Tuesday, July 17, 2012

Ikithibitika tu! Baba ba mama Lulu matatani

Yasemekana endapo Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam Julai 23, mwaka huu itamaliza utata wa umri wa Elizabeth Michael ‘Lulu’ na kuthibitisha umri aliokuwa nao wakati anapata mkasa wa kifo cha Steven Kanumba, kuna uwezekano wazazi wake, mzee Michael Kimemeta na Lucresia Karugila wakaingia matatani.
Kwa mujibu wa mtaalam wa sheria (jina linahifadhiwa), bila kuingilia uhuru wa mahakama alisema kuwa kuna vipengele vya sheria vinaweza kuwabana kwa kigezo cha malezi ya mtoto.
“Kwa mfano The Law Of The Child Act ya 2009, inaainisha kuwa mzazi anatakiwa kusimamia malezi ya mtoto kwa kumpatia mahitaji muhimu kama chakula, malazi, matibabu na mengineyo na ikithibitika yanakiukwa, hatua ya kwanza kisheria yawezekana mzazi akapokonywa mtoto na kulelewa chini ya mahakama,” alisema na kuongeza:
“Kwa maana hiyo, kama ikithibitika wazazi wa Lulu walikuwa wakishindwa kumzuia mtoto kushiriki katika matendo yanayokinzana na haki za mtoto (au kushindwa kumtimizia haki zake) basi kwa namna moja au nyingine wanaweza kuingia matatani.”

No comments:

Post a Comment