Sunday, September 16, 2012

Sudan Kusini yazamisha meli yake yenyewe

Wakuu wa Sudan Kusini wanachunguza sababu ya jeshi kushambulia na kuizamisha meli yao wenyewe kwenye Mto Nile.
Msemaji wa jeshi la Sudan Kusini Kanali Philip Aguer
Wanajeshi kumi walifariki na wengine hamsini wametoweka.
Msemaji wa jeshi la Sudan Kusini, Kanali Philip Aguer, amesema meli hiyo ilipita kituo cha ukaguzi usiku bila ya kusimama ingawa ilitakiwa kusimama.
Alisema meli hiyo ilikuwa imebeba wanajeshi kama 170.


No comments:

Post a Comment