Wednesday, September 12, 2012

Mchungaji Mtanzania aliyemuoa mwanaume mwenzake huyu hapa

MCHUNGAJI wa Kanisa la Glory of God Miracle Center, Peter Rashid Aboubakar (pichani), ametupiwa skendo kisha yeye mwenyewe akakiri kuoa mwanaume mwenzake.
Peter ambaye mwenyewe hupenda aitwe mtume, ameshuhudia mbele ya Uwazi kwamba ni kweli alioa mwanaume lakini ni zama ambazo alikuwa hajaokoka wala kupata upako wa kuongoza kanisa.
Awali, Uwazi lilipokea taarifa kutoka kwa vyanzo vyake kwamba Peter na utumishi wa Mungu wapi na wapi, kwa maana ana rekodi za uchafu, ikiwemo kuishi kinyumba na mwanaume mwenzake.
Chanzo chetu kilidai kuwa Peter alimuoa mwanaume mwenzake anayeitwa Abdallah Athuman na waliishi wote Ilala, Dar es Salaam.

DIAMOND: NILISHAWAHI MKUTA WEMA AKIWA UCHI NA MTU MWINGINE HOTELINI.

Baada ya kuamua kutokaa kimya kutokana na shutuma zilizotolewa dhidi yake na mpenzi wake wa zamani WEMA SEPETU, Mwimbaji DIAMOND PLATNUMS ameamua kutoa kauli yake ya mwisho kuhusu Wema.
Diamond anakiri kwamba hakutaka kabisa kumzungumzia Wema kwenye vyombo vya habari baada ya kuachana kwa sababu hakutaka malumbano lakini imebidi iwe hivyo kwa sababu ya hasira aliyoipata kutokana na Wema kuzungumza uongo mwingi dhidi yake.
Exclusive na millardayo.com Diamond amekiri kwamba aliachana rasmi na Wema mwezi january mwaka huu na hiyo ni kutokana na kukerwa na tabia za Wema alizozikemea lakini mwisho wa siku hakufanikiwa, zikawa zinaendelea…. ambapo tabia hizo ni pamoja na Wema kuwalipa waandishi wa habari wa magazeti ili watoe stori zake, japo Diamond alikua anawalipa waandishi wasiandike chochote, yeye alikua anawalipa zaidi.

Chris Brown atupia tatoo yenye sura ya Rihanna

Msanii anayefanya vizuri sana katika game la muziki wa R&B kutoka  pande za state.Huyu si mwingine anafahamika kwa jina la Chris brown.Msanii huyu siku za hivi karibuni alionekana amepiga new tatoo katika shigo yake.tatoo hiyo ilizua sana maneno kutoka kwa watu kwamba ni sura ya msanii ambaye anafanya game la muziki American anafahamika kwa jina la Rihanna.
 Hii ndiyo tatoo mpya ya chris brown ambayo inasemekana kwamba ni sura ya Rihanna.

Kweli hizi ni nyakati za mwisho

HUYU NDIO MTOTO ALIEMUOA MAMA YAKE


Monday, September 10, 2012

Kweli ng'ombe hazeeki maini, babu miaka 70 afumaniwa

Habari kutoka arusha, Chanzo chetu cha habari kuripoti juu ya fumanizi la babu mwenye umri wa miaka 70, Rafael Mitasio aliyenaswa gesti akiwa na mke wa mpangaji wake, taarifa tulizozinasa zinadai kuwa mzee huyo amesusiwa mwanamke huyo.
Chanzo chetu cha habari kimedai kuwa, mara baada ya habari hiyo kutoka gazetini, mume wa mwanamke huyo aliyefahamika kwa jina la baba Tausi aliumia sana hivyo akampa kisogo kitendo kilichomfanya mgoni huyo atangaze kumuoa.
“Ile habari ilipotoka kwa kweli mume wa yule mwanamke aliumia sana, akaamua heri huyo mzee amchukue kabisa kama ameona anaweza kumtunza kuliko yeye.

Aina mbalimbali za watu wanaoweza kukukatisha tamaa

KWA sehemu kubwa, maisha ya mwanadamu yanategemea sana ushirikiano wa watu wenzake. Watalaamu wanasema mafanikio na kutofanikiwa ni watu.
Huwezi kusema umefanikiwa kisiwani kusikokuwa na watu ambao watakuwa sehemu ya mafanikio yako. Mtu yeyote hataonekana ameendelea kwa kuwa na viwanda vingi msituni wanakoishi wanyama wasiofahamu umuhimu wa nyama ya kusindika.
Aidha, kipimo cha kutofanikiwa hakitokani na maisha ya upweke bali ya kujilinganisha na watu wengine wanaozunguka maisha yako ya kila siku. Tajiri wa kijijini ni yule anayemiliki Bajaj ambazo wengine kwenye eneo analoishi hawana.
Ni ukweli ulio wazi kwamba utajiri wa mtu wa shamba wanakoishi maskini wengi hauwezi kuwanyima usingizi matajiri wa mjini wanaotembelea magari na kuishi kwenye nyumba za kifahari. Maana yangu hapa ni kwamba maisha ni watu.
Siku zote kwenye maisha yangu ninapokutana na binadamu wenzangu huwafikiria katika sehemu mbili. Kwanza kukwama kokote katika maisha kutatokana nao, lakini pili, ni  kufanikiwa kwangu sehemu ya ninachokitarajia kutoka kwao.

Orodha ya majina ya wasanii walioingia 20 bora ya kutengeneza mkwanja mrefu Marekani


 

GWIJI wa Hip Hop ambaye pia ni Mtayarishaji wa muziki na Mjasiriamali nchini Marekani, Andre Romelle Young maarufu kwa jina la Dr. Dre ndiye msanii wa Hip Hop anayetengeneza fedha nyingi  kwa sasa. Kwa mujibu wa mtandao wa Forbes, Dr. Dre anaongoza akiwa ametengeneza kiasi cha dola milioni 110 zaidi ya shilingi bilioni 173 za Kitanzania kwa mwaka 2012. Anayemfuatia ni mwanmuziki Sean John Combs maarufu kama  P. Diddy anayetengeneza kiasi cha dola milioni 45 zaidi ya shilingi bilioni 70 za Kitanzania. Wa tatu ni msanii Shawn Corey Carter maarufu kama Jay-Z anayejiingizia kiasi cha dola milioni 38 sawa na shilingi bilioni 59.9 za Kitanzania.