Thursday, July 19, 2012

JUSTINE BIEBER AFURAHIA UMRI WA MAMA YAKE


Justin Bieber amesema kuwa karibu mno na mama yake kiumri, ambaye alimzaa akiwa na miaka 18, kumewafanya wawe marafiki.
Akizungumza na 2Day FM, Justin amesema: "She's amazing'... Ni wazi nilikuwa kama ajali kwake, ni poa sana mama yangu bado ni mdogo, ni rafiki na mama yangu pia, amekuwa strict sana siku zote, ameniweka kwenye mstari.”
Katika mahojiano hayo Justin alizungumzia pia jinsi ambavyo huwa haoni shida kuperform mbele ya maelfu ya watu lakini hupata shida kubwa anapotaka kuongea mbele yao.
Alieleza:"Napenda kuperform, kupiga tour na kuwa na umati mpya wa watu kila usiku, ni kitu nikipendacho siku zote.. Ni ajabu kuwa naweza kuperform mbele ya watu wengi lakini ukifika wakati wa kuongea napata shida, sijui kabisa jinsi ya kuzungumza mbele ya watu wengi."
Aidha Justin alizungumzia pia mipango ya kufanya filamu ambapo amesema ameanza mazunguzo na muigizaji Mark Wahlberg kufanya filamu mpya.


No comments:

Post a Comment