Mwanakijiji wa Magomeni wilayani Bagamoyo, Khamisi Tanga mwenye miaka 46 ameota
matiti kwa madai ya kutumia dawa za ARV’S zinazotumiwa na watu wenye
maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Akizungumza na waandishi wa habari waliokwenda wilayani humo kufanya
utafiti kuhusu utekelezaji wa sheria ya ukimwi na Chama cha Waandishi wa
Habari za Ukimwi (AJAT), Khamisi alisema alipatwa na mkasa huo miaka
mitatu iliyopita.
Akisimulia namna alivyoanza kuugua, alisema awali aliona matiti yake
yakiongezeka ukubwa kila kukicha, lakini hakujua kama lingeweza kuja
kuwa tatizo kubwa kama lilivyo sasa.
Baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya, ilimbidi kwenda kliniki
anayohudhuria kupata dawa na kuwaeleza manesi, ambapo walimjibu kuwa
imesababishwa na dawa anazotumia, na hivyo kulazimika kukatizwa dozi
hiyo na kupewa aina nyingine.
Hata hivyo, Khamisi alisema pamoja na kubadilishiwa dozi, hakuna
mabadiliko na kuongeza kwamba hivi karibuni alipewa dawa nyingine ambazo
kati ya hizo kuna zile zilizomsabishia kukua matiti na tayari ameanza
kupata maumivu aliyokuwa akipata awali.
Kwa mujibu wa Khamisi, ameshahangaika kupata matibabu hadi Hospitali ya
Rufaa ya Muhimbili, lakini hadi leo hajapatiwa tiba stahili ya kumaliza
tatizo hilo.
“Watanzania naomba wanisaidie kwa njia yoyote ile ili niondokane na
hali hii, kwani inanidhoofisha sana na kunikosesha raha, hasa mbele ya
wanaume wenzangu.
“Hapa ninavyoongea na nyie waandishi, nilipimwa hadi kansa na matiti
ndiyo kama hivyo mnavyoyaona, yanaendelea kukua na huniuma sana, hasa
wakati ninapolala,” alisema.
Alitumia fursa hiyo kumuomba Rais Jakaya Kikwete kumsaidia ili arudi
katika uanamume wake, kwa sababu hivi sasa maisha yake yanazidi kuwa
magumu kwa vile hawezi kufanya kazi yoyote. Mtaalamu wa magonjwa, Dk.
Dina Komakoma, akielezea sababu za kutokewa kwa hali hiyo kwa wagonjwa
wenye maambukizi ya VVU, alisema ni jambo la kawaida japo hutofautiana.
“Wengine hujikuta wakinenepa au wakikonda sana, na hili la Khamis sio
mtu wa kwanza kupatwa na hali hiyo,” alisema na kuongeza kwamba
inapotokea mgonjwa akapata hali tofauti kama hiyo, anapaswa kusitishiwa
dawa...
No comments:
Post a Comment