Saturday, July 14, 2012

KAULI KAMILI KUTOKA KWA MMILIKI WA FACEBOOK KUHUSU KUFUNGA FACEBOOK


PALO ALTO  – Facebook continues to deny rumors it is shutting down on July 15th of 2012.  WWN, however, has confirmed that it is true.
On January 9th, WWN’s ace reporter, J.B. Smitts, broke the international story that Facebook was going to close down on July 15th because Mark Zuckerberg wanted to return to a normal life.   The story caused a worldwide sensation, and J.B. Smitts has been nominated for a Pulitzer Prize for breaking it.

Maneno 8 ambayo ni sumu kumwambia mwenzi wako


Unapokuwa faragha na mpenzi wako, kuna baadhi ya mambo unatakiwa kuyaepuka kwani yanaweza kutibua hali ya hewa na mwishowe kutopata ile furaha mliyodhamiria.
Achilia mbali hayo ya kufanya, pia kuna maneno ambayo unatakiwa kujichunga sana kutoyatamka pale unapokuwa kwenye uwanja wa kujidai na mpenzi wako. Haya nayo madhara yake ni makubwa kwani yanaweza hata kuufanya uhusiano wenu ukafikia tamati. Maneno hayo 8 ni haya yafuatayo;

Wema avamiwa na Majambazi na kumkomba vitu kadhaa


SIKU chache baada ya kuanika utajiri wake, staa wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu (pichani), amevamiwa na majambazi na kukombewa vitu kadhaa huku gari lake aina ya Toyota Lexus lenye namba za ujsali T 211 BXR likinusurika kuibwa, Ijumaa lina kila sababu ya kukujuza.
Tukio hilo lilijiri usiku wa kuamkia Julai 9, mwaka huu, nyumbani kwake Kijitonyama, jijini Dar es Salaam ambapo majambazi hayo yaliingia ndani kwake kwa kuruka ukuta licha ya kwamba kuna walinzi wawili.
KIKWAZO CHA NGUVU
Hata hivyo, baada ya kuzamia ndani ya geti, majambazi hayo yalishindwa kuingia ndani kabisa kutokana na milango madhubuti iliyopo kwenye nyumba hiyo ya kisasa.


Friday, July 13, 2012

Nafasi za Kazi 30 13 july



Barnaba anaswa na Gubegube wakitoka gesti

Siku chache baada ya mwanamuziki Barnaba Elias kutangaza kujaaliwa mtoto wa kiume aliyezaa na mwanamke anayeishi naye, msanii huyo hivi karibuni alinaswa akiwa na demu mwingine kwenye nyumba ya kulala wageni mjini hapa.
Barnaba alifika Zanzibar kwa ajili ya kufanya shoo kwenye Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF) linaloendelea Kisiwani Unguja ambapo paparazi wetu akiwa kwenye gesti ya Malindi alimuona binti mmoja akiingia na kumtaka mhudumu ampe funguo za chumba alicholala msanii huyo.
“Mimi naomba unipe funguo za chumba atakacholala Barnaba kwani ndicho nitakacholala,” alisema binti huyo ambaye inadaiwa alitokea Dar.
Kauli hiyo ilimshangaza mhudumu wa mapokezi ambaye alimtaka demu huyo kurudia alichokisema na jibu likawa:

Aunt Ezekiel ana mimba ya miezi sita




SIKU chache baada ya staa wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel kuripotiwa kufunga ndoa mjini Dubai, mchumba wa staa huyo aliyetambulika kwa jina moja tu la Jeff amesema kuwa, anashangazwa na Aunt kuolewa huku akiwa na ujauzito wake, Amani linashuka na mistari ya habari hii.
Akizungumza na Amani jijini Dar hivi karibuni, Jeff amesema kuwa taarifa za kuolewa kwa Aunt alizipata akiwa nchini China na kushtuka sana.
“Kinachonishangza ni huyo jamaa anafungaje ndoa na mwanamke ambaye ana ujauzito wangu wa miezi sita ambao aliondoka nao kwenda Dubai?” alihoji Jeff.
Jeff aliendelea kutiririka kama mtu alikuwa akiimba mashairi ya Muziki wa Injili kuwa, kingine kinachomuumiza ni tabia ya Aunt kumuomba fedha za matumizi akiwa Dubai huku akijua kwamba amefunga ndoa na mtu mwingine.
“Wanawake ni mama zetu lakini ni wauaji wakubwa, inakuwaje anagawa mimba ya mtu kwa mwanaume mwingine halafu mbaya zaidi nilipokuwa China kila wiki alikuwa akiniomba fedha za matumizi nami nikawa namuagiza aende sehemu kuchukua kumbe ni mke wa mtu!” alishangaa Jeff.

Kuwa makini na vyakula vya super market




EMPLOYMENT OPPORTUNITIES: Bank of Tanzania




EMPLOYMENT OPPORTUNITIES
The Bank of Tanzania, an equal opportunity employer and Tanzania’s central bank, is looking for
suitably qualified Tanzanian citizens of high personal integrity to fill the following vacant positions at BOT Headquarters, Dar es Salaam and its Branches.

Mnyika awasilisha ushahidi wizi BoT

Hatimaye Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika, amewasilisha ushahidi wa awali kwa Katibu wa Bunge, kuhusu tuhuma alizozitoa bungeni dhidi ya Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM), Mwigulu Nchemba, kwamba ni mmoja wa watuhumiwa katika kashfa ya ukwapuaji wa mabilioni ya fedha uliofanywa katika Akaunti ya Malipo ya Nje (Epa) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Thursday, July 12, 2012

FILAMU YA KUCHANGIA MATIBABU YA SAJUKI KUZINDULIWA JIJINI ARUSHA


Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu, akielezea jambo wakati akiongea na waandishi wa habari siku ya jana katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Jijini Dar es salaam, juu ya uzindi wa Filamu ya SAYLA, filamu ambayo ni muendelezo wa harambee za kumsaidia msanii mwenzao wa filamu hapa nchi Sajuki, filamu ambayo itaazinduliwa katika mikoa minne ya Dodoma, Dar es samaam,Morogoro na Arusha, kulia ni Mke wa Sajuki Wastara Juma" wastara"

Dada poa aibua varangati kwa mteja wake


TIMBWILI la aina yake limeibuka baada ya msichana mmoja aliyedaiwa kuwa changudoa kumng’ang’ania njemba moja iliyojulikana kwa jina moja la Shabani kwa madai kwamba alimkimbia gesti bila kumpa fedha yake baada ya kumla uroda.

Komba Hoi INDIA


    MBUNGE wa Mbinga Magharibi Kepteni mstaafu, John Damian Komba anadaiwa kuwa yuko hoi nchini India alikokwenda kwa ajili ya matibabu, Risasi Mchanganyiko lina mkoba uliojaa habari hii.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vimeeleza kuwa Mhe. Komba aliondoka nchini wiki iliyopita.
Komba ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kundi la Sanaa za Maonesho la Tanzania One Theatre (TOT) alikwenda nchini humo kwa ajili ya kucheki afya yake lakini amelazimika kufanyiwa upasuaji wa nyonga baada ya kushauriwa na madaktari.
“Awali alikuwa amekwenda kwa lengo la kuangalia afya yake lakini baada ya kufanyiwa uchunguzi akagundulika kuwa ana matatizo ya nyonga, hivyo akatakiwa kufanyiwa upasuaji haraka sana,” kilisema chanzo chetu kimojawapo.
Mmoja wa ndugu wa karibu na Komba, kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini kwa vile yeye siyo msemaji wa familia, alithibitisha hilo.
Huyu hapa anazungumza: “Ni kweli mzee amekwenda India. Tunashukuru Mungu ameshafanyiwa
upasuaji na anaendelea vizuri. Muhimu kwa Watanzania ni kumuombea dua apone haraka.”

Wednesday, July 11, 2012

ALERT FOR MOBILE PHONE USERS

[NOT SO SURE WITH THIS "ALERT"]!
PLEASE SHARE THIS Use only your LEFT EAR when using Mobile Phones, and avoid using the RIGHT EAR , as that makes our brain more prone to mobile radiation. This was found out by a latest research from Apollo Medical Team . Please share this info with your loved ones Use only your LEFT EAR when using Mobile Phones, and avoid using the RIGHT EAR , as that makes our brain more prone to mobile radiation. This was found out by a latest research from Apollo Medical Team . Please share this info with your loved ones

VIFO vya wapendanao wawili


VIFO vya wapendanao wawili, Yusuph Badi na mchumba wake aliyefahamika kwa jina la Pendo waliofariki dunia Keko Toroli jijini Dar es Salaam kutokana na kuungua kwa moto vimezua utata baada ya mwanaume kukutwa akiwa amekaa kando ya mwanamke ambaye alikutwa akiwa amelala chali chumbani.
Mwandishi wetu aliyefanya uchunguzi wa vifo vya wapendanao hao, aliambiwa na mashuhuda kuwa tukio hilo limezua utata baada ya wawili hao kukutwa katika hali hiyo na hakukuwa na hitilafu ya umeme na marehemu hao hawakuwa na mshumaa wala kibatari chumbani mwao.
Rafiki wa marehemu Pendo, aliyejitambulisha kwa jina la Fatuma alikuwa na haya ya kusema: “ Nilifika nyumbani kwa Pendo jioni ya Julai tano mwaka huu na tukazungumza hadi saa tano usiku nikaondoka. Saa saba nikapata taarifa kuwa nyumba yao imeteketea kwa moto.
“Mazingira waliofia hawa wenzetu yana utata mkubwa, watu wanajiuliza moto huo umetokana na nini kwa kuwa ndani ya chumba chao hakukuwa na mshumaa wala kibatari, walikuwa wakitumia tochi tu,” alisema Fatuma.
Naye mjumbe wa mtaa huo wa Keko Toroli, Zubeda Sobo alisema: “Nilisikia watu wakilia katika nyumba hiyo huku moto ukiwaka. Niliamuru watu wafungulie mota kwa ajili ya kusukuma maji ya kuuzima moto.
“Baadaye tulifanikiwa kuingia ndani na kukuta maiti ya mwanaume ikiwa imeketi kwenye kiti na mwanamke akiwa amelala chali kitandani, ajabu ni kwamba chaga za kitanda, simu na noti ambazo zilikuwa kwenye waleti, hazikuungua.
“Kwa kweli nashindwa kuelewa mazingira ya moto huu na wananchi wengi tumepigwa na butwaa,” alisema kwa masikitiko mjumbe huyo.
Alibainisha kuwa polisi na zima moto walifika moto ukiwa umeshazimwa na wananchi.
Marehemu Yusuph alizikwa katika makaburi ya Chang’ombe na Pendo alisafirishwa Ijumaa wiki iliyopita kwenda Arusha kwa mazishi.

Ang'atwa pua kisa kutembea na mume wa jirani yake


        Kutembea na mwenzi wa jirani yako wanasema zingua udanje. Mama wa nyumbani Mrs. Ruka Amoha ambae anadai kuwa mumewe amemnyima unyumba kwa miezi kadhaa sasa, ameamua kutoa hasira zake kwa jirani Mrs. Yemi Adelani.
“siwezi kukubali Yemi amfaidi mume wangu na wake pia kwa wakati mmoja nakufanya mi nishindwe kumfaidi mume wangu"amesema ruka mama mwenye watoto watatu.
Tukio hili limetokea Lagos, Nigeria na Dr Oriele Agege amekubali kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa pua ya Yemi imeumizwa sana na anahitaji kufanyiwa  plastic surgery to survive.

Tuesday, July 10, 2012

Wema Sepetu aitwa Ikulu ya TZ

 Wema Isaac Sepetu.

WEMA Isaac Sepetu amelidokeza gazeti alipendalo la Ijumaa Wikienda kuwa ameitwa ikulu ya Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza kwa mwaliko maalum.
Wema alisema mwaliko huo aliupata mara tu baada ya kuzindua ile filamu yake ya Super Star wiki mbili zilizopita ambapo katika mwaliko huo wa ujumbe kutoka ikulu hiyo ulimuomba kutoisambaza kwanza kabla ya kwenda kuizindua nchini humo.
 
“Waliniambia juu ya mimi kuomba uraia wa nchi hiyo ili kukuza filamu zao. Kusema kweli nilikuwa nina ratiba ya kwenda kuizindua filamu yangu Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Yaani sijui hata walijuaje. Sijui ni nini kimetokea, nina wasiwasi. Hata sijui nitaongea nini na Rais wa Burundi,” alisema Wema na kuongeza kuwa maandalizi yakikamilika atatii wito huo muda wowote.

Kigogo anataka kuwaua baadhi ya wabunge wa chadema



MBOWE ASEMA MPANGO HUO UNARATIBIWA NA KIGOGO WA USALAMA WA TAIFA, MKUCHIKA ASEMA NI TUHUMA NZITO, AZIVUTIA KASI
 

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),kimetoa tuhuma nzito kikidai kigogo mmoja (jina tunalo) wa Idara ya Usalama wa Taifa anaratibu mpango wa kuwaua viongozi wake waandamizi akiwamo Katibu Mkuu, Dk Willbrod Slaa na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika.
Kwa sababu hiyo, chama hicho kimeitisha kikao cha Kamati Kuu (CC) leo kujadili mambo mbalimbali na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe amesema ajenda kuu itakuwa kuzungumzia usalama wa viongozi wao kutokana na vitisho hivyo.
Kuhusu tuhuma hizo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), George Mkuchika amesema tuhuma hizo ni nzito na atazijibu kwa maandishi.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika Dar es Salaam jana, Mbowe alitaja majina ya baadhi ya maafisa idara hiyo (majina tunayahifadhi) na kudai kuwa mmoja kati yao ndiye anayeratibu shughuli hiyo na tayari yupo mjini Dodoma kwa ajili ya kuongoza  kundi linalotaka kumdhuru Mnyika.
 
Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alisema mbali na viongozi hao wawili, mwingine aliyedai kuwa anafuatiliwa ni Mjumbe wa Kamati Kuu, Godbless Lema akidai kwamba, taarifa zinaonyesha kuwa wanafuatiliwa kwa saa 24.
Mbowe alidai kwamba idara hiyo ambayo haifanyi shughuli za siasa, inatumia ofisi yake vibaya kwa kufuatilia viongozi hao wakidhani chama hicho kina mambo ya siri kinayotaka kuyafanya katika nchi hii.
 
“Sisi Chadema hatuna mambo ya siri tunayotaka kufanya katika nchi hii. Matatizo ya Watanzania yapo wazi na yanajulikana na kila mmoja, Serikali ya CCM itekeleze sera na ahadi zao kwa wananchi na si vitisho,” alisema Mbowe na kuongeza:
 
“Tunaomba wananchi waelewe kuwa viongozi wao wako hatarini, lakini Chadema hatutarudi nyuma katika kutetea haki  za wanyonge hata kwa kufa na hatuwezi kupeleka malalamiko yetu polisi sababu nao ni sehemu ya tatizo.”
 
Alisema chama chake kimekuwa kikihusishwa na mambo mengi ukiwamo mgomo wa madaktari unaoendelea na kusema Chadema hakiko nyuma ya mgomo huo na hakijawahi kukutana na kufanya kikao na madaktari.
 
“Wametuhusisha na mambo mengi na sasa wanasema tuko nyuma ya mgomo wa madaktari, taarifa hizo siyo za kweli na wala hatujawahi kukaa nao kikao chochote kujadili masuala yao, madaktari wana madai ya haki zao. Hapa tunaingia kwenye utaratibu wa kutesana ili kupata taarifa, mmesikia Dk Ulimboka aliteswa ili aseme Chadema iko nyuma ya mgomo,” alidai Mbowe.
 
Hata hivyo, Mbowe alisema suala la kutokuwa nyuma ya mgomo huo haliwanyimi fursa ya kutetea makundi ya watu wanaodai haki zao wakimwamo madaktari na kusema anaunga mkono tamko la viongozi wa dini.
 
“Viongozi wa dini wametoa tamko lao jana (juzi), wakitaka Serikali kuwarudisha madaktari na kumalizia suala hilo kwa njia ya mazungumzo,” alisema.
Alisema Chadema kinaunga mkono tamko hilo akisema si busara kuwa fukuza kwa sababu Serikali imetumia gharama kuwaandaa.
Dk Slaa anena
 
Kwa upande wake, Dk Slaa alisema Chadema kimeamua kutotoa madai yake polisi akidai kuwa imepokea madai mengi kutoka kwa viongozi na wanachama ya kutendewa visivyo lakini hakuna hata moja lililowahi kufanyiwa kazi.
Kuhusu kitisho la kuuawa alidai kwamba alianza kutishiwa siku nyingi na kusisitiza kuwa hilo haliwezi kuwanyamazisha.
 
“Taarifa za sasa wanaanza na Mnyika na kufuatia mimi, ninachosema wafanye watakavyo hatutaacha kufanya kazi yetu, hata nilipoibua tuhuma za EPA niliwaambia watuhumiwa wengine wa sakata hilo ni Usalama wa Taifa,” alisema Dk Slaa.
 
Dk Slaa alitaja baadhi ya mambo ambayo alidai kuwa hayakushughulikiwa yalipowasilishwa polisi kuwa ni vinasa sauti alivyowekewa kwenye chumba alichokuwa amelala wakati wa vikao vya Bunge Mjini Dodoma.
Alisema vifaa hivyo vilichukuliwa na polisi kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi lakini hadi leo hakuna taarifa iliyotolewa hata kwake licha ya kuwa mhusika mkuu.
Mnyika: Namwachia Mungu
 
Akizungumzia madai hayo, Mnyika alisema anamuachia Mungu kwa kuwa ndiye aliyetoa uhai hata kwa hao wanaofikiria kutekeleza kitendo hicho.
Mnyika alidai kuwa baada ya kupata taarifa hizo ambazo alisema zimeandaliwa kwa ama kunyeshwa sumu au kuvamiwa na majambazi, alikutana na familia yake na uongozi wa chama chake ambao kwa pamoja wamemtaka aendelee na kazi ya kutetea rasilimali za taifa.
 
“Nilipopata taarifa hizi nimekutana na viongozi wangu wa chama na jana usiku (juzi), nilikutana na familia yangu, kwa pamoja wameniambia niendelee na kazi hii ninayoifanya kwani nimetumwa na wananchi na sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, ”alisema Mnyika.
Kwa upande wake, Lema alisema  taarifa za kufuatiliwa na watu hao wanaodaiwa kuwa ni wa Usalama wa Taifa alizipata kwa mmoja wa vyanzo vyake kutoka serikalini.
 
“Nilipigiwa simu na mtu mmoja kutoka serikalini aliyeniambia kuna gari nyuma linanifuatilia, nilipogeuka niliona na kusimama kisha nikashuka na kubadili gari na lenyewe likaendelea kunifuatilia katika gari nililokuwa nimepanda,” alidai  Lema.

Lema alidai kwamba hata juzi asubuhi alikutana nalo katika nyumba aliyofikia na alipolikaribia watu hao walishusha vioo na kumsalimu wakimwita ni Mbunge wa Arusha aliyeko kwenye likizo.

Mapokezi ya Dr. Asha Rose Migiro akirejea nchini



Mratibu Mkazi wa Umoja Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou (katikati) akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere kumpokea Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dr. Asha Rose Migiro aliyemaliza muda wake leo wakati akirejea nchini Tanzania. Kushoto ni Afisa wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini Hoyce Temu.

Baadhi ya Mabalozi, Wahadhiri na Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakiwa wamejipanga kumpokea Dr. Asha Rose Migiro.

Msafara wa Dr. Asha Rose Migiro ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Mh. Benard Membe (gari la pili) kuelekea sehemu maalum ya mapokezi.

Dr. Asha Rose Migiro akishuka kwenye gari yake baada ya kukanyaga Ardhi ya Tanzania.
Dr. Asha Rose Migiro akipokelewa kwa shangwe na zawadi za maua kutoka kwa ndugu, jamaa, marafiki na wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje waliofika kumlaki.
Dr. Asha Rose Migiro akisalimiana na baadhi ya mabalozi wapya walioteuliwa na Mh. Rais hivi karibuni. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou.
Dr. Asha Rose Migiro akiendelea kusalimiana na Baadhi ya Mabalozi. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Benard Membe sambamba na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou.
Waziri Membe na Dr. Migiro wakielekea kwenye chumba maalum cha mapumziko kabla ya mkutano na waandishi wa habari.
Dr. Asha Rose Migiro (katikati), akizungumza na waandishi wa habari nchini Tanzania baada ya kumaliza muda wake kama Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambapo pamoja na mambo Mengi amesisitiza kwamba hatojihusisha na siasa kwa sasa. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Benard Membe na Kulia ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou.
Dr. Asha Rose Migiro akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe.
Dr. Asha Rose Migiro (katikati) akiteta jambo Waziri Membe sambamba na Viongozi mbalimbali wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini wakiongozwa na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dr. Alberi Kacou (kushoto) waliofika kumlaki katika Uwanja wa Ndege wa Mwl. J.K Nyerere.
Mbunge wa Singida Mjini Mh. Mohammed Dewji akimpongeza Dr. Asha Rose Migiro kwa kazi nzuri alipokuwa akitumikia kama Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa walipokutana leo katika Uwanja wa ndege.
Pichani Juu na Chini ni wakinamama wakimwimbia Happy Birthday Dr. Asha Rose Migiro ikiwa ni maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa aliporejea nyumbani leo.
Kikundi cha Ngoma kikitoa burudani kwa Dr. Migiro (hayupo pichani)
Dr. Asha Rose Migiro akizungumza Jambo na Dr. Alberic Kacou wakati wakitizama burudani ya ngoma iliyoandaliwa maalum kwa ajili yake. Kushoto ni Waziri Membe.
Dr. Migiro akiwasalimia wasanii wa kikundi cha ngoma.
"Karibu tena Nyumba Mama"... Waziri Membe akiagana na Dr. Asha Rose Migiro baada ya mapokezi.
Dr. Asha Rose Migiro akiagana na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Dr. Alberic Kacou.
Dr. Asha Rose Migiro akiondoka katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere sambamba na ulinzi mkali wakiwemo maafisa wa kimataifa kutoka Ufilipino waliohakikisha ametua nchini Salama.
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) ambaye amemaliza muda wake, Dk. Asha Rose Migiro, amerejea nyumbani leo na kusema kwamba anatarajia kurudi kufundisha katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako alikuwa akifundisha kabla ya kuingia kwenye ulingo wa siasa. Kinyume na matarijio ya watu wengi, Dk. Migiro amesema kuwa kwa sasa hatarajii kujishughulisha katika mambo ya siasa na wala hana mipango ya kugombea urais siku za mbele.
Amesema kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amamteua kuwa Balozi Maalum wa Malaria katika Bara la Afrika na kuongeza kuwa pamoja na kwamba shughuli hizo atakuwa anazifanya kwa muda wake mchache, bado kuna uwezekano mkubwa zikambana na kushindwa kujishughilisha na mambo ya kisiasa.