Tuesday, July 10, 2012

Mapokezi ya Dr. Asha Rose Migiro akirejea nchini



Mratibu Mkazi wa Umoja Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou (katikati) akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere kumpokea Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dr. Asha Rose Migiro aliyemaliza muda wake leo wakati akirejea nchini Tanzania. Kushoto ni Afisa wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini Hoyce Temu.

Baadhi ya Mabalozi, Wahadhiri na Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakiwa wamejipanga kumpokea Dr. Asha Rose Migiro.

Msafara wa Dr. Asha Rose Migiro ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Mh. Benard Membe (gari la pili) kuelekea sehemu maalum ya mapokezi.

Dr. Asha Rose Migiro akishuka kwenye gari yake baada ya kukanyaga Ardhi ya Tanzania.
Dr. Asha Rose Migiro akipokelewa kwa shangwe na zawadi za maua kutoka kwa ndugu, jamaa, marafiki na wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje waliofika kumlaki.
Dr. Asha Rose Migiro akisalimiana na baadhi ya mabalozi wapya walioteuliwa na Mh. Rais hivi karibuni. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou.
Dr. Asha Rose Migiro akiendelea kusalimiana na Baadhi ya Mabalozi. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Benard Membe sambamba na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou.
Waziri Membe na Dr. Migiro wakielekea kwenye chumba maalum cha mapumziko kabla ya mkutano na waandishi wa habari.
Dr. Asha Rose Migiro (katikati), akizungumza na waandishi wa habari nchini Tanzania baada ya kumaliza muda wake kama Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambapo pamoja na mambo Mengi amesisitiza kwamba hatojihusisha na siasa kwa sasa. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Benard Membe na Kulia ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou.
Dr. Asha Rose Migiro akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe.
Dr. Asha Rose Migiro (katikati) akiteta jambo Waziri Membe sambamba na Viongozi mbalimbali wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini wakiongozwa na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dr. Alberi Kacou (kushoto) waliofika kumlaki katika Uwanja wa Ndege wa Mwl. J.K Nyerere.
Mbunge wa Singida Mjini Mh. Mohammed Dewji akimpongeza Dr. Asha Rose Migiro kwa kazi nzuri alipokuwa akitumikia kama Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa walipokutana leo katika Uwanja wa ndege.
Pichani Juu na Chini ni wakinamama wakimwimbia Happy Birthday Dr. Asha Rose Migiro ikiwa ni maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa aliporejea nyumbani leo.
Kikundi cha Ngoma kikitoa burudani kwa Dr. Migiro (hayupo pichani)
Dr. Asha Rose Migiro akizungumza Jambo na Dr. Alberic Kacou wakati wakitizama burudani ya ngoma iliyoandaliwa maalum kwa ajili yake. Kushoto ni Waziri Membe.
Dr. Migiro akiwasalimia wasanii wa kikundi cha ngoma.
"Karibu tena Nyumba Mama"... Waziri Membe akiagana na Dr. Asha Rose Migiro baada ya mapokezi.
Dr. Asha Rose Migiro akiagana na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Dr. Alberic Kacou.
Dr. Asha Rose Migiro akiondoka katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere sambamba na ulinzi mkali wakiwemo maafisa wa kimataifa kutoka Ufilipino waliohakikisha ametua nchini Salama.
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) ambaye amemaliza muda wake, Dk. Asha Rose Migiro, amerejea nyumbani leo na kusema kwamba anatarajia kurudi kufundisha katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako alikuwa akifundisha kabla ya kuingia kwenye ulingo wa siasa. Kinyume na matarijio ya watu wengi, Dk. Migiro amesema kuwa kwa sasa hatarajii kujishughulisha katika mambo ya siasa na wala hana mipango ya kugombea urais siku za mbele.
Amesema kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amamteua kuwa Balozi Maalum wa Malaria katika Bara la Afrika na kuongeza kuwa pamoja na kwamba shughuli hizo atakuwa anazifanya kwa muda wake mchache, bado kuna uwezekano mkubwa zikambana na kushindwa kujishughilisha na mambo ya kisiasa.

No comments:

Post a Comment