Thursday, June 21, 2012

Balaa lingine night club za mbele

THE HOUSTON RAPPER "TRAE THA TRUTH" APIGWA RISASI AKIWA NIGHT CLUB.


Katika tukio lingine katika club baada ya lile la Chriss Brown na Drake eti inasemekana walileteana walirushiana chupa club na kupeleka Chriss Brown kuumia kidevu, huko Hoston watu sita walipigwa risasi katika Southwest Strip NightClub na watatu kufa papo hapo kati ya majeruhi alikuwepo rapper kutoka Houston Trae Tha Truth.  Habari kutoka MvFox Houston zinasema wawili kati ya hao waliopigwa risasi walikuwepo wavulana wawili na mwanamke mmoja.

Wednesday, June 20, 2012

John Mnyika atolewa nje ya Bunge


                                                   Hapa Mnyika akitoka nje ya Bunge

Mbunge wa jimbo la Ubungo John Mnyika akitoka nje ya viwanja vya Bunge la Tanzania leo mjini Dodoma baada ya kukataa kufuta kauli ya kumdhalilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa dhaifu. Mbunge huyo alitoa kauli hiyo wakati akichangia Bajeti ya serikali ya mwaka 2012/13 katika mkutano unaoendelea.

                                        Hapa Mnyika akisindikizwa na watu wa Ulinzi Bungeni
   
Kitendo kilichodaiwa kuwa ni udhalilishaji na kashfa kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Monday, June 18, 2012

Dawa za kurefusha maisha (ARV) zatishia kubadilisha muonekano wa Bw.Khamisi Tanga mkazi wa Bagamoyo



Mwanakijiji wa Magomeni wilayani Bagamoyo, Khamisi Tanga mwenye miaka 46 ameota matiti kwa madai ya kutumia dawa za ARV’S zinazotumiwa na watu wenye maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Akizungumza na waandishi wa habari waliokwenda wilayani humo kufanya utafiti kuhusu utekelezaji wa sheria ya ukimwi na Chama cha Waandishi wa Habari za Ukimwi (AJAT), Khamisi alisema alipatwa na mkasa huo miaka mitatu iliyopita.
Akisimulia namna alivyoanza kuugua, alisema awali aliona matiti yake yakiongezeka ukubwa kila kukicha, lakini hakujua kama lingeweza kuja kuwa tatizo kubwa kama lilivyo sasa.
Baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya, ilimbidi kwenda kliniki anayohudhuria kupata dawa na kuwaeleza manesi, ambapo walimjibu kuwa imesababishwa na dawa anazotumia, na hivyo kulazimika kukatizwa dozi hiyo na kupewa aina nyingine. 
Hata hivyo, Khamisi alisema pamoja na kubadilishiwa dozi, hakuna mabadiliko na kuongeza kwamba hivi karibuni alipewa dawa nyingine ambazo kati ya hizo kuna zile zilizomsabishia kukua matiti na tayari ameanza kupata maumivu aliyokuwa akipata awali.
Kwa mujibu wa Khamisi, ameshahangaika kupata matibabu hadi Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili, lakini hadi leo hajapatiwa tiba stahili ya kumaliza tatizo hilo. 
 “Watanzania naomba wanisaidie kwa njia yoyote ile ili niondokane na hali hii, kwani inanidhoofisha sana na kunikosesha raha, hasa mbele ya wanaume wenzangu.
“Hapa ninavyoongea na nyie waandishi, nilipimwa hadi kansa na matiti ndiyo kama hivyo mnavyoyaona, yanaendelea kukua na huniuma sana, hasa wakati ninapolala,” alisema.
Alitumia fursa hiyo kumuomba Rais Jakaya Kikwete kumsaidia ili arudi katika uanamume wake, kwa sababu hivi sasa maisha yake yanazidi kuwa magumu kwa vile hawezi kufanya kazi yoyote. Mtaalamu wa magonjwa, Dk. Dina Komakoma, akielezea sababu za kutokewa kwa hali hiyo kwa wagonjwa wenye maambukizi ya VVU, alisema ni jambo la kawaida japo hutofautiana.
“Wengine hujikuta wakinenepa au wakikonda sana, na hili la Khamis sio mtu wa kwanza kupatwa na hali hiyo,” alisema na kuongeza kwamba inapotokea mgonjwa akapata hali tofauti kama hiyo, anapaswa kusitishiwa dawa...