Miongoni mwa vitu vinavyochangia kuharibu uhusiano wa kimapenzi ni
hisia. Wapenzi wengi wameachana kwa sababu si kwamba walithibitisha
ubaya wa wenzao ila walijijaza wenyewe hisia mbaya na kujikuta
wamepoteza thamani ya kupenda. Hebu angalia hisia nane hatari ili
uzikimbie mapema kabla hazijakuharibia penzi lako.
1. NASALITIWA
Kuishi
katika mapenzi huku ukiwa na fikra kwamba mwenza wako anakusaliti ni
jambo baya kwa vile huathiri msukumo wa ndani wa kupenda. Matokeo yake
utajikuta ukishindwa kutimiza wajibu wako kama mke/mume kwa sababu tu ya
kuendekeza hisia mbaya. Acha kuhisi, tafuta ukweli.
2. TUTAACHANA
Kuna
wapenzi ambao wanaishi na mawazo ya “ipo siku tutaachana”. Wanafanya
hivyo eti kwa kutafsiri mwenendo usioridhisha wa mapenzi yao. Kusema
kweli hili ni jambo baya kwani huondoa ari na kujenga ufa wa mapenzi.
Huwafanya wapenzi kubakia na wazo moja tu, la kutafuta sehemu mbadala ya
kwenda baada ya kuachana. Usiwaze kabisa kuachana hata kama mnagombana
na mwenzako kila siku.
3. SIWEZI MAPENZI
Baadhi ya wapenzi
huwa na hisia kwamba hawayawezi mapenzi. Hata kama hawajaambiwa chochote
kuhusu kutowatosheleza wenza wao faragha hukimbilia kujihukumu.
Hujaambiwa kama umecheza chini ya kiwango, hofu ya nini? Usiwaze hivyo,
kama una lolote linalokufanya uwe na hofu muulize mwenzio.
4. NINA KASORO
Naamini
mitaani wapo watu ambao huamini wana kasoro fulani ndiyo maana
hawafikii viwango vya kupendwa kama wanavyovihitaji. “Yaani mimi
ningekuwa kama fulani ningefurahi sana lakini ufupi wangu ndiyo tatizo.”
Hizi ni hisia mbaya tu, kumbuka kuna wafupi wanapendwa ile mbaya.
Jisahihishe na epuka kujishusha hadhi kwenye hisia zako.
5. NITAMUUA
Miongoni
mwa hisia mbaya kabisa kwenye mapenzi ni kufikiria kumuua mwenzako kwa
sababu yoyote. “Nikimfumania na mwanaume mwingine nitamuua.” Mtu
anayetawaliwa na mawazo ya aina hii anajiweka katika mtego mbaya
kisaikolojia wa kuja kutekeleza kile anachojiapiza hata kwa sababu
ndogo. Usifikirie hivyo maishani mwako.
6. NIMEKOSEA KUCHAGUA
Usijihukumu
makosa kwa sababu umeona mpenzi wako ana tatizo fulani. Fahamu kuwa
kasoro ni sehemu ya ubinadamu. Weka mikakati ya kumuongoza mwezio kuliko
kuhitimisha kwa mawazo kwamba ulikosea kumchagua. “Ningejua kama yuko
hivi nisingemchagua.” Usiwaze hivi!
7. HATUWEZI KUZAA
Kuna
wapenzi ambao kwa kuishi miaka mitatu au minne pamoja bila kupata mtoto
hufikia kwenye fikra kwamba hawawezi kuzaa. “Mmm, mwaka wa nne umepita
bila mtoto, nadhani sisi hatuwezi kuzaa.” Kwa nini msizae?Hizo ni fikra
zako, hamjaambiwa na daktari sasa iweje uwaze hivyo? Jipe moyo kwani
kuna watu walizaa baada ya miaka kumi, iweje ninyi wa mwaka mmoja?
8. UNANIDANGANYA
Ipo
aina ya watu ambao hata kama wakiambiwa wanapendwa sana, hukimbilia
kusema na kuamini kuwa wanadanganywa. “Mmm unanidanganya.” Atasema hivyo
licha ya kuona mwanaume anavyojituma kumsotea na kumuonesha kila dalili
za mapenzi. Hili ni jambo baya, ukithibitisha kwamba unapendwa usihisi
unadanganywa, utapoteza bahati yako.
No comments:
Post a Comment