Tuesday, July 17, 2012

NDOA YA HEMED YAKWAMA, KISA ELIMU NDOGO

NDOTO kufunga pingu za  maisha  siku za  karibuni alizokuwanazo nyota  kutoka 'Bongo moive' Hemed Suleiman 'PHD', zimeota mbawa kufuatia  wazazi wa mlimbwende aliyetaka kumuoa kuweka ngumu.
katika mahojino ya dakika kadhaa aliyofanya  na  chanzo chetu, Hemed amesema kuwa tayari alikuwa ameanza taratibu za kushughulikia ndoa yake na mrembo huyo iliyopangwa kufungwa  kimya kimya  kwa kuogopa watu wenye nia mbaya   lakini amejikuta akilazimika kustisha harakati hizo kufuatia wazazi wa binti huyo wakaweka ngumu kwa madai kuwa wanataka mtoto wao amalize kwanza  masomo yake  na kupata 'mastaz' kwa kuwa  elimu ya  Degree aliyonayo hivi sasa wanahisi bado haijamtosha.
 "unajua mchumba  wangu hivi sasa ana elimu ya degree hivyo wazazi wamesema kwao hiyo bado ni elimu ndogo hivyo hawezi kuruhusu jambo hilo kwanza  mpaka apate 'mastaz' halafu ndiyo mambo mengine yatafuata, imeniuma sana kwa kuwa wenyewe tulishakubaliana na mwenzangu alikuwa tayari kwa hilo" alisema  Hemed.

 katika hatua  nyingine Hemed ameiambia teentz.com kuwa yuko katika  hatua za mwisho kutoa  muvi yake mpya aliyoibatiza jina  la Mererani ndani yake akiwa amemshirikisha  swahiba wake wa  kitambo Yusuf Mlela sambamba na wakali wengine kibao wanaofanya  kweli na  Bongo movie
wakati huo huo nyota huyo amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula tayari kwa ujio wa ngom ayake mpya  iliyopewa jina  la  Mama Kimbo sambamba na video yake ambayo soon itakuwa hewani  kupitia chanzo chetu.

No comments:

Post a Comment