Monday, July 16, 2012

LAMAR AKANUSHA KUTOA RUSHWA


Produza na mmilikiwa studio maarufu ya muziki Bongo, Fishcrub, Lamar Niekamp amekanusha tetesi za kutoa rushwa kwa baadhi ya watangazaji na ma-Dj wa vituo vya redio nchini kwa lengo la kupewa chapuo kwa nyimbo zilizopita kwenye mikono yake.

Lamar anayeshikilia tuzo mbili za KTMA kama Produza bora amefunguka kuwa kamwe hajwahi kufanya jambo kama hilo isipokuwa kinachotokea ni ubora wa ngoma zinatoka kwenye studio hiyo kwa kufuatana na kujikuta zikipata airtime kubwa kwenye media kwa wakati mmoja.
“Kinachotokea ni ubora ngoma ambazo mimi nazifanya, hakuna kitu kingine ,lakini kikubwa ni kuwa ninapowapa wasanii kazi zao wao ndiyo hujikuta wanazigonganisha kwenye vituo vya redio kutokana na haraka zao ndiyo maana unaweza kukuta nyimbo zaidi ya tano ambazo zote nimetangeneza mimi zinapata airtime kwa wakati mmoja” alisema Lamar.

No comments:

Post a Comment