Tuesday, July 17, 2012

STAA BONGO MOVE APIGWA STOP KUIGIZA


Nyota  kutoka tasnia ya  filamu Bongo Skyner Ally huenda asionekane tena kwenye ulimwengu wa move kufuatia kupigwa  stop kushiriki katika  kuigiza.
Stori  'under carpet' ambazo chanzo chetu imezinyaka kutoka kwa mmoja wa wapambe wa mwigizaji huyo aliyeng'arisha nyota yake kupitia filamu ya  'SECOND WIFE' iliyopikwa na mkali Ray Kigosi, zinasomeka kuwa  Skyner amepigwa stop na  wazazi wa  upande pili  (wakwe) ili aweze kulea vizuri mtoto wake badala ya kutumia muda mwingi akiwa kambini na waigizaji wengine kwa ajiri ya kurekodi 'muvi'.

"amezuiwa, na sijui kama ataruhusiwa kipindi cha  karibuni  na  huenda  ikawa moja kwa moja  kwani ameambiwa atulie alee familia na mtoto wake, alisema mpambo huyo.

"kuona hivyo, chanzo chetu ilimvutia waya  msanii  huyo na  majibu yake yakawa  hivi: unaweza kuona nimezuiwa lakini kwangu mimi sijachukulia hivyo kilichopo ni kuwa  nimetulia kwanza nilee mtoto wangu na familia pia, kwa sasa nipo Tanga nimekuja kusalimia ndugu na baada ya muda nitarejea Dar halafu ndiyo nitatoa jibu kamili kama  nitaendelea ama la" alisema Skyner.

No comments:

Post a Comment