Sunday, September 16, 2012
ALICHOSEMA MSTAAFU WA FREEMASONS KUHUSU MKAPA NA MWAI KIBAKI KUWEMO NDANI YA HICHO CHAMA.
Kwa longtime sasa hivi Tanzania imeshuhudia magazeti mengi pamoja na stori za internet kwenye blogs, website na facebook kuhusu Freemasons, kwa kiasi kikubwa baada ya hizo habari, picha iliyojengeka kuhusu Freemasons ni kwamba ni dini ya kishetani.
Wametajwa mastaa mbalimbali wa Tanzania pamoja na viongozi wa kisiasa kwamba nao wamejiunga na dini hiyo akiwemo rais mstaafu wa Tanzania William Mkapa na Rais Mwai Kibaki wa Kenya.
Exclusive kwenye THE INTERVIEW ya CLOUDS TV Mtangazaji Gerald Hando amefanya interview na Sir Andy Chande ambae alikua freemasons lakini kwa sasa amestaafu.
Moja kati ya mambo aliyoyazungumzia ni pamoja na taarifa za Kibaki na Mkapa kuwemo kwenye hicho chama, hapa namkariri akisema “Hakuna hata mmoja kati ya mkapa wala kibaki ambae ni Freemason, nilipofika hapa mwaka 1950 katika biashara zangu nilikutana na watu wengi katika Nyanja mbalimbali ambao walikuwa wakiandaa chama cha freemasons ambao walinialika kwenye vikao mbalimbali Uganda, Kenya, uingereza na kwingineko kama Ghana na Khumasi ila nikastafu baada ya miaka 19 kufanya kazi na freemasons.
Sihusiki tena na freemasons huku Tanzania, ila kama uingereza naenda mara kwa mara kwa sababu bado kuna baadhi ya mashirika ninayofanyakazi nayo hadi sasa, Freemasons sio kama watu wengi wanavyosikia au kuambiwa.. kuna tofauti”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment