao kwa kufuata sheria tu." Vile vile, "… kuhusiana na utoaji wa maamuzi, viongozi wa umma watatekeleza wajibu wao kufuatana na sheria na kwa maslahi ya umma." Zaidi ya hayo, "… kuhusiana
na maslahi binafsi, viongozi wa umma hawatakuwa na maslahi binafsi
ambayo yanaweza kuathiriwa na maamuzi ya serikali wanayoshiriki katika
kuyafanya." Mwisho, "… kuhusiana na
maslahi ya umma, pale wanapochaguliwa au kuteuliwa, viongozi wa umma
watapanga masuala yao kwa namna itakayozuia migongano ya maslahi ya
wazi, iliyojificha au inayoonekana kuwepo na pale ambapo migongano hiyo
inatokea kati ya maslahi binafsi na maslahi ya umma basi itatatuliwa kwa
kuangalia zaidi maslahi ya umma."
Mheshimiwa Spika,
kwa kuzingatia ushahidi huu wa maandishi, Kambi Rasmi ya Upinzani
Bungeni inamtaka Mbunge yeyote wa chama chochote cha siasa chenye
uwakilishi ndani ya Bunge lako tukufu, anayefuata imani yoyote ya dini
aseme kama, kwa mujibu wa vifungu hivi vya Sheria ya Maadili ya Viongozi
wa Umma, Mkurugenzi Mtendaji Mhando ana sifa za kuitwa kiongozi
mwadilifu wa umma. Hivyo, pamoja na uchunguzi wa kawaida unaoendelea,
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inamtaka Mkurugenzi wa Mashtaka aamuru
hatua za uchunguzi wa kijinai zichukuliwe dhidi ya Mkurugenzi Mtendaji
Mhando kuhusu tuhuma za ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka. 17
Mheshimiwa Spika; hata
hivyo hatua hizo dhidi ya Mkurugenzi wa TANESCO na watendaji
waliohusika zisigeuzwe kuwa kafara ya kuficha uzembe na udhaifu wa
Serikali kwa ujumla wake kwa kuwa taarifa za utendaji wa TANESCO kuhusu
mpango wa dharura wa umeme pamoja na ununuzi wa mafuta uliokuwa
ukifanyika zilikuwa zikiwasilishwa kwenye vikao vya Wizara ya Nishati na
Madini na hata vikao vya baraza la mawaziri. Hivyo, ili ukweli wa kina
uweze kujulikana Kambi Rasmi ya Upinzani inapendekeza kuwa bunge
liazimie kuunda Kamati Teule ya Bunge kuchunguza masuala yote ya
ukiukwaji wa sheria, matumizi mabaya ya madaraka na tuhuma za ufisadi
katika utekelezaji wa mpango wa dharura wa umeme na ununuzi wa mafuta wa
ajili ya mitambo ya umeme. Uchunguzi huo uhusishe pia mkaguzi mkuu
kufanya ukaguzi wa kiuchunguzi (Forensic Audit) kwa malipo yaliyofanywa
na makampuni ya BP (Sasa PUMA Energy), Oryx na Camel Oil ili kubaini
iwapo kuna vigogo zaidi wa serikali waliojinufaisha kwa kisingizio cha
dharura ya umeme. Izingatiwe kwamba masharti ya ibara ya 27(2) ya Katiba
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inamtaka kila mtu "… kutunza vizuri mali ya Mamlaka ya Nchi na ya pamoja (na) kupiga vita aina zote za uharibifu na ubadhirifu….".
Mheshimiwa Spika; Kambi Rasmi ya Upinzani tuliitaka Serikali katika mwaka wa fedha 2011/2012 itoe taarifa kuhusu utekelezaji wa 18
mpango
wa uboreshaji wa utendaji wa Shirika la Umeme (TANESCO) sanjari na
kutoa ripoti ya tathmini ya utekelezaji wa mpango maalum wa kurekebisha
hali ya kifedha ya shirika (2006-2010). Hata hivyo, katika mwaka husika
wa fedha utendaji wa TANESCO na hali yake ya kifedha imeendelea kususua
huku ukigubikwa na tuhuma za ubadhirifu na udhaifu wa kiutendaji hali
ambayo imepelekea pia mkurugenzi mtendaji na maafisa wengine waandamizi
kusimamishwa na kuchunguzwa. Kambi Rasmi ya Upinzani inaona kwamba hali
hii ni matokeo ya udhaifu katika uteuzi na usimamizi wa serikali kwa
mashirika ya umma na inataka uwajibikaji kutokana na hali hiyo kudumu
kwa muda mrefu. Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka serikali iwaeleze
watanzania ni mikataba mingapi mibovu yenye kuipa mzigo mkubwa wa
kifedha TANESCO na kuongeza gharama kwa wananchi imefanyiwa mapitio
katika mwaka wa fedha 2011/2012.
Mheshimiwa Spika, kwa
upande mwingine, udhaifu wa kutokutekeleza mipango ya uzalishaji wa
gesi na makaa ya mawe kwa wakati umesababisha utegemezi mkubwa kwenye
matumizi ya mafuta katika mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura.
Takribani nusu ya umeme unaozalishwa nchini hivi sasa unazalishwa kwa
kutumia dizeli, mafuta ya ndege na mafuta mazito hali ambayo imeongeza
mahitaji makubwa ya uagizaji wa mafuta toka nje ya nchi. Hii
imesababisha mahitaji makubwa ya fedha za kigeni kwa ajili 19
ya
kuagiza mafuta na hivyo kuchangia katika kuporomoka kwa thamani ya
shilingi. Aidha, ongezeko kubwa la uagizaji toka nje limeathiri urari wa
biashara na hivyo kuchangia katika mfumuko wa bei. Hivyo, Watanzania
hivi sasa wanabeba mzigo wa kupanda kwa bei za bidhaa na gharama za
maisha kwa ujumla kutokana na ufisadi kwenye mikataba, ubadhirifu katika
matumizi, uzembe katika uongozi na upungufu katika utekelezaji wa
mipango mbalimbali ya serikali kwenye sekta ya nishati.
Mheshimiwa Spika, mzigo
huu usingekuwa mkubwa iwapo Serikali ingetekeleza katika mwaka wa fedha
2011/2012 maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani ya kuhakikisha nyongeza ya
fedha kwenye bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kwa upande wa sekta
ndogo ya Gesi kwa ajili ya mitambo ya umeme na kuharakisha kuwekeza
katika Bomba la Gesi pamoja na ujenzi wa mtambo wa kutengeneza Gesi (LPG
extraction Plant).
Kutokana na hatimaye Serikali
kuzindua ujenzi wa Bomba la gesi katika mwaka wa fedha 2012/2013 na
ahadi ya Wizara ya Nishati na Madini kuwa ujenzi huo utakamilika katika
kipindi cha miezi kumi na nane ijayo, Kambi Rasmi ya Upinzani inataka
serikali kutoa kauli ya uhakika kwa taifa; je, katika kipindi hiki cha
mpito imeweka mikakati gani ya kuhakikisha mitambo ya kufua umeme
iliyopo inayotumia gesi itapata gesi inayohitajika kuliondoa taifa
katika upungufu wa 20
umeme.
Mheshimiwa Spika, katika
mwaka wa fedha 2011/2012 tuliitaka Serikali iache kutoa kisingizio cha
‘ufinyu wa bajeti’ katika kutekeleza maoni na mapendekezo ya kuongeza
fedha za Miradi ya maendeleo ya sekta za nishati na madini na
tulipendekeza vyanzo vya nyongeza vya mapato kwa ajili ya sekta tajwa
ikiwemo: kupunguza misamaha ya Kodi ikiwemo kuondoa msamaha wa ushuru wa
mafuta kwa Kampuni za Madini peke hatua ambayo ingeongeza mapato ya
mapato ya shilingi bilioni 59; Kutoka Vyanzo vipya vya mapato
tulivyovianisha; kwa upande wa sekta ya madini kwa kurekebisha kodi
sekta ya madini peke yake tungeweza kukusanya shilingi bilioni 240
katika mwaka wa fedha 2011/2012. Kambi rasmi ya Upinzani inataka maelezo
toka kwa Serikali ni kwa kiwango gani ushauri huo umezingatiwa.
Mheshimiwa Spika,
uchambuzi wa Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu makadirio ya bajeti ya
mwaka wa fedha 2011/2012 ulionyesha uwezo mdogo na kasi ndogo ya
kufikisha umeme vijijini kwa upande wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA).
Kasi ndogo ya kusambaza umeme ilielezwa pia mijini kutokana na idadi
kubwa ya maombi ya wananchi wanaotaka kufungiwa umeme huku Shirika la
Umeme (TANESCO) likiwajibu kuwa halina uwezo kwa sasa mpaka lipate
miradi. Kambi Rasmi ya Upinzani ilitaka ufanyike ukaguzi wa kiufanisi
kuhusu utekelezaji wa miradi ya usambazaji wa umeme; hivyo, 21
serikali
inapaswa kueleza iwapo ukaguzi husika ulifanyika na hatua
zilizochukuliwa na serikali katika kuongeza kasi ya usambazaji wa
umeme.
Mheshimiwa Spika, Kambi
Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali ieleze katika mwaka wa fedha
2011/2012 imetekeleza kwa kiwango gani mkakati wa kupunguza gharama za
manunuzi na pia kupunguza kiwango cha uagizaji wa nguzo na vifaa vingine
kutoka nje ili kutumia rasilimali za ndani ili kuchangia katika kukuza
uzalishaji na uchumi wetu. Izingatiwe kwamba malalamiko yameendelea
kuhusu mazingira ya kupitishwa kwa zabuni za ununuzi wa nguzo,
transforma na nyaya za umeme kwa kiwango kikubwa toka nje ya nchi huku
viwanda vya ndani mathalani TANALEC ABB, East African Cables (hususani
kampuni tanzu ya Tanzania Cables) na vingine vikididimia. Hali hii
imesababisha pia kukwama kwa utekelezwaji wa miradi mbalimbali ya
kusambaza umeme kutokana kwa kile kinachoelezwa kuwa ni vifaa
kutokupatikana kwa wakati toka nje ya nchi.
Mheshimiwa Spika, Kambi
Rasmi ya Upinzani imesikitishwa na kasi ndogo ya serikali wakati wa
utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2011/212 kuhusu kupunguza
gharama wanazotozwa wananchi za kuunganishiwa huduma ya umeme suala
ambalo linapunguza kasi ya uunganishwaji wa umeme. Bado tumeendelea
kupokea malalamiko toka kwa wananchi wanaotakiwa na TANESCO kulipia
nguzo na gharama nyingine za kuunganishwa 22
umeme
kwa viwango ambavyo ni vigumu kwa wananchi wa kawaida kumudu. Hivyo,
tunaitaka Serikali ieleze hatua za ziada inazokusudia kuchukua pamoja na
kutekeleza maoni yetu ya kutaka TANESCO ibadili mfumo wa ankara ili
kuruhusu kuingiza kwa mteja gharama hizo kidogo kidogo katika kipindi
hiki cha mpito. Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani inawahimiza wananchi
kutumia Kanuni za Sheria ya Umeme zilizotolewa kwenye gazeti la Serikali
tarehe 4 Februari 2011 (GN 63) ambazo kifungu cha nne kinaeleza namna
mteja atakavyofidiwa na kampuni ya usambazaji pale ambapo mteja
anajigharamia mwenyewe kuvutiwa umeme ili fursa hiyo iweze kutumika
ipasavyo; hata hivyo kanuni hizo zinahitaji pia kufanyiwa marekebisho
kwa kuwa zimeweka mkazo katika fidia kutolewa kutokana na malipo ya
wateja wengine badala ya mapato ya Shirika kwa ujumla wake.
Gesi Asilia
Mheshimiwa Spika, tarehe 15 Julai 2011 Kambi Rasmi ya Upinzani kuwa nchi yetu imejaliwa utajiri wa gesi asilia katikati ya lindi la umasikini wa wananchi na kwamba taifa letu lina fursa ya kuwa nchi kiongozi katika gesi Afrika na kushindana kimataifa ikiwa tutaweka mstari wa mbele upeo, umakini na uadilifu katika sekta ya nishati kuepusha laana ya rasilimali. Hata hivyo, mapitio ya utekelezaji kwa mwaka wa fedha 2011/2012 yanaonyesha bado serikali haichukui hatua thabiti kushughulikia ufisadi na udhaifu wa kiuongozi katika sekta ndogo ya gesi asili hivyo hatua za haraka zisipochukuliwa 23
Mheshimiwa Spika, tarehe 15 Julai 2011 Kambi Rasmi ya Upinzani kuwa nchi yetu imejaliwa utajiri wa gesi asilia katikati ya lindi la umasikini wa wananchi na kwamba taifa letu lina fursa ya kuwa nchi kiongozi katika gesi Afrika na kushindana kimataifa ikiwa tutaweka mstari wa mbele upeo, umakini na uadilifu katika sekta ya nishati kuepusha laana ya rasilimali. Hata hivyo, mapitio ya utekelezaji kwa mwaka wa fedha 2011/2012 yanaonyesha bado serikali haichukui hatua thabiti kushughulikia ufisadi na udhaifu wa kiuongozi katika sekta ndogo ya gesi asili hivyo hatua za haraka zisipochukuliwa 23
katika mwaka wa fedha 2012/2013 na kuendelea rasilimali inaweza kuwa chanzo cha migogoro na kuhatarisha pia usalama wa nchi.
Mheshimiwa Spika, kwa
muda mrefu sasa taifa letu limekuwa likitegemea mradi mkubwa wa
Songosongo kwa shughuli za uendelezaji, uzalishaji, na usafirishaji
ambao uko chini ya Kampuni ya Songas. Hata hivyo, kampuni ya Songas
imeiajiri Kampuni ya PanAfrican Energy Tanzania (PAT), ambayo ni
mshirika wa TPDC katika uzalishaji, usambazaji na ugavi wa gesi asili.
Kambi Rasmi ya Upinzani ilieleza bungeni tarehe 15 Julai 2011 kuhusu
tuhuma za ufisadi na ukiukwaji wa mikataba katika sekta ndogo ya gesi na
kutaka kuundwa kwa kamati teule ya bunge kuchunguza suala hilo. Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ilifanya uchunguzi wa masuala
husika na taarifa kuwasilishwa bungeni; hata hivyo mpaka sasa maamizio
ya bunge kufuatia taarifa hiyo hayajatekelezwa kwa ukamilifu. Kambi
Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kueleza ni kwanini mpaka sasa kiasi
cha dola milioni 20.1 zilizopunjwa kifisadi hazijareshwa na serikali
iache kutumia kisingizio cha kuundwa kwa Timu ya Majadiliano (GNT)
kuchelewesha utekelezaji wa maazimio.
Mheshimiwa Spika, mradi
mkubwa wa maendeleo ambao umepangwa katika mwaka wa fedha ni ujenzi wa
bomba la Gesi kutoka Mtwara mpaka Dar es salaam ambapo kwenye kasma
3162 24
umetengewa kiasi cha shilingi
93,000,000,000 huku kiwango kingine cha fedha za mradi huo kikitarajiwa
kupatikana kutokana na mkopo kutoka nje. Kutokana na unyeti wa mradi huo
kwa mustakabali wa nchi na maisha ya wananchi wa sasa na baadaye, Kambi
Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kuwasilisha bungeni na kuweka wazi
kwa umma mkataba wa mradi husika ili bunge liweze kuishauri na
kuisimamia serikali kuanzia katika hatua za awali kuhakikisha kwamba
maslahi ya taifa yanalindwa katika hatua zote na pia wananchi
wananufaika kutokana na fursa za uwekezaji huo mkubwa. Aidha, pamoja na
ujenzi wa mitambo miwili ya kusafishia gesi asili Mnazi Bay na Songo
Songo kama sehemu ya mradi huo; Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka
Serikali kueleza ni miradi ipi inayoambatana na mradi huo ambayo
imepangwa kuwanufaisha wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara ikiwemo
kuharakisha utekelezaji wa mradi wa kuzalisha umeme wa MW 300 Mtwara na
MW 230 wa Somanga Fungu (Kilwa).
Mheshimiwa Spika, pamoja
na ujenzi wa Bomba la Gesi, Kambi ya Rasmi ya Upinzani inasisitiza
mradi wa kujenga kiwanda cha kujaza gesi kwenye mitungi (LPG) na mradi
wa usambazaji wa gesi Dar es salaam pamoja na mradi wa matumizi ya gesi
kwenye magari inayotekelezwa na Shirika la Petroli Nchini (TPDC)
inapaswa kuongezewa rasilimali katika mwaka wa fedha 2012/2013. Kuanza
kwa utekelezaji wa mradi kwa ajili ya viwanda vichache na Kaya 57 25
za
eneo la Mikocheni ni hatua ndogo ukilinganisha na mahitaji; hivyo,
utekelezaji kwa mwaka wa fedha 2012/2013 upanuliwe wigo ili kuhusisha
pia kuwezesha taasisi zingine mathalani Chuo Kikuu cha Dar es salaam
kuweza kuunganishwa katika mtandao wa matumizi ya gesi asili. Hatua hii
itapunguza pia matumizi ya umeme katika maeneo yenye kuweza kutumia gesi
na kubakiza umeme mwingine utakaoweza kutumika kwenye maeneo ikiwemo ya
viwandani yenye upungufu wa nishati mbadala.
Mafuta
Mheshimiwa Spika, taarifa za Hali ya Uchumi wa Taifa katika mwaka 2011 mfumuko wa bei ya nishati na mafuta umeongezeka kwa asilimia 41.0 kwa mwezi Disemba 2011 ikilinganishwa na asilimia 12.3 katika kipindi kama hicho mwaka 2010. Kambi Rasmi ya Upinzani inarejea kusisitiza kwamba (ukiondoa kupanda kwa bei ya chakula kunakotokana na kushuka kwa uzalishaji na udhaifu katika usambazaji) chanzo kikuu cha hali cha mfumuko wa bei ni ongezeko la bei ya nishati hususani mafuta, umeme na gesi, hali ambayo imeshindwa kudhibitiwa kwa mikakati makini ya haraka na kuelekea kuwa tishio kwa utulivu wa taifa kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Mheshimiwa Spika, taarifa za Hali ya Uchumi wa Taifa katika mwaka 2011 mfumuko wa bei ya nishati na mafuta umeongezeka kwa asilimia 41.0 kwa mwezi Disemba 2011 ikilinganishwa na asilimia 12.3 katika kipindi kama hicho mwaka 2010. Kambi Rasmi ya Upinzani inarejea kusisitiza kwamba (ukiondoa kupanda kwa bei ya chakula kunakotokana na kushuka kwa uzalishaji na udhaifu katika usambazaji) chanzo kikuu cha hali cha mfumuko wa bei ni ongezeko la bei ya nishati hususani mafuta, umeme na gesi, hali ambayo imeshindwa kudhibitiwa kwa mikakati makini ya haraka na kuelekea kuwa tishio kwa utulivu wa taifa kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Mheshimiwa Spika, tarehe
15 Julai 2011 kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani iliitahadharisha
Serikali kwamba muswada wa Sheria ya Fedha uliopitishwa na bunge tarehe
22 Juni 2011 usingeweza 26
kupunguza
ugumu wa maisha kwa wananchi kwa kuwa serikali haikupunguza mzigo mkubwa
wa kodi badala yake iliweka kipaumbele katika kupunguza tatizo la
uchakachuaji kwa kuongeza mzigo mkubwa wa kodi katika mafuta ya taa.
Matokeo yake ni kwamba katika mwaka wa fedha 2011/2012 kiwango cha kodi
kwenye bei ya mafuta ya petrol hakikupungua, kodi katika dizeli
ilipungua kwa kiwango cha shilingi 99 huku mafuta ya taa yakiongezeka
kodi kwa shilingi 358 kwa lita na kuongeza mzigo wa gharama za maisha
kwa sababu ya udhaifu wa serikali na vyombo vyake katika kudhibiti
uchakachuaji kwa kusimamia utawala wa sheria.
Mheshimiwa Spika, Kambi
Rasmi ya Upinzani inataka Serikali ieleze ni hatua zipi ambazo Serikali
imechukua dhidi ya athari za kupanda kwa bei ya mafuta ya taa kwa
wananchi wa kipato cha chini na pia kwa hali ya mazingira nchini
kutokana na ongezeko la matumizi ya kuni na mkaa. Aidha, ikiwa mkakati
huu umeweza kudhibiti uchakachuaji Serikali inatoa maelezo gani kutokana
na kuwepo kwa malalamiko ya kuendelea kwa aina nyingine za
uchakachuaji, na ni kwa nini taifa liendelee kuingia gharama za vinasaba
vinavyowekwa na EWURA wakati inaelezwa kwamba uchakachuaji umeweza
kudhibitiwa baada ya kupandisha bei ya mafuta ya taa?
Aidha,
kama sehemu ya mchakato wa kupunguza gharama za mafuta kufuatia
mabadiliko ya kodi, tozo na mfumo wa uingizaji wa mafuta serikali ieleze
imefikia hatua gani katika mwaka wa fedha 27
2011/2012
kufanya mapitio ya mkataba baina ya EWURA na kampuni ya Global Fluids
International (T) Ltd kuhusu ufanisi na gharama za kuweka vinasaba na
kuleta vifaa maalum vya kupima ubora (XRF).
Mheshimiwa Spika,
ukiondoa kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia na ukubwa wa
kodi zinazotozwa na serikali bei ya mafuta inakuwa juu kutokana na mfumo
mzima wa uagizaji, usafirishaji, uingizaji, uhifadhi na usambazaji.
Mfumo uliopo unanufaisha makampuni makubwa mengi yakiwa ya kigeni na
wafanyabiashara wachache wa ndani pamoja na baadhi ya viongozi wa
serikali wasiokuwa waadilifu kwa kulinyonya taifa na kuongeza gharama za
maisha kwa Watanzania walio wengi.
Mheshimiwa Spika, hali
hii ndiyo iliyokwamisha kwa miaka mingi kuanza kwa mfumo wa uagizaji na
uingizaji wa mafuta ya pamoja (Bulk Procurement System) ili kupunguza
gharama; hata hivyo hata baada ya kuanza kwa utaratibu husika katika
mwaka wa fedha 2011/2012 tija ya kutosha ya mfumo huo haijapatikana
kutokana na udhaifu wa kimfumo. Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka
Serikali kueleza sababu za kutokurejesha hifadhi ya taifa ya kimkakati
ya taifa ya mafuta (National Strategic Oil Reserve) pamoja na
kutokukamilisha mchakato wote wa kufufua Kampuni ya Taifa ya Mafuta
(COPEC) kinyume na ahadi ya Wizara ya Nishati na Madini ya mwaka 2011.
Aidha, ni kwa nini serikali haikununua hisa za kampuni ya BP kwa kiwango
cha kuwa na umiliki wa asilimia 100 28
(100%)
ili kuongeza miundombinu ya uhifadhi na usambazaji wa mafuta kwa uchumi
na usalama wa nchi. Kwa upande mwingine, Wizara ya Nishati na Madini
ieleze hatua mahususi ilizochukua katika mwaka wa fedha 2011/2012 za
kulinda maslahi ya nchi katika kampuni ya TIPER ambayo serikali ina hisa
50% katika hatua za uingizaji na uhifadhi wa mafuta.
Mheshimiwa Spika, Ili
kuongeza tija na ufanisi wa TPDC, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka
Serikali itoe maelezo kuhusu hatua zilizochukuliwa kwenye mwaka wa fedha
2011/2012 za kulifanyia marekebisho shirika hilo ili kuwa na mamlaka
itakayohusika na kutoa vibali kwenye leseni na kusimamia uchimbaji wa
mafuta na gesi na kampuni itakayoshiriki katika biashara ya mafuta na
gesi.
Madini
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Ripoti ya Hali ya Uchumi wa Taifa katika mwaka 2011 thamani ya mauzo ya madini nje ilikuwa dola za kimarekani 1,965.23 milioni ikilinganisha na dola za kimarekani 1,536.93 milioni mwaka 2010, sawa na ongezeko la asilimia 27.9. Hii ilitokana na kupanda kwa bei ya dhahabu katika soko la dunia. Hata hivyo mchango kwenye pato la taifa umekuwa ni asilimia 3.3 tu miaka karibu mitatu toka kutungwa kwa sheria mpya ya madini mwaka 2010. Udhaifu wa Serikali katika kusimamia utawala wa sheria unapaswa kuondolewa kwa bunge kupitisha maazimio ya kuisimamia serikali kulinusuru taifa dhidi ya hali hii ambayo utajiri 29
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Ripoti ya Hali ya Uchumi wa Taifa katika mwaka 2011 thamani ya mauzo ya madini nje ilikuwa dola za kimarekani 1,965.23 milioni ikilinganisha na dola za kimarekani 1,536.93 milioni mwaka 2010, sawa na ongezeko la asilimia 27.9. Hii ilitokana na kupanda kwa bei ya dhahabu katika soko la dunia. Hata hivyo mchango kwenye pato la taifa umekuwa ni asilimia 3.3 tu miaka karibu mitatu toka kutungwa kwa sheria mpya ya madini mwaka 2010. Udhaifu wa Serikali katika kusimamia utawala wa sheria unapaswa kuondolewa kwa bunge kupitisha maazimio ya kuisimamia serikali kulinusuru taifa dhidi ya hali hii ambayo utajiri 29
wetu
unaendelea kuondoka, kwa pamoja na hatua zingine, kuwezesha mwingiliano
baina ya sekta ya madini na sekta nyingine za kiuchumi katika nchi.
Mheshimiwa Spika, Kambi
ya Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kueleza hatua iliyofikia katika
kuzingatia ushauri tulioutoa wa kutaka Wizara ya Nishati na Madini
ishirikiane na Wizara ya Fedha kuboresha mfumo wa utoaji wa taarifa za
malipo ya kodi kwa kampuni za madini ili malipo ya kila kampuni na
mchangunuo wake yafahamike kwa umma badala ya mfumo wa sasa ambapo
hurundikwa pamoja katika takwimu za idara ya walipa kodi wakubwa.
Mheshimiwa Spika, Kambi
Rasmi ya Upinzani inataka Serikali ieleze hatua ilizochukua kwenye
mwaka wa fedha 2011/2012 katika kuongeza kiwango cha mapato ikiwemo ya
kodi kutokana na uchimbaji wa madini kwa kutekeleza mikakati ya kupenya
kuta za umiliki na mitaji (capital and ownership structures)
zilizojengwa kwa muda mrefu na makampuni ya kimataifa kwa kutumia mianya
ya udhaifu wa kisheria na ushawishi wa kifisadi uliosababisha mikataba
mibovu katika sekta ya madini nchini.
Mheshimiwa Spika, wakati
umefika sasa kwa Serikali kuwasilisha bungeni ripoti ya tathmini ya
utekelezaji wa mapendekezo ya tume/kamati mbalimbali ambazo ziliundwa na
serikali kwa nyakati 30
mbalimbali
kwa kutumia fedha nyingi za walipa kodi lakini mapendekezo yake bado
hayajatekelezwa kwa ukamilifu wake. Kwa miaka mingi Serikali inazo
taarifa za makampuni makubwa ya madini kutumia sehemu kubwa ya uwekezaji
wao kama mkopo (debt financing) na kutumia mianya hiyo ya kisheria na
kimikataba kuwezesha wamiliki na wanahisa kupata faida mapema kuliko
kuweka mtaji kwa kuwa riba ya mikopo huondolewa katika kukokotoa kodi.
Kambi Rasmi ya Upinzani inarudia tena kuitaka serikali iwaeleze Watanzania ni trilioni ngapi za mapato tumezikosa kati ya mwaka 1995 mpaka 2010 katika kipindi cha miaka 15 ya kuachia mianya ya upotevu wa mapato kwa kuruhusu asilimia kubwa ya mikopo kuwa mitaji. Aidha, ni hatua gani zimechukuliwa kwa waliohusika kuliingiza taifa katika mikataba mibovu iliyoruhusu makampuni hayo kujitangazia hasara kila mwaka huku yakipata faida kubwa.
Kambi Rasmi ya Upinzani inarudia tena kuitaka serikali iwaeleze Watanzania ni trilioni ngapi za mapato tumezikosa kati ya mwaka 1995 mpaka 2010 katika kipindi cha miaka 15 ya kuachia mianya ya upotevu wa mapato kwa kuruhusu asilimia kubwa ya mikopo kuwa mitaji. Aidha, ni hatua gani zimechukuliwa kwa waliohusika kuliingiza taifa katika mikataba mibovu iliyoruhusu makampuni hayo kujitangazia hasara kila mwaka huku yakipata faida kubwa.
Mheshimiwa Spika, katika
nchi yetu tuna migodi mikubwa mbalimbali kati yake sita ilianzishwa
kati ya mwaka 1998 -2009 kwa ajili ya kuzalisha dhahabu ambayo ni Golden
Pride Mine (1998), Geita Gold Mine (2000), Bulyanhulu Gold Mine (2001),
North Mara Gold Mine (2002), Buhemba Gold Mine (2002) na Tulawaka Gold
Mine (2005), Buzwagi Gold Mine ( 2009). Buhemba Gold Mine walifunga
uzalishaji mwaka 2006 31
Mheshimiwa Spika,
migodi yote hii waliwasilisha upembuzi yakinifu serikalini kabla ya
kuanza uzalishaji na kuonyesha kuwa watalipa kodi ya makampuni
(Corporate tax) lakini mpaka sasa ni michache tu ambayo imeanza kulipa
Shilingi Bilioni 32.18 kutoka Resolute Tanzania Limited na Shilingi
Bilioni 145.52 kutoka Geita Gold Mine Limited tu , pamoja na makampuni
haya kunufaika na kupanda kwa bei ya dhahabu kwenye soko la dunia kwa
zaidi ya mara tatu kuanzia mwaka 2002, na wakati huohuo makampuni haya
yakiendelea kuweka uwekezaji mkubwa kwenye miradi yao. Kutokana na
umuhimu wa sekta hii nitaeleza japo kwa kifupi kuhusiana na baadhi ya
migodi hiyo mmoja mmoja:
Mheshimiwa Spika,
mgodi wa Bulyanhulu ambao mwanzoni ulitarajiwa kuwa na maisha ya miaka
15 na walitarajia kuzalisha ounces 400,000 za dhahabu kwa kila mwaka ila
wamekuwa wakizalisha ounces 6.5 milioni za dhahabu kwa gharama ya
kuzalisha ounce 1 kwa dola 130. Aidha walitegemea kuzalisha madini ya
Shaba (Copper ) ounces 7.26 milioni na madini ya fedha ounces 5 milioni
na kwa sasa umri wa mgodi ni miaka 25 , yaani muda umeongezeka kwa
kipindi cha miaka 10 zaidi. Mgodi wa Bulyanhulu uliwekeza kiasi cha dola
550 milioni kwa mchanganuo wa kuwa dola 300 milioni kwa uwekezaji wa
awali kabla ya kuanza uchimbaji na dola 250 milioni kwa shughuli za
uendeshaji wa mgodi. Mgodi huu ulitegemea kuzalisha kiasi cha dola 900
milioni kutokana na uchimbaji na uuzaji wa madini ya shaba (copper)
pekee na 32
mapato ya dhahabu yalikuwa
yamewekewa ukomo wa dola 300 kwa ounce tuu pamoja na kuwepo kwa
badiliko la bei kwa zaidi ya mara tatu yaani sasa ni dola 950 kwa ounce
moja. Ilikadiriwa kuwa mrahaba wa asilimia 3 uliotegemewa kulipwa
serikalini ni kiasi cha dola 58 milioni, na fedha zilizopaswa kulipwa
moja kwa moja serikalini zilikadiriwa kuwa ni dola 64 milioni ( mrahaba
dola 58 milioni,mrahaba wa moja kwa moja –direct dividend dola 2 milioni
na kodi ya zuio ya dola 4 milioni). Mgodi wa Bulyanhulu kwa sasa
umeweza kuongeza hifadhi ya dhahabu kutoka tani 13.64 milioni na kufikia
kiwango cha tani 36.05 milioni mwaka 2007 kiwango ambacho ni asilimia
90 zaidi ya kiwango kilichokadiriwa wakati wa kusaini mikataba na kuanza
uchimbaji. Mpaka mwaka 2007 mgodi huu ulilipa kiasi cha dola 26.54
milioni kama mrahaba kwa serikali, na hawajalipa kodi ya makampuni .
Mheshimiwa spika, kuhusu
Mgodi wa Geita Gold Mine mgodi huu ulianzishwa kwa gharama
inayokadiriwa kuwa dola 152 milioni kwa ajili ya uwekezaji wote ambao
ulifanywa kabla ya kuanza shughuli za uchimbaji na gharama za kuendeleza
uchimbaji kwenye mgodi husika. Mgodi hu ulikuwa umeweka malengo ya
kifedha kwa bei ya dola 300 kwa ounce na kuwa thamani halisi (NPV) ni
dola 100 milioni,Net cash flow dola 201 milioni, mrahaba dola 30
milioni,kodi ya makampuni dola 13 milioni,kipindi cha kurejesha gharama
miaka 5 na gharama za uzalishaji ni dola 181 kwa ounce. Kwa mwaka 2000
mapato halisi yalikuwa dola 14 milioni na hii ilitokana na ukweli 33
kuwa
kulikuwa na uzalishaji mdogo, na pia bei iliyokuwa imetarajiwa ya dola
350 kwa ounce haikupatikana ila ilikuwa dola 279.321 kwa ounce moja.
Mwaka 2004 mapato halisi yalikuwa zaidi ya mara nne ya matarajio nah ii
ilitokana na uzalishaji kuwa mkubwa na bei ya dhahabu kuongezeka kwani
likikuwa dola 409.271 kwa ounce ikilinganishwa na ukadiriaji wa dola 350
kwa ounce uliokuwa umewekwa awali. Ila kwa ujumla ni kuwa mapato halisi
ya mgodi huu kuanzia mwaka 2001 yamekuwa yakiongezeka mara dufu
kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji na bei ya dhahabu kuendelea
kupanda kwenye soko la dunia. Mpaka mwaka 2007 mgodi huu ulikuwa
haujalipa kodi ya makampuni pamoja na uzalishaji kuongezeka na kuwa mara
mbili zaidi ya matarajio na bei ya dhahabu kuwa kubwa mara tatu zaidi
ya matarajio kwenye soko la dunia na hii iliufanya mgodi huu mapato yake
kuongezeka zaidi ya mara tatu na mgodi uliendelea kutangaza kuwa
unapata hasara na haujaweza kurejesha uwekezaji uliofanywa.
Mheshimiwa Spika, kuhusu
mkodi wa Tulawaka katika mgodi huu uwekezaji uliofanywa ulikadiriwa
kuwa ni dola 34.6 milioni na gharama za uendeshaji zilitarajiwa kuwa
dola 325 kwa uzalishaji wa ounce 1, thamani halisi (NPV) Dola 9.507
milioni,net cash flow dola 29 milioni, mrahaba dola 5.367 milioni na
kipindi cha kurejesha gharama miaka 4(pay back period) na walitarajia
kulipa kodi ya makampuni mwaka 2008 ya dola 2.8 milioni. Kwa mwaka 2004
hapakuwa na uzalishaji na hivyo hapakuwa na mapato yeyote ila 34
kwa
mwaka 2004-2007 mapato halisi ya mgodi huu yamekuwa asilimia 72.5 ya
zaidi ya makadirio ya awali yaliyowekwa. Mpaka mwaka 2007 mgodi huu
haukuwahi kulipa kodi ya makampuni pamoja na ukweli kuwa uzalishaji
ulikuwa asilimia 7 chini ya matarajio ila mapato halisi yaliongezeka kwa
asilimia 72.5 zaidi ya matarajio yaliyowekwa.
Mheshimiwa Spika, kwa
upande wa Mgodi wa North Mara mpaka disemba 2007 ilikadiriwa kuwa kuna
ounce 3.6 milioni ukilinganisha na zilizokuwa zimetangazwa awali wakati
mgodi unaanza uzalishaji kuwa ni 2.94 milioni ounce mwaka 2002 wakati wa
ufunguzi rasmi wa mgodi. Mgodi huu mpaka mwaka 2007 ulikuwa
umebadilisha wamiliki kwa zaidi ya wamiliki 3 tofauti tofauti na ii
inafanya kuwa ngumu sana kuweza kupata taarifa halisi za mwenendo wa
m,apato kutokana na kila mmiliki kuweka utaratibu wake na kuanza upya
kama vile hapakuwa na kilichofanywa na mmiliki aliyemtangulia. Aidha
wamiliki wa awali waliweza kuuza migodi hii na kunufaika moja kwa moja
bila serikali kupata chochote kutokana na mauziano yaliyofanywa.
Mheshimiwa Spika, kwa
taarifa hizi tunaweza kuelewa kuwa uzalishaji halisi wa dhahabu kwenye
migodi hiyo mitano kuanzia mwaka 1999 -2007 ulikuwa 8.388 milioni ounces
ukilinganisha na matarajio yaliyowekwa awali kuwa ni kuzalisha 6.882
milioni ounces ambacho ni asilimia 21.88 zaidi ya matazamio ya awali.
Umri kwa 35
ajili ya uzalishaji wa
migodi hii umeongezeka kwa wastani wa miaka 4 kwa kiwango cha chini na
miaka 10 kwa kiwango cha juu, na hii ilitokana na kugundulika kwa
machimbo mapya ya dhahabu pamoja na kuongezeka kwa teknolojia ya kisasa
zaidi kwenye tasnia hii.
Mheshimiwa Spika, mapato
halisi yaliyoweza kupatikana kutokana migodi hii mitano mikubwa kwa
kipindi hicho cha kuanzia mwaka 1999-2007 ilikuwa dola 3.8 bilioni
ambazo ni asilimia 64 juu zaidi ya matarajio yaliyowekwa wakati
uwekezaji ukifanywa ambayo ni dola 2.3 bilioni .Pamoja na mapato hayo ni
kuwa fedha iliyolipwa serikalini kama mrahaba ilikuwa dola 99.6 milioni
tu kwa kipindi chote hicho. Kwa migodi yote hiyo matarajio ya bei
yaliyowekwa yalikuwa kati ya dola 300-350 kwa ounce wakati uhalisia ni
kuwa bei ilipanda na kufikia kiasi cha dola 950 kwa ounce 1.
Mheshimiwa wa Spika, mapitio
yaliyofanywa na Mamlaka ya ukaguzi wa madini (TMAA) kuanzia mwaka
2004-2008 nchini yalionyesha kuwa mgodi wa TanzaniteOne Tanzanite Mine
(TTM) umekuwa ukilipa mrahaba kwa kutumia viwango vya awali vya
makadirio ambavyo viliwekwa wakati mgodi huu ukianzishwa nchini.
Halikadhalika ripoti hiyo inaonyesha kuwa kampuni hii imekuwa ikitoa
taarifa za zisizokuwa za kweli juu ya mauzo yaliyofanyika nchini na
kwenye makampuni makubwa nje ya nchi ili kuweza kukwepa kulipa mrahaba
stahiki serikalini. Tathmini hiyo ya ukaguzi 36
inaonyesha
kuwa kwa kipindi hicho kiasi cha dola 42.7 milioni kiliongezeka zaidi
kulingana na kiwango kilichotangazwa nchini na kampuni hiyo. Hii maana
yake ni kuwa kiasi cha dola 2.1 milioni kilichopaswa kulipwa kama
mrahaba serikalini hakikulipwa kama inavyotakiwa kwa mujibu wa sheria ya
madini kifungu cha 93 (the Mining Act, Cap., 123) . Suala hili ni kwa
mujibu wa barua iliyotumwa kwa Meneja wa kamapuni ya Tanzanite one
iliyoandikwa tarehe 02.10.2009 yenyeKumb.Na DA23/168/01 iliyoandikwa
na aliyekuwa Kamishina wa Madini Mhe.Dalali Kafumu akiwataka wawekezaji
hao kulipa hata hivyo deni hilo halikulipwa kwa wakati. Kambi Rasmi ya
Upinzani inaitaka Serikali kueleza hatua ilizochukua huu ya kampuni
hiyo. Aidha, tunaitaka Serikali kutoa maelezo ya kina kuhusu kuhamishwa
kwa umiliki wa kampuni hiyo kwa kuzingatia kwamba baada ya kutungwa kwa
Sheria ya Madini ya mwaka 2010 Serikali iliahidi kwamba uchimbaji katika
eneo hilo ungeachwa kwa wachimbaji wadogo wadogo.
Kambi
ya Upinzani , inaitaka serikali kuweka hadharani ripoti na taarifa zote
zilizowahi kutolewa kuhusiana na uwekezaji katika uchimbaji wa madini
nchini kuanzia mwaka 1995 hadi 2010 na kama serikali imefaidika na nini
kutokana na uwekezaji huo.
Pili , tunahitaji mikataba yote iwekwe hadharani kwani kutokana na taarifa hizi ni hakika kuwa mikataba yetu ni mibovu sana na tunalipotezea taifa mapato mengi na hivyo kuendelea kudidimiza uchumi wa taifa. 37
Pili , tunahitaji mikataba yote iwekwe hadharani kwani kutokana na taarifa hizi ni hakika kuwa mikataba yetu ni mibovu sana na tunalipotezea taifa mapato mengi na hivyo kuendelea kudidimiza uchumi wa taifa. 37
Tatu,
Bunge liazimie kuwa mikataba yote mipya ya uchimbaji wa madini , mafuta
na gesi lazima sasa iletwe Bungeni na kujadiliwa kwa maslahi ya
watanzania , kwani kama tukiendelea na utamaduni wa kusaini mikataba
husika kisirisiri taifa hili litaendelea kupoteza mapato kutokana na
uzembe na ufisadi kwa wanaohusika na mikataba
Mheshimiwa Spika, kutokana
na kuendelea kuporomoka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania, Kambi
Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kueleza hatua iliyofikiwa katika
kutekeleza mapendekezo yaliyotolewa ya kutaka Wizara ya Nishati na
Madini ishirikiane kwa karibu na Wizara ya Fedha katika kuweka mikakati
na usimamizi wa kuhusisha sekta ya madini katika kuimarisha fedha yetu.
Wakati umefika sasa wa kuwezesha Benki Kuu kutunza sehemu ya hifadhi
yetu ya fedha za kigeni katika mfumo wa madini ya dhahabu. Hivyo Wizara
ya Nishati na Madini ishirikiane na Benki Kuu kuweka mfumo wa kununua
dhahabu kwa wachimbaji wadogo wadogo na pia kutoza sehemu ya mrabaha wa
dhahabu kwa ajili ya uhifadhi kama ilivyoshauriwa na Kambi Rasmi ya
Upinzani pamoja na kamati mbalimbali za bunge. Kambi Rasmi ya Upinzani
inasisitiza kwamba utaratibu huu uende sambamba na kusimamia mfumo wa
kuhakikisha kwamba makampuni hayo yanatunza sehemu kubwa ya fedha za nje
(walau 60%) kwenye benki za ndani ili kusaidia kudhibiti kuporomoka kwa
shilingi ya Tanzania.38
Mheshimiwa Spika, Sheria
ya Madini ya mwaka 2010 imeipa majukumu muhimu STAMICO ya kuwa
mwakilishi na msimamizi wa rasilimali za madini nchini kwa niaba ya
serikali. Mapitio ya utekelezaji kwa mwaka wa fedha 2011/2012
yanadhihirisha kwamba majukumu haya muhimu ya kisheria hayajawekewa
mazingira wezeshi yakutosha ya kimfumo, kirasilimali na kikanuni
takribani miaka miwili tangu kutungwa kwa sheria husika. Kambi Rasmi ya
Upinzani inaitaka Serikali kuharakisha marekebisho ya sheria ndogo
(Establishment Order) iliyounda STAMICO ili kuendana na mahitaji ya sasa
na kuongeza mtaji wake ikiwemo kurejesha rasilimali zilizochukuliwa
ikiwemo majengo. Serikali izingatie kwamba sera mkakati katika sekta ya
madini iwe ni kuhakikisha Watanzania wana umiliki katika miradi mikubwa
ya madini ama kupitia hisa za makampuni hayo kuwekwa katika soko la
ndani (DSE) au kwa kampuni ya umma kushikilia sehemu kubwa ya uwekezaji
hasa katika madini nyeti ikiwemo urani.
Mheshimiwa Spika, wwa
kuwa katika mwaka wa fedha 2011/2012 Wakala wa Jiolojia (GST)
aliendelea na utekelezaji wa mradi wa kutambua maeneo ya madini, Wizara
ya Nishati na Madini ieleze iwapo utekelezaji wa mradi huo ulienda
sambamba na kufanya tathmini ya kina (mineral appraisal) ya madini yetu
ili kupendekeza mabadiliko ya kisheria na kimikataba ambayo yatawezesha
utajiri wa madini yetu kutumika kama mtaji na dhamana katika hatua ya
kuhakikisha taifa letu linanufaika na rasilimali zake kama 39
ilivyopendekezwa
na Kambi Rasmi ya Upinzani. Aidha, ni kiwango gani cha mapato
kilichopatikana kwenye mwaka wa fedha 2011/2012 kutokana na kuiwezesha
GST kutoza malipo kwa mujibu wa sheria ndogo (Establishment Order)
iliyounda wakala husika. Ili kulinda maslahi ya taifa kuhusu matumizi ya
ramani na ripoti za utafiti na uchunguzi huo katika mwaka wa fedha
2012/2013 ukaguzi maalum (Special Audit) ufanyike kuhusu mfumo wa utoaji
leseni za utafutaji na uchimbaji wa madini nchini ili kudhibiti uporaji
(grabbing) unaoendelea katika rasilimali muhimu za taifa.
Mheshimiwa Spika, tarehe
15 Julai 2011 tulitoa tahadhari juu ya maamuzi ya serikali ya kuendelea
na hatua za mbele katika utafutaji na uchimbaji wa madini ya urani bila
kukamilisha maandalizi ya kisera, kisheria, kikanuni na kitaasisi
yanayohitajika suala ambalo linaachia mianya ya upotevu wa mapato kwa
taifa kama ilivyokuwa kwenye madini mengine na pia linaweza kuhatarisha
usalama. Aidha, Kambi ya Rasmi ya Upinzani ilitaka maelezo ya kina
kuhusu mauzo na mabadilishano ya umiliki yaliyofanyika baina ya kampuni
ya Australia (Mantra Resources) na Kampuni ya Urusi ya ARMZ Uranium
Holding kampuni tanzu ya Rosato. Mauzo hayo yamehusisha kuhamishiana
umiliki wa maeneo ya Tanzania Mkuju River (Mbamba Bay) na Bahi Kaskazini
(Dodoma). Kambi Rasmi ya Upinzani inatambua kwamba Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) ilifanya ufuatiliaji juu ya suala hilo, hivyo Wizara ya
Nishati na Madini inapaswa kueleza kiasi gani cha fedha kimefanikiwa
kupatikana na 40
ni hatua zipi
Serikali imechukua kwa makampuni mengine ya madini, mafuta na gesi asili
yaliyofanya mauziano katika mwaka wa fedha 2011/2012.
Mheshimiwa Spika, licha
ya ahadi ya serikali ya toka mwaka 2010 ya kumaliza migogoro katika
sekta ya madini baina ya wachimbaji wakubwa na wachimbaji wadogo wadogo
ikiwemo kudhibiti migongano kati ya wenye leseni kubwa na leseni ndogo,
migogoro hiyo imeendelea katika mwaka wa fedha 2011/2012. Kambi Rasmi ya
Upinzani inaitaka Serikali kuwasilisha bungeni orodha ya maeneo yote
yenye migogoro ya madini nchini pamoja na ratiba ya utatuzi wa migogoro
husika. Pia, pamoja na kuandaa Mkakati wa Kuwaendeleza wachimbaji wadogo
ili mkakati huo usiwe maneno matupu; Serikali iwasilishe pia mpango
kazi na bajeti ya utekelezaji wa mkakati husika. Aidha, Serikali
ianzishe mfumo wa kisheria wa kuwezesha wananchi waliokuwa wakilimiki
ardhi katika maeneo yenye madini kuweza pamoja na fidia ya mazao na
maendelezo kuwa na hisa katika umiliki wa migodi husika.
Mheshimiwa Spika, kufuatia
kushamiri kwa migogoro baina ya wafanyakazi na wawekezaji katika sekta
ya madini, Kambi Rasmi ya Upinzani inapendekeza Wizara ya Nishati na
Madini iweke mfumo wa mashauriano na Wizara nyingine ili kuharakisha
utatuzi wa migogoro husika. Aidha, kumekuwepo na wimbi la malalamiko ya
wafanyakazi walioachishwa katika migodi wa Bulyankulu, Kampuni ya
Caspian katika mgodi wa Mwadui Shinyanga , masuala ambayo 41
yanahitaji
ushirikiano wa wizara na mamlaka mbalimbali katika kuyashughulikia.
Aidha, Wizara ya Nishati na Madini itoe maelezo kuhusu taarifa
zilizotolewa bungeni tarehe 13 Aprili 2012 kuwa wafanyakazi ikiwemo wa
migodini kupitia vyama vyao walihusishwa kutoa maoni yaliyopelekea
kufutwa kwa fao la kujitoa (withdrawal benefits); suala ambalo Chama Cha
Wafanyakazi wa Migodini (TAMICO) kimelikanusha. Kwa kuwa ufafanuzi
uliotolewa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii (SSRA)
kwa barua yenye Kumb. Na. AE/164/334/Vol II/2 umekataliwa katika migodi
mbalimbali, Wizara ya Nishati na Madini imechukua hatua gani kuepusha
migogoro iliyoanza kujitokeza baina ya wafanyakazi wa migodini na
serikali kufuatia kupitishwa kwa vifungu husika vya sheria vyenye
kuagiza mafao kutolewa baada ya kufikisha umri wa hiyari wa kustaafu wa
miaka 55 au umri wa lazima wa miaka 60.
Mheshimiwa Spika, Kambi
Rasmi ya Upinzani ilihoji tarehe 15 Julai 2011 kuhusu tuhuma za Kampuni
ya New Almasi (1963) Limited kuchimba almasi kwa miaka 35 Mkoani
Shinyanga licha ya muda wa leseni yake Na. 224 kwisha na leseni yenyewe
kufutwa katika rejesta ya leseni za madini. Taarifa zilizopo zinaonyesha
kwamba mkataba kati ya New Almasi (1963) Ltd uliingiwa kinyemela kwa
lengo la kuwezesha uchimbaji wa almasi kuendelea katika eneo hilo
kinyume cha sheria na ili kuendeleza wizi wa rasilimali ya nchi yetu.
Mamia ya wananchi waishio maeneo jirani na eneo la New Almas 42
wamekuwa
wakinyanyaswa kwa miaka mingi na vyombo vya dola kama vile polisi,
mahakama na vyombo vya utawala kwa madai kwamba ni wavamizi wa eneo la
leseni ya New Almasi. Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali ieleze
hatua ilizochukua kwenye mwaka wa fedha 2011/2012 kuichunguza kampuni
hiyo, uhalali wa shughuli zake za uchimbaji almasi katika eneo la
Luhumbo, kiasi cha almasi iliyochimbwa kwa kipindi chote tokea tarehe 1
Juni 1965 hadi tarehe 8 Mei 2000 na zilizokoenda fedha zilizotokana na
mauzo ya almasi hiyo. Aidha, Serikali ifafanue utaratibu wa kisheria
ambao uliiruhusu Williamson Diamond Ltd. kuendelea kuchimba almasi
katika eneo la Luhumbo pamoja na utata juu ya uhalali wa leseni katika
eneo hilo.
MAKADIRIO YA MATUMIZI YA WIZARA YA NISHATI NA MADINI KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013
Mheshimiwa Spika, makadirio ya Matumizi na Mpango wa Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2012/2013, ni shilingi bilioni 641,269,000 ikilinganishwa na Shilingi 538, 514,071,000 zilizotengwa wa Wizara mwaka 2011/2012 baada ya kufanyika kwa uhamisho wa fedha. Bajeti hiyo imeongezeka kwa Shilingi 102,755,658,000 sawa na ongezeko la asilimia 19, hata hivyo ongezeko hili ni dogo ukilinganisha na mahitaji yaliyotajwa na Mpango wa Taifa wa miaka mitano. 43
Mheshimiwa Spika, makadirio ya Matumizi na Mpango wa Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2012/2013, ni shilingi bilioni 641,269,000 ikilinganishwa na Shilingi 538, 514,071,000 zilizotengwa wa Wizara mwaka 2011/2012 baada ya kufanyika kwa uhamisho wa fedha. Bajeti hiyo imeongezeka kwa Shilingi 102,755,658,000 sawa na ongezeko la asilimia 19, hata hivyo ongezeko hili ni dogo ukilinganisha na mahitaji yaliyotajwa na Mpango wa Taifa wa miaka mitano. 43
Mheshimiwa Spika, makadirio
ya mapato kwa upande wa makisio ya makusanyo ya maduhuli kwa mwaka
2012/2013 ni Shilingi 193,007,543,000. Kati ya makusanyo hayo, jumla ya
Shilingi 173,702,263,000 zitakusanywa na Idara ya Madini, Shilingi 19,
217,277,000 zitakusanywa na Idara ya Nishati na Petroli, na Shilingi
88,003,000 zitakusanywa na Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali
Watu. Kambi Rasmi ya Upinzani inataka Wizara ya Nishati na Madini
ichukue hatua zaidi za kuongeza mapato kwa kifungu cha 2001 cha Idara ya
Madini Kasma 140101 ya Ada za Madini na Kasma 140353 ya Mrabaha kwa
pamoja; maeneo hayo yakiongezewa usimamizi kwa mujibu wa matakwa ya
Sheria ya Madini ya mwaka 2010 na kanuni zake yana uwezo wa kulipatia
taifa kiasi kisichopungua bilioni 200 katika mwaka wa fedha 2012/2013.
Aidha, Wizara ya Nishati na Madini itoe maelezo iwapo matarajio ya
makusanyo katika Sekta ya Nishati na Petroli kifungu cha 3001 hususani
kasma 140274 yanajumuisha marejesho ya mapato ya mauzo ya gesi asili
yaliyopunjwa kati ya mwaka 2004 mpaka 2010. Kambi Rasmi ya Upinzani
inaitaka Serikali izingatie kuwa mapato katika shughuli za TPDC za
utafiti wa mafuta pamoja na mauzo ya gesi asili yanaweza kabisa
kuongezeka ziada ya makadirio ya makusanyo ya bilioni 19 tu iwapo
udhibiti katika gharama na ukaguzi wa mikataba utaongezeka katika mwaka
wa fedha 2012/2013. Pia ili kuongeza mapato kwa serikali na TPDC Kambi
Rasmi ya Upinzani inataka mrabaha wa asilimia 12 kwenye 44
gesi
uanze kutozwa kwa mujibu wa sheria na isitishe mara moja utaratibu wa
baadhi kuachiwa kutokulipa malipo husika kwa mujibu wa wa sheria.
Mapitio ya kitabu cha mapato yameonyesha kwamba wakati kwenye kifungu
cha 2001 cha madini kuna mrabaha hakuna kasma hiyo kwenye kifungu 3001
kinachohusika na gesi na mafuta.
Mheshimiwa Spika; Matumizi
ya Kawaida yanaombewa Jumla ya Shilingi 110,078, 868,000 kati ya fedha
hizo shilingi 17, 292, 347,000 ni kwa ajili ya mishahara (P. E) ya
Wizara na Mashirika yaliyo chini yake na Shilingi 92,786, 521, 000 ni
kwa ajili ya Matumizi Mengineyo (OC). Kambi Rasmi ya Upinzani inatoa rai
kwa wabunge na bunge kuungana pamoja kabla ya kupitisha matumizi haya
makubwa ya kawaida kwenye matumizi mengineyo pamoja na kuitaka Wizara ya
Nishati na Madini kubana matumizi kwa kupunguza matumizi yasiyo ya
lazima, Serikali itakiwe kutoa maelezo ya kina kuhusu matumizi ya
kifungu cha 1005 cha Kitengo cha Sheria ambacho kina kasma ya 229900
ambayo kwa mwaka wa fedha 2012/2013 kimetengewa kiasi cha Shilingi
4,000,000,000 kama gharama za utetezi wa Serikali katika kesi ya IPTL
ikiwemo kwa ajili ya kuilipa kampuni ya Mkono &Co. Advocates .
Izingatiwe kwamba katika mwaka wa fedha 2011/2012 Serikali ilifanya
uhamisho wa fedha wa kiasi cha Shilingi Bilioni 10 kwa ajili ya gharama
za kuendesha kesi zilizopo mahakamani zinazoihusu Wizara. Kambi Rasmi ya
Upinzani inaitaka Serikali kueleza jumla ya fedha zilizotumiwa na
Wizara kati ya mwaka 45
1995 mpaka
2011 kwa ajili ya kulipa makampuni binafsi ya uwakili kwenye kesi kubwa
za kitaifa na za kimataifa pamoja na kutaja orodha ya makampuni hayo.
Aidha, Serikali ieleze mkakati wa kudhibiti ongezeko la gharama za
kisheria ambazo ni mzigo mkubwa kwa mashirika ya umma na wananchi walipa
kodi kwa kuwa yamekuwepo mazingira ya kesi kuendelezwa kwa muda mrefu
na kugeuzwa kuwa vitega uchumi vya watu wachache. Mifano ya kesi
zilizodumu kwa muda mrefu ni ya IPTL ambayo Serikali inawakilishwa na
Mkono and Co. Advocates na ile ya Dowans ambayo Serikali imekuwa
ikiwakilishwa kwa nyakati mbalimbali na Rex Attorneys.
Mheshimiwa Spika, mwaka
2011 Benki ya Standard Hong-Kong ambayo ni mdeni mkuu katika sakata la
IPTL ilifungua kesi ya madai katika mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi
(ICSID case Na. ARB/10/20) inayodai kiasi cha dola za Kimarekani milioni
225, pamoja na riba katika kuendesha kesi hiyo. Katika muendelezo wa
Serikali kampuni ya uwakili ya Mkono ilipewa zabuni ya kuitetea Serikali
katika shauri hilo, na kwa kujiamini iliishauri Serikali kuwa kesi hiyo
kama Serikali tungeshinda pamoja na wanasheria wengine kuwa na maoni
kinzani kuhusu suala hilo. Lakini kutokana na uroho na kutaka maslahi
binafsi kwa Kampuni ya Mkono inaishauri Serikali isifanye usuluhishi nje
ya mahakama ya ICSID wakati wadai kupitia kwa Mfilisi wa Mali na Madeni
za IPTL wanakubali kusuluhishwa nje ya mahakama. 46
Mheshimiwa Spika, Kambi
Rasmi ya Upinzani Bungeni inaliona hili kuwa ni mchezo wa kuihujumu
Serikali ambao umekuwa ukifanywa na makampuni binafsi ya uwakili
kuchelewesha kesi ili yeye aendelee kulipwa mabilioni ya fedha za
walipakodi. Huu ni uhujumu wa kodi za wavuja jasho wa nchi hii.
Mheshimiwa Spika, katika
muendelezo huo huo Kampuni ya Mkono &Advocates kwa sababu ya uzoefu
wake wa kazi hiyo na ushawishi wake mkubwa kwa viongozi wa Serikali
imekuwa ni kawaida kwa kampuni hiyo kuingia mikataba kuzitetea Kampuni
za nje zenye kutiliwa shaka kama ilivyo Kampuni ya matangazo inayotoka
bara Asia inayojiita Asia Business Channel inayodai kutengeneza
matangazo ya biashara. Kampuni hiyo yenye mwelekeo wa kutaka kutapeli
ilitambulishwa kwa Mtendaji Mkuu wa TMAA na Waziri wa Nishati kipindi
hicho Mheshimiwa William Ngeleja kwa barua yenye Kumb. Na. AB 88/233/01
ya tarehe 8 Desemba, 2011. Lengo lilikuwa ni TMAA kuingia mkataba wa
kutangaza sekta yetu ya madini nje ya nchi.
Katika
biashara hiyo ya kulazimisha, kampuni hiyo iliitumia Kampuni ya Mkono
&Advocates kuandika barua ya kusudio la kuishtaki TMAA kama
itashindwa kuilipa kampuni ya ASIA BUSINESS CHANNEL kiasi cha paundi za
Kiingereza 35,500 kwa kazi ambayo majadiliano yalikuwa hayajafikia hatua
ya mwisho. Kambi ya Upinzani inajiuliza Kampuni hii kweli ni ya
wazalendo au ni ya watu ambao wanasukumwa na dhamira ya kufilisi
rasilimali za Watanzania? 47
Mheshimiwa Spika, Kambi
Rasmi ya Upinzani inaitaka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambayo
ina mamlaka ya kuiwakilisha Serikali katika kesi zote zinazoihusu
Serikali ieleze imechukua hatua gani kuhusu hali hii na ifungulie
mashtaka Kampuni zote zenye kuonyesha uzembe na hujuma katika kuishauri
serikali kwenye kesi mbalimbali za kitaifa na kimataifa zinazohusu
nishati na madini.
Mheshimiwa Spika, aidha,
kama Ofisi ya Mwanasheria Mkuu itashindwa kutekeleza hilo ni wazi
Mshauri huyo Mkuu wa Serikali katika mambo ya sheria atakuwa na yeye
ameshindwa kazi na hivyo ni bora awape nafasi watu wenye uwezo wa
kuangalia na kusimamia maslahi ya umma.
Mheshimiwa Spika, Miradi
ya Maendeleo imetengewa Jumla ya Shilingi 531, 190, 861,000 kati yake
Shilingi 431,190, 861,000 ni fedha za ndani na Shilingi 100,000,000,000
ni fedha za nje. Kati ya hizo kifungu cha 2001 cha Madini kimetengewa
katika Kasma 3152 Shilingi 240,000,000 tu tena za nje kwa ajili ya Uwazi
katika Tasnia ya Uziduaji (Tanzania Extrative Industries Transparency
Initiatives –TEITI) hivyo kutokana na umuhimu wa asasi hiyo katika
kuweka mfumo wa uwazi katika usimamizi na uvunaji wa rasilimali za
madini, mafuta na gesi asili ni muhimu kiwango cha fedha kikaongezwa na
kuhakikisha kwamba Sheria ya TEITI inatungwa katika mwaka wa fedha
2012/2013. Aidha, Taarifa zote tatu za TEITI (Reconciliation Reports)
ziwasilishwe na kujadiliwa bungeni. Kwa upande mwingine, bunge
lisikubali kupitisha kiasi cha Shilingi 40,000,000,000 kinachoombwa 48
kwenye
Kasma 3160 kwa ajili ya kulipia madeni ya Kiwira (KCPL) mpaka uhakiki
ufanyike juu ya uhalali wa viwango vya madeni husika kwa kuwa mradi
mzima uligubikwa na tuhuma za ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka.
Mheshimiwa Spika, kwa
upande wa Miradi ya Maendeleo ya Nishati na Petroli kifungu cha 3001,
Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali itoe maelezo kuhusu sababu za
kutekelezwa taratibu kwa mradi wa TEDAP (Kasma 3132) ambao iwapo
utaharakishwa utakuwa na mchango katika kuboresha mfumo wa gridi pamoja
na kuhamasisha matumizi ya nishati jadidifu kama vyanzo mbadala katika
uzalishaji umeme nje ya gridi. Aidha, pamoja na nyongeza ya fedha za
miradi ya maendeleo kwa ajili ya Wakala pamoja na Mfuko wa Umeme
Vijijini (REA/REF) (Kasma 3113); Kambi Rasmi ya Upinzani inasisitiza
umuhimu wa kuongeza kiwango cha fedha za ndani ili kufikia bilioni 150
ili kuharakisha kasi ya uzalishaji na usambazaji wa umeme vijijini. Pia,
kutokana na kasi ndogo ya usambazaji wa umeme, pamoja na kuondoa kodi
katika vifaa vya umeme wa jua, serikali ieleze hatua ilizochukua katika
kuweka mazingira wezeshi kwa vifaa vya umeme wa dharura kuweza
kupatikana kwa urahisi mathalani vifaa vya kuhifadhia umeme (invertors).
Kupitia Kasma 3147 Wizara ya Nishati na Madini inaomba 47,959,861,000
kwa mwaka wa fedha 2012/2013 kwa ajili ya kununua mafuta ya kuendesha
mitambo ya dharura, hivyo ni muhimu maelezo yakatolewa kuhusu matumizi
ya fedha za mafuta ya 49
mitambo ya dharura kwa mwaka wa fedha 2011/2012 ili kujenga uhalali wa matumizi ya mwaka huu wa fedha.
Mheshimiwa Spika, Wizara
ya Nishati na Madini inaomba shilingi 62,000,000,000 kwa ajili ya Mradi
wa Kuboresha Mifumo ya Umeme Katika Jiji la Dar es salaam (Kasma 3154).
Pamoja na mradi huo kuweka mkazo katika kufunga transfoma kubwa zaidi
na njia kubwa za umeme za msongo wa kV 33 kwa ajili ya wateja wakubwa wa
katikati ya Jiji; mradi uweke mkazo pia katika usambazaji wa umeme
pamoja na kuongeza nguvu ya umeme katika maeneo ya pembezoni ya Jiji la
Dar es salaam. Izingatiwe kwamba matatizo ya miundombinu ya umeme katika
Jiji la Dar es salaam kutoendana na kasi ya ongezeko la mahitaji ya
umeme hayapo katikati ya jiji pekee bali pia yapo maeneo ya pembezoni
yenye ongezeko la wakazi na vitega uchumi mbalimbali. Baadhi ya maeneo
hayo ni pamoja na Malambamawili, Kwembe, Goba Matosa, Msakuzi, King’ongo
na mengineyo katika Manispaa mbalimbali za Jiji la Dar es salaam.
Aidha, Wizara ieleze iwapo kiasi cha 10,000,000,000 kilichotengwa ajili
ya kulipa fidia wananchi wanaoishi katika maeneo hatarishi yanayozunguka
mitambo ya kuzalishia umeme ya Ubungo kitatosha kukamilisha kazi hiyo
kwa mwaka wa fedha 2012/2013 ili kuepusha uwezekano wa gharama
kuongezeka kutokana na riba ya kuchelewa kufanya malipo kama ilivyotokea
kwa miaka iliyopita. 50
Mheshimiwa Spika, katika
mwaka wa fedha 2012/2013 na kutokana na Mpango wa Dharura wa Umeme
uliopitishwa bungeni tarehe 13 Agosti 2011 Serikali imepanga kuanza
utekelezaji wa miradi ya MW 240 Kinyerezi ambao umetengewa shilingi
5,000,000,000 katika Kasma 3163 na MW 150 Kinyerezi ambao umetengewa
shilingi bilioni 13,000,000,000 katika Kasma 3164. Hata hivyo, kwa
miradi yote hiyo Serikali iko katika hatua ya majadiliano na kufunga
mikataba ya mikopo na Kampuni za SUMITOMO na Jacobsen wakati ambapo
michakato ya miradi hiyo ilianza toka mwaka 2009. Kambi Rasmi ya
Upinzani inarejea kuitaka Serikali kutangaza matatizo ya nishati ni
janga la taifa ili kuweka mfumo wa dharura wa kushughulikia kwa haraka
kwa usimamizi wa uongozi mkuu wa nchi tofauti na sasa ambapo miradi hiyo
inachukuliwa kuwa ni ya kawaida chini ya Wizara ya Nishati na Madini.
Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani inataka uhakika toka kwa Serikali iwapo
mitambo hiyo inayotarajiwa kutumia gesi itakamilika lini na iwapo
itapata nishati husika kwa wakati na kwa uhakika kwa kuzingatia
kuchelewa kuanza kwa ujenzi wa bomba la gesi. Pia, Serikali itaje miradi
mingine ya nyongeza ambayo utekelezaji wake unakusudiwa kuanza katika
mwaka wa fedha 2012/2013 ili kufidia pengo la mwaka wa fedha 2011/2012
na kuhakikisha kwamba kila mwaka wastani wa MW 360 za mitambo isiyokuwa
ya kukodi zinaingia katika Gridi ya Taifa katika kipindi cha utekelezaji
wa Mpango wa Taifa wa Miaka Mitano.
Mheshimiwa Spika, Mpango wa Taifa wa miaka mitano (2011/2012-51
2015/2016)
umelenga kuongeza uzalishaji wa umeme mpaka kufikia MW 2780 kwa
kuongeza MW 1788 kwa mujibu wa miradi iliyotajwa kwenye mpango kipengele
A.1.3 kuhusu nishati. Lengo hili ni dogo ukilinganisha na rasilimali
ambazo zipo katika taifa letu; hivyo Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka
Serikali kueleza imefikia hatua gani katika kufanya mapitio ya mpango
huo na kuongeza miradi mingine mikubwa ukiwemo wa Stiggler Gorge ambao
una uwezo wa kuzalisha MW 2100 kama nilivyopendekeza bungeni tarehe 14
Juni 2011 na kuingiza pia makadirio ya ujumla ya MW zinazotokana na
miradi midogo midogo itakayoanzishwa katika maeneo mbalimbali kama
tulivyoshauri tarehe 15 Julai 2011.
Mheshimiwa Spika,
ili kutekeleza miradi iliyosalia kwa wakati Kambi Rasmi ya Upinzani
inarudia kuitaka Wizara ya Nishati na Madini kueleza mazingira wezeshi
ambayo yanakusudiwa kuandaliwa ili miradi ifuatayo iweze kupata
rasilimali kwa wakati na makubaliano kukamilishwa mapema:
Iringa-Mchuchuma na Ngaka (Makaa ya Mawe-300), Kiwira (MW 200) , Singida
(Upepo) na Morogoro/Iringa- Ruhudji (Maji- MW 358).
Mheshimiwa Spika, ni
aibu kwa taifa kuendelea kutegemea vyanzo ambavyo vilianzishwa na
Serikali ya Awamu ya Kwanza iliyoongozwa na Hayati Mwalimu Nyerere, na
awamu zilizofuata sio tu zimeshindwa kuongeza kasi ya kuzalisha umeme
bali pia 52
zimeshindwa kukarabati
mitambo hiyo na hivyo kuzalisha chini ya kiwango. Taarifa ya Hali ya
Uchumi ya mwaka 2010 ilionyesha kwamba vituo vya kuzalisha umeme
vilikuwa vikifua umeme kwa wastani wa 53.5 tu ya uwezo wake; hivyo Kambi
Rasmi ya Upinzani inaitaka pia Serikali kueleza imechukua hatua gani
kwa mwaka 2011/2012 na inapanga kuchukua hatua gani za dharura kwa mwaka
wa fedha 2012/2013 kuhakikisha uwezo wa vyanzo vilivyopo kuzalishaji
unaongezeka sanjari na kupunguza upotevu wa umeme kutokana na ubovu wa
mifumo ya usafirishaji na usambazaji.
Mheshimiwa Spika; ili
kujiandaa kitaalamu kama taifa kwa mipango kabambe ya gesi wakati nchi
ikisubiri Sera ya gesi, Sheria ya Gesi na Mpango Kabambe wa Gesi (Gas
Master Plan) vinavyopaswa kuwasilishwa katika Mkutano wa Tisa wa Bunge.
Pia Kambi Rasmi ya Upinzani inataka Wizara ya Nishati na Madini ieleze
hatua iliyofikiwa katika kukamilisha mtaala wa uhandisi wa gesi na
mafuta ili fani hizo ziweze kutolewa kwenye Chuo Cha Madini Dodoma.
Aidha, wakati wa kuhitimisha mjadala wa mpango wa mpango wa taifa wa
miaka mitano tarehe 14 Juni 2011 serikali ilikubali pendekezo la
kuanzisha Chuo Kikuu cha Mtwara. Hata hivyo hicho hakijaingizwa kwenye
Mpango wa Taifa wa Miaka Mitano toleo la mwezi Juni 2012 kifungu cha
A.1.5. Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kueleza ni hatua zipi
zitaanza kuchukuliwa kwenye mwaka wa fedha 2012/2013 na Wizara ya
Nishati na Madini kwa kushirikiana na mamlaka nyingine zinazohusika
kuwezesha kuanzishwa kwa Chuo 53
Kikuu
hicho muhimu ambacho kitatoa mchango mkubwa kwa taifa katika masuala ya
mafuta na gesi na bidhaa zitokanazo na gesi na mafuta.
Mheshimiwa Spika,
katika kuimarisha sekta ya gesi na sekta kuwa na manufaa kwa nchi yetu,
narudia tena mapendekezo kama tulivyoyatoa katika hotuba ya Kambi Rasmi
ya Upinzani kama ilivyowasilishwa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani
katika hotuba yake Ofisi ya Waziri Mkuu nanukuu kama ifuatavyo:
"Mheshimiwa Spika, Kambi
ya Upinzani inatoa mapendekezo yafuatayo katika kuimarisha na kuboresha
sekta ya gesi na mafuta hapa nchini ili kuitayarisha nchi kwa utajiri
huu mkubwa:
i. Wananchi wanaozunguka maeneo yanayopatikana au yanayopitia gesi asili wawe sehemu ya mipango ya maendeleo ya gesi asili na hivyo kunufaika na matumizi ya gesi badala ya kuachwa, hali inayoleta manunguniko na tishio la uendelevu wa sekta husika na haswa ikizingatiwa kuwa uwekezaji unaofanywa katika sekta hii kama wananchi hawataona kuwa na wao ni wafaidika ni rahisi sana kuweza kuhujumu miundombinu hii na kuhatarisha usalama na hata uhai wa wananchi wengine .
ii. Ujenzi wa miundombinu ya gesi uwe unazingatia mahitaji ya muda mrefu ili kupunguza gharama na kuondokana na uhaba na uharibifu wa maliasili, mfano bomba la Songosongo liliwekwa bila kuzingatia mahitaji asili ya gesi na
i. Wananchi wanaozunguka maeneo yanayopatikana au yanayopitia gesi asili wawe sehemu ya mipango ya maendeleo ya gesi asili na hivyo kunufaika na matumizi ya gesi badala ya kuachwa, hali inayoleta manunguniko na tishio la uendelevu wa sekta husika na haswa ikizingatiwa kuwa uwekezaji unaofanywa katika sekta hii kama wananchi hawataona kuwa na wao ni wafaidika ni rahisi sana kuweza kuhujumu miundombinu hii na kuhatarisha usalama na hata uhai wa wananchi wengine .
ii. Ujenzi wa miundombinu ya gesi uwe unazingatia mahitaji ya muda mrefu ili kupunguza gharama na kuondokana na uhaba na uharibifu wa maliasili, mfano bomba la Songosongo liliwekwa bila kuzingatia mahitaji asili ya gesi na
54
hivyo kujikuta kuwa wanashindwa kusafirisha gesi ya kutosha kutumiwa na wahitaji wote; iii.
Tuwekeze kwenye kuwapa elimu na maarifa vijana wa Kitanzania na haswa kwenye Sekta ya gesi ili waweze kupata utaalamu wa jinsi ya kusimamia sekta hii kama ambavyo nchi majirani zetu wa Uganda na Msumbiji wamefanya kwa kuwapeleka vijana wao nje ya nchi ili kupata utaalamu juu ya uendeshaji wa sekta hii.
iv. Serikali iliahidi kwa Shirika la Fedha la Kimataifa kwamba Sheria ya usimamizi bora wa Fedha za Mafuta na Gesi (Petroleum Revenue Management act) italetwa Bungeni mnamo mwezi Novemba. Kambi ya Upinzani inasisitiza kwamba Sheria hii iletwe haraka ili kuweka wazi mapato yatokanayo na utajiri huu na namna bora ya kutumia fedha hizi ili kuzuia uchumi kuathiriwa na pia kuzuia ufisadi. Hatutaki Tanzania iwe kama nchi nyingine za Kiafrika ambazo utajiri wa Mafuta na Gesi umekuwa ni laana badala ya Neema.
v. Serikali iweke mazingira bora ya kujenga uwezo wa Watanzania kutoa huduma kwenye kila hatua ya utafutaji wa Mafuta na Gesi. Hivi sasa kuna zaidi ya wageni 1200 kwenye Meli za kutafuta Mafuta na Gesi katika Pwani ya Mtwara, Lindi na Pwani. Kwa masikitiko makubwa sana wageni hawa wanakula hata nyanya, mchicha na vitunguu kutoka nje ya Tanzania.
Tuwekeze kwenye kuwapa elimu na maarifa vijana wa Kitanzania na haswa kwenye Sekta ya gesi ili waweze kupata utaalamu wa jinsi ya kusimamia sekta hii kama ambavyo nchi majirani zetu wa Uganda na Msumbiji wamefanya kwa kuwapeleka vijana wao nje ya nchi ili kupata utaalamu juu ya uendeshaji wa sekta hii.
iv. Serikali iliahidi kwa Shirika la Fedha la Kimataifa kwamba Sheria ya usimamizi bora wa Fedha za Mafuta na Gesi (Petroleum Revenue Management act) italetwa Bungeni mnamo mwezi Novemba. Kambi ya Upinzani inasisitiza kwamba Sheria hii iletwe haraka ili kuweka wazi mapato yatokanayo na utajiri huu na namna bora ya kutumia fedha hizi ili kuzuia uchumi kuathiriwa na pia kuzuia ufisadi. Hatutaki Tanzania iwe kama nchi nyingine za Kiafrika ambazo utajiri wa Mafuta na Gesi umekuwa ni laana badala ya Neema.
v. Serikali iweke mazingira bora ya kujenga uwezo wa Watanzania kutoa huduma kwenye kila hatua ya utafutaji wa Mafuta na Gesi. Hivi sasa kuna zaidi ya wageni 1200 kwenye Meli za kutafuta Mafuta na Gesi katika Pwani ya Mtwara, Lindi na Pwani. Kwa masikitiko makubwa sana wageni hawa wanakula hata nyanya, mchicha na vitunguu kutoka nje ya Tanzania.
55 vi.
Vile
vile tudhibiti makampuni ya Ulinzi kutoka nje kuwa na silaha kali kali
kwa kujenga uwezo wa Jeshi letu la Majini (Navy) ili liwe na kikosi
maalumu kwa ajili ya kulinda meli za kutafuta mafuta na Gesi na
Makampuni haya yatozwe tozo maalumu. Ni hatari sana makampuni ya kigeni
kuwa na masilaha makubwa ndani ya ramani ya nchi yetu".
Mheshimiwa Spika, Kambi
Rasmi ya Upinzani Bungeni inaendelea kusisitiza kwamba muswada wa
sheria ya fedha wa mwaka 2012 uhakikishe misamaha wa kodi ya mafuta kwa
kampuni za utafutaji wa mafuta na Gesi inaondolewa. Izingatiwe kuwa
uzoefu kutokana na misamaha ambayo imekuwa ikitolewa kwa makampuni ya
madini unadhihirisha kwamba makampuni mengi yanatumia mwanya huo kuleta
mafuta yasiyo na kodi na kuyaingiza kwenye soko la ndani la reja reja.
Hivyo, misamaha hii haina maslahi kwa taifa na ni mianya mingine ya
uhujumu uchumi kwa kuwa kampuni za utafutaji mafuta na gesi zinayo fursa
kwa mujibu wa mikataba (PSA) kurejeshewa gharama zao mara baada ya
mafuta kupatikana. Aidha, uamuzi huu uhusishe pia kampuni za madini bila
kujali mikataba (MDA) kwa kuwa imethibitika kampuni hizi zote
hutengeneza faida nono bila kulipa kodi inavyostahili.
Mheshimiwa Spika, ili
kudhibiti hali hii ya ukwepaji kodi na kuongeza mapato ya serikali
katika mwaka wa fedha 2012/2013 Kambi Rasmi ya Upinzani inarudia kuitaka
Wizara ya Nishati na Madini ieleze 56
hatua
mahususi ambazo itazichukua kutekeleza mapendekezo yafuatayo: kutunga
Sheria ya kuhakikisha kwamba mikopo kwenye makampuni ya uwekezaji wa
madini katika mahesabu ya kodi isizidi 60% ya mtaji; kutunga Sheria
kuhakikisha kwamba riba ya mikopo kwenye makampuni yanayohusiana
haitaondolewa kwenye mahesabu ya kodi; kufanya marekebisho ya sheria
kuhakikisha kwamba kodi ya mtaji (capital gains) inatozwa katika
mauziano ya makampuni yote ya madini ambayo mali zake au uwekezaji wake
uko nchini hata kama mauziano hayo yamefanyika nje ya nchi kwa
kuzingatia kuwa mapendekezo yaliyoingizwa kwenye muswada wa sheria ya
fedha wa mwaka 2012 hayakuzingatia kwa ukamilifu msingi wa mapendekezo
yaliyotolewa na Kambi Rasmi ya Upinzani mwaka 2011. HITIMISHO
Mheshimimiwa Spika; kambi rasmi ya upinzani inapenda kuhitimisha kwa kusisitiza kwa mara nyingine kwamba kwa sehemu kubwa matatizo katika sekta za nishati na madini yamechangiwa na sababu za kibinadamu za kutowajibika ipasavyo kisera, kimaamuzi, kiusimamizi na kiutendaji kwa viongozi wa kiserikali wenye dhamana na watendaji wengine na hivyo kusababisha ugumu wa maisha kwa wananchi na kuathiri uchumi wa nchi. 57
Mheshimiwa Spika, mabadiliko
ya kimfumo yanahitajika ili kuwezesha hatua za haraka za kusimamia sera
sahihi, uongozi makini na taasisi thabiti katika sekta nyeti za nishati
na madini sanjari na kuchukua hatua kali dhidi ya ufisadi uliofanyika
katika sekta hizi, kufanya mapitio ya mikataba na kuharakisha
utekelezaji wa mipango kwa ushirikiano kati ya serikali na sekta
binafsi.
Mheshimiwa Spika, nimalize
kwa kuwashukuru wananchi wa Ubungo kwa ushirikiano wao katika kazi
nifanyazo za kuwawakilisha kwenye vyombo vya maamuzi na kuhamasisha
maendeleo Jimboni. Kwa namna ya pekee nitambue mchango wa madiwani wote
tunaoshirikiana katika kipindi ninachokuwa kwenye majukumu mengine ya
ujenzi wa taifa. Nawashukuru viongozi wa dini washauri wangu wa kiroho
na wanafamilia yetu ya Dalali kwa upendo na kuniasa kuendeleza ujasiri
na uadilifu katika kusimamia ukweli, haki na ustawi wa Jamii.
Mheshimiwa Spika,
natambua
kwa shukrani mchango wa viongozi wenzangu wa Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) makao makuu, Mkoa wa Kinondoni Kanda Maalum Dar e
salaam, Jimbo la Ubungo na wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika
wajibu wa kuwatumikia Watanzania na kuhamasisha mabadiliko katika taifa
letu. Hali tete na tata ya sasa inatutaka tuwe na mshikamano zaidi mpaka
kieleweke. 58
Mheshimiwa Spika;
nawashukuru
baadhi ya viongozi katika mamlaka mliotambua kwamba "siasa siyo uadui"
na kunipa ushirikiano kwenye serikali kuu, Wizara ya Nishati na Madini,
Manispaa ya Kinondoni, katika kamati ya nishati na madini na wabunge
wengine kwa ujumla katika kutekeleza majukumu ya kibunge kwa manufaa ya
taifa letu na watu wote.
Mheshimiwa Spika
,
baada ya kusema hayo naomba bunge lako lijadili mapitio ya utekelezaji
wa bajeti ya mwaka wa fedha 2011/2012 na makadirio ya matumizi ya Wizara
ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2012/2013 kwa kuzingatia maoni
tuliyoyatoa ya kuongeza bajeti ya wizara husika; kupokea mapendekezo ya
kuzingatiwa katika muswada wa sheria ya fedha wa mwaka 2012 na kupitisha
maazimio mahususi ya kuhakikisha sekta za nishati na madini zinachangia
kikamilifu katika kuinua uchumi wa nchi na kuboresha maisha ya
wananchi;
Mheshimiwa Spika; kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani naomba kuwasilisha
John Mnyika (Mb)
Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani
Wizara ya Nishati na Madini
27/07/2012
Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani
Wizara ya Nishati na Madini
27/07/2012
No comments:
Post a Comment