Saturday, July 21, 2012

Madada POA watangaza ofa kabla ya mwezi mtukufu kuanza

KATIKA hali ya kushangaza, usiku wa Jumanne iliyopita, chanzo chetu kiliwanasa akina dada wanaojiuza ‘machangudoa’ ambao walisema hawatakuwepo katika eneo la biashara kwa muda wa mwezi mmoja kwa sababu ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Wakati wewe ukikosa hata nauli ya mjini Mtanzania mwenzio anafanya kufuru kama hili

 Davies Mosha
“HII sasa ni kufuru!” Hivi ndivyo utakavyoweza kusema kwa Davies Mosha ambaye ni makamu mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Yanga, ambaye nafasi yake kwa sasa klabuni hapo inashikiliwa na Clement Sanga.
Kwa tafsiri ya haraka, yawezekana Mosha anaweza kuwa ndiye kiongozi pekee wa soka nchini kumiliki gari la kifahari na lenye gharama kubwa aina ya Lamborghini kama ambalo linamilikiwa na mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney.

14 wauawa katika shambulizi Marekani


Ukumbi wa Sinema mjini Denver

Rais Barack Obama na mkewe Michele wameelezea masikitiko yao kufuatia mauawaji ya watu kumi na wanne mjini denver huko colorado.
Obama alisema kuwa serikali itafanya kila juhudi kuwasaidia watu wa eneo la tukio, la Aurora wakati huu mgumu.
Alikiri kuwa serikali itakahakikisha aliyehusika anakamatwa.
Mtu mmoja aliyekuwa amefunika uso wake kwa barakoa aliwauwa kwa kuwapiga risasi watu hao kumi na wanne na kuwajeruhi takriban hamsini wakati wa onyesho la filamu ya Batman,The Dark Knight Rises.

MKURUGENZI MTENDAJI WA NBC, LAWRENCE MAFURU ASIMAMISHWA KAZI KUCHUNGUZWA

Mr. Lawrence Mafuru,  Managing Director of National Bank of Commerce (NBC).

Dotnata Amuacha mumewe na kubadili dini

 MSANII mkongwe katika tasnia ya filamu za Kibongo, Husna Posh ‘Dotnata’ amebadili dini kutoka Uislam na kuwa Mkristo kwa kile alichodai ni kutengeneza maisha yake baada ya kuhangaika na mambo ya dunia kwa muda mrefu.
Akichezesha taya na chanzo chetu, Dotnata alisema amefikia uamuzi huo baada ya kuugua na kuhangaika kwa waganga wengi kwa muda mrefu bila ya mafanikio.
Dotnata ametaja sababu nyingine ni mama yake mzazi ambaye alifikia hatua ya kususa kumtembelea nyumbani kwake hasa kipindi cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani akimtaka aokoke.
“Mama alinipa masharti kwamba nitakapookoka ndipo atakapofika kwangu jambo ambalo lilikuwa linaninyima amani na kunifanya nichukue uamuzi huo,” alisema.
Dotnata ambaye awali alikuwa ni Mkristo amebatizwa upya na anatumia jina lake la awali kabla ya kuwa Muislam la Iluminata na amejiunga na Kanisa la Ufufuo na Uzima (kwa Gwajima) lililopo Kawe jijini Dar.

Friday, July 20, 2012

Jokate na Wema wakataa kata wa kata kusuluhishwa

KUTOELEWANA kati ya ma-Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu (No. 1) na Jokate Mwegelo (No.2) (pichani) kumeendelea kushika kasi na sasa bifu lao lina kila dalili ya kwenda hadi mwisho wa maisha yao, chanzo chetu lina shuka na ushahidi wa kutosha.
Awali bifu la wawili hao lilidaiwa kuwa chanzo chake kilitokana na Jokate kuunga uhusiano wa kimapenzi na msanii nyota wa Bongo Fleva, Abdul Nasibu ‘Diamond’ huku akijua wazi ana uchumba na Wema.
Uadui ulianzia hapo, Wema akalia sana kupitia vyombo vya habari, lakini mara zote Jokate amekuwa akikanusha kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Diamond licha ya kwamba ushahidi wa kimazingira umekuwa ukikidhi kwamba wawili hao wanatoka pamoja.
Kufuatia hali hiyo, Wema na Jokate wakawa maadui wakubwa huku jamii ikiwatazama kwa macho ya chongo kuhusu uhusiano wao kuharibiwa na kitu mapenzi.

JINSI YA KUMTAMBUA MWANAMKE ANAYEKARIBIA KUKUACHA!


 Kuna tofauti kubwa ya kimaamuzi kati ya mwanaume na mwanamke kwenye suala la kuachana. Inaelezwa kwamba, wanaume ni rahisi kwao kuamua ndani ya dakika moja na kutangaza kuvunja uhusiano, lakini kwa wanawake maamuzi yao mara nyingi hutanguliwa na dalili, ingawa hata wanaume nao wanazo.

Uchunguzi unaonesha kuwa, wanawake wengi hawawezi kuficha sana hisia zao za mapenzi, lakini pia kwenye chuki hawakujaaliwa uvumilivu. Wanasaikolojia wanakiri kwamba, kutambua mawazo yaliyomo ndani ya mwanamke kwa kumtazama muonekano wake usoni ni rahisi kuliko mwanaume ambaye anatajwa kuwa na uwezo kuficha mawazo yake.

Muongozo huo wa kitaalamu wa kumtambua mwanamke anayekaribia kukuacha ni kazi rahisi, ambayo inaweza kuanzia kwenye kona ya mazoea ya tabia zake za kila siku kwenye uhusiano wa kimapenzi. Ni imani yangu kuwa kila mwanaume anamfahamu mpenzi wake katika sura mbili za chuki na furaha yake.

Atakuwa mwanaume wa ajabu ambaye atarudi nyumbani kwake na kushindwa kusoma sura ya mkewe na kujua kama ana furaha au amekwazika.
Ninapotazama uwezekano rahisi wa kumtambua mwanamke, nafika mahali pa kuamini kuwa dokezo chache nitakazotoa hapa chini zinaweza kuwa msaada kwa wanaume wengi kujua kama wamekaribia kuwekwa kando kimapenzi.

MWANAFUNZI WA IFM AFARIKI KIFO CHA KUTATANISHA: AOKOTWA MAENEO YA KOKO BEACH AKIWA HAJITAMBUI.

Marehemu Agnes B. King'unza wakati wa uhai wake.

Agnes alikuwa ni mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) akiwa mwaka wa kwanza akichukua Shahada ya Kodi (Bachelor of Taxation).
 
Agnes aliokotwa na msamaria mmoja ambaye kwa taarifa za awali zinasema alikuwa ni mlinzi wa nyumba moja maeneo ya Koko Beach ambako ndio alikutwa ametupwa na watu wasiofahamika na kupelekwa kituo cha Polisi cha Oysterbay na baadae kukimbizwa hospitali ya Agha khan.

Thursday, July 19, 2012

Nafasi za Kazi 30 Leo Tarehe 18 July

Nursing Officer/Midwife
Elite Career Choices
Deadline: Jul 27, 2012

Deputy Director of Disability Hospital
Elite Career Choices
Deadline: Jul 27, 2012

Physiotherapist
Elite Career Choices
Deadline: Jul 27, 2012

Occupational Therapist
Elite Career Choices
Deadline: Jul 27, 2012

Anesthesiologist
Elite Career Choices
Deadline: Jul 27, 2012

Advocacy Manager – Child Rights
Save the Children
Deadline: Jul 25, 2012

Regional Accountant
SMEC
Deadline: Jul 27, 2012

Habari picha mwanzo mwisho wa uokoaji wa wahanga wa ajali ya

Mwokoaji akiwa na mmoja wa maiti wa ajali hiyo
 Waokoaji wakiokoa moja ya maiti. wakiwa katika boti ya Kilimanjaro. 

MBINU 13 ZA KUYAVUKA MAISHA YA HUZUNI


TUANZE kwa kutafakari baadhi ya taarifa za kuhuzunisha, ambazo wengi wetu tunakutana nazo kila siku katika maisha yetu. “Kuanzia leo umefukuzwa kazi”, “Nimeamua tuachane”, “Baba yako mzazi amefariki leo asubuhi”,  “Mwanao amefariki.” Bila shaka taarifa za aina hii zinahuzunisha na swali linabaki tufanyeje tunapokuwa na mawazo ya aina hii?
Ukweli ni kwamba, yakitokea mawazo mabaya katikati ya furaha huwezi kuiondoa, lakini pamoja na hayo baadhi ya watu hutumia muda mwingi sana kuhuzunishwa na tatizo ambalo pengine lingeweza kumalizwa kwa saa chache na mhusika kubaki huru.
      Wapo watu kati yetu wanaweza kufuga mawazo ya kuachwa na wapenzi wao kwa miaka mitano mfululizo, huku wengine wakitumia miezi mingi kuondokana na huzuni iliyotokana na kutukanwa na wazazi, kufokewa na bosi, kupata hasara katika biashara,   kufeli mitihani na kadhalika.

Usiombe ufumaniwe hautapita tena mbele ya watu

USIOMBE yakukute! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya kusikia kisa cha aliyewahi kuwa mpenzi wa mwanamuziki wa TAKEU, Nice Lucas Mkenda ‘Mr. Nice’, Lulu John (mwenye blauzi nyekundu) anayedai kumfumania mumewe (siyo Mr. Nice),chanzo chetu kinafunguka.
Lulu alidai kumfumania bwana’ke Abdulatif Salum na mwanamke ambaye jina halikupatika kwenye gesti moja iliyopo Kinondoni B jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki iliyopita.
SINEMA ILIKUWA HIVI

JUSTINE BIEBER AFURAHIA UMRI WA MAMA YAKE


Justin Bieber amesema kuwa karibu mno na mama yake kiumri, ambaye alimzaa akiwa na miaka 18, kumewafanya wawe marafiki.
Akizungumza na 2Day FM, Justin amesema: "She's amazing'... Ni wazi nilikuwa kama ajali kwake, ni poa sana mama yangu bado ni mdogo, ni rafiki na mama yangu pia, amekuwa strict sana siku zote, ameniweka kwenye mstari.”
Katika mahojiano hayo Justin alizungumzia pia jinsi ambavyo huwa haoni shida kuperform mbele ya maelfu ya watu lakini hupata shida kubwa anapotaka kuongea mbele yao.
Alieleza:"Napenda kuperform, kupiga tour na kuwa na umati mpya wa watu kila usiku, ni kitu nikipendacho siku zote.. Ni ajabu kuwa naweza kuperform mbele ya watu wengi lakini ukifika wakati wa kuongea napata shida, sijui kabisa jinsi ya kuzungumza mbele ya watu wengi."
Aidha Justin alizungumzia pia mipango ya kufanya filamu ambapo amesema ameanza mazunguzo na muigizaji Mark Wahlberg kufanya filamu mpya.


Wednesday, July 18, 2012

Balotelli Earns £120,000 A Week While His Mum Works As A Cleaner

He earns £120,000 a week, likes to drink vintage champagne straight from the bottle and once famously put hundreds of pounds on to a church collection plate.

But Mario Balotelli's generosity doesn't appear to extend to his mother, who works as a cleaner in an office only a few miles from her son's £3million mansion.

While the Manchester City footballer glides around in his gleaming £120,000Bentley Continental GT, Rose Barwuah has a more humble mode of transport – the number 11 bus.

Five times a week, she catches the bus  to start her job as a cleaner at a car lease  firm on the outskirts of Cheadle, near  Manchester, earning little more than the minimum wage of £6.08  an hour.

US Approves First HIV Prevention Pill

The first-ever daily pill to help prevent against HIV was approved Monday by US regulators for use in uninfected adults who are at risk for getting the virus that causes AIDS.

The pill as pre-exposure prophylaxis (PrEP) has been hailed by some AIDS experts as a potent new tool against human immunodeficiency virus, but somehealth care providers are concerned it could encourage risky sex behavior.

In addition, the regimen is estimated to cost around $14,000 per year, making it out of reach of many.

“Truvada alone should not be used to prevent HIV infection,” said Debra Birnkrant, director of the division of antiviral products at the FDA.

Tuesday, July 17, 2012

Wanaume nao Kutumia Sindano za Kupangilia Uzazi

 Baada ya wanawake kwa miaka mingi kuwa ndio wenye jukumu la kutumia vidonge na njia nyingine katika kupangilia uzazi, watafiti nchini China wamekamilisha utafiti wao ambao utawasaidia wanaume kuwasaidia wanawake jukumu hilo baada ya kutoa sindano kwaajili ya wanaume zitakazosimamisha uzalishaji wa mbegu za kiume kwa muda Wanasayansi nchini China wamekamilisha utafiti wao wa sindano kwaajili ya wanaume ili kusaidia kuzuia mimba zisizohitajika.
Sindano hizo zinasimamisha kwa muda uzalishaji wa mbegu za kiume na watafiti hao walisema kwamba uzalishaji wa mbegu za kiume unaweza ukaendelezwa muda wowote ule.

NDOA YA HEMED YAKWAMA, KISA ELIMU NDOGO

NDOTO kufunga pingu za  maisha  siku za  karibuni alizokuwanazo nyota  kutoka 'Bongo moive' Hemed Suleiman 'PHD', zimeota mbawa kufuatia  wazazi wa mlimbwende aliyetaka kumuoa kuweka ngumu.
katika mahojino ya dakika kadhaa aliyofanya  na  chanzo chetu, Hemed amesema kuwa tayari alikuwa ameanza taratibu za kushughulikia ndoa yake na mrembo huyo iliyopangwa kufungwa  kimya kimya  kwa kuogopa watu wenye nia mbaya   lakini amejikuta akilazimika kustisha harakati hizo kufuatia wazazi wa binti huyo wakaweka ngumu kwa madai kuwa wanataka mtoto wao amalize kwanza  masomo yake  na kupata 'mastaz' kwa kuwa  elimu ya  Degree aliyonayo hivi sasa wanahisi bado haijamtosha.
 "unajua mchumba  wangu hivi sasa ana elimu ya degree hivyo wazazi wamesema kwao hiyo bado ni elimu ndogo hivyo hawezi kuruhusu jambo hilo kwanza  mpaka apate 'mastaz' halafu ndiyo mambo mengine yatafuata, imeniuma sana kwa kuwa wenyewe tulishakubaliana na mwenzangu alikuwa tayari kwa hilo" alisema  Hemed.

STAA BONGO MOVE APIGWA STOP KUIGIZA


Nyota  kutoka tasnia ya  filamu Bongo Skyner Ally huenda asionekane tena kwenye ulimwengu wa move kufuatia kupigwa  stop kushiriki katika  kuigiza.
Stori  'under carpet' ambazo chanzo chetu imezinyaka kutoka kwa mmoja wa wapambe wa mwigizaji huyo aliyeng'arisha nyota yake kupitia filamu ya  'SECOND WIFE' iliyopikwa na mkali Ray Kigosi, zinasomeka kuwa  Skyner amepigwa stop na  wazazi wa  upande pili  (wakwe) ili aweze kulea vizuri mtoto wake badala ya kutumia muda mwingi akiwa kambini na waigizaji wengine kwa ajiri ya kurekodi 'muvi'.

ALBAM YA WEUSI YAKWAMA


Staa wa hip hop kutoka 'Kruu' ya Weusi iliyokita kambi  pande za A-Town, Nikki wa Pilli amesema kuwa albam ya kundi hilo iliyokuwa itoke mapema mwezi uliopia imekwama.

Usijipe presha, kama unampenda muamini kisha ziba masikio!

Assalam alaikum mpenzi msomaji wangu wa safu hii. Mambo vipi? Natumani kwamba muwazima kabisa na mnaendelea vyema na majukumu yenu ya kila siku. Mimi namshukuru Mungu kwani amekuwa akinipa nguvu ya kuandika haya ninayoamini yana manufaa kwenu.
Ndugu zangu, ili uweze kudumu katika uhusiano wako unatakiwa kujenga mazingira ya kumuamini sana mpenzi wako. Nasema hivyo kwa kuwa, mapenzi ni imani. Ni sawa na kuamini Mungu yupo licha ya kwamba hujawahi kumuona.
Vivyo hivyo, amini tu kwamba mpenzi wako anakupenda kwa dhati licha ya kwamba hujaufungua moyo wake na kathibitisha kwamba ndani yake uko wewe peke yako.
Mpende, muamini na weka akilini mwako kwamba, kamwe hawezi kukusaliti licha ya kwamba kinyume chake pia ni sawa. Hiyo itakusaidia wewe kuendelea kuishi maisha ya furaha na amani bila kuwa na presha.
Jiulize, ni wanaume wangapi ambao wake zao wanagawa penzi nje ya ndoa lakini wao wanawaamini kupita maelezo? Ni wanawake wangapi ambao waume zao ni viwembe kwelikweli lakini wanawaamini kupindukia? Unadhani ni kwa nini? Ni kwa sababu wamejijengea mazingira ya kuwaamini wenzao wao wa kiwango kikubwa na kuziba masikio yao kukwepa wambeya.

Shilole chupuchupu kuvuliwa nguo barabarani

 Zuwena Mohamed ‘Shilole’.


MSANII wa filamu na muziki wa Pwani, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ameponea chupuchupu kuvuliwa nguo barabarani maeneo ya Darajani mjini zanzibar baada ya kukatiza mitaa ya sokoni akiwa katupia kigauni kifupi ajabu.

Ikithibitika tu! Baba ba mama Lulu matatani

Yasemekana endapo Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam Julai 23, mwaka huu itamaliza utata wa umri wa Elizabeth Michael ‘Lulu’ na kuthibitisha umri aliokuwa nao wakati anapata mkasa wa kifo cha Steven Kanumba, kuna uwezekano wazazi wake, mzee Michael Kimemeta na Lucresia Karugila wakaingia matatani.
Kwa mujibu wa mtaalam wa sheria (jina linahifadhiwa), bila kuingilia uhuru wa mahakama alisema kuwa kuna vipengele vya sheria vinaweza kuwabana kwa kigezo cha malezi ya mtoto.
“Kwa mfano The Law Of The Child Act ya 2009, inaainisha kuwa mzazi anatakiwa kusimamia malezi ya mtoto kwa kumpatia mahitaji muhimu kama chakula, malazi, matibabu na mengineyo na ikithibitika yanakiukwa, hatua ya kwanza kisheria yawezekana mzazi akapokonywa mtoto na kulelewa chini ya mahakama,” alisema na kuongeza:

MTOTO WA KAMBO WA USHER RAYMOND KUTOLEWA KWENYE LIFE SUPPORT MASHINE MWANZONI WA MWEZI WA NANE


wiki moja baada ya mtoto wa kambo wa Usher Raymond  Kyle Glover kutangazwa kuwa ubongo wake umekufa baada ya ajali ya jet ski katika ziwa Lanier Atlanta, inasemekana kuwa ex-wife wa Usher Tameka Foster atalazimika kumtoa mtoto huyo mwenye miaka 11 kwenye life support mashine mapema mwezi wa nane.
habari zinasema kuwa kampuni ya insurance ya Tameka inategemea kutoa deadline ya kuendelea kulipa billi kubwa kutoka katika hospitali hiyo na kuweka wazi kuwa ni miezi kadhaa ijayo. mama wa mtoto Tameka amesema anaamini miujiza itatokea na mtoto huyo atarudi tena duniani ....

BEYONCE NA SOLANGE KNOWLES WAGOMBANA KISA URAFIKI NA KIM KARDASHIAN





The Keeping Up With The Kardashiansreality star ameingia kaatika urafiki na Grammy award-winning singer baada ya kuwa na uhusiano na rafiki wa karibu wa Beyonce, Kanye West. Beyoce na Kim wameonekana pamoja katika 'Watch The Throne' tour ya Kanye na Jay-Z na katika tuzo zilizopita hivi karibuni za BET, huku ikisemekana kuwa Kim pia anazidi kujiweka karibu na mtoto wa Beyonce mwenye miezi sita sasa, Blue Ivy.

*BREAKING NEWS*

Msanii CHEGE apata ajali mbaya ya gari usiku huu Temeke Dar es salaam, ameumia ila gari halifai kabisa. Chanzo ni mtu wa pikipiki......
Tutaendelea kuwajuza kadri tutakavyoendelea kupokea habari, Tumuombeeni kwa Mungu asiwe ameumia sana

Monday, July 16, 2012

Ajali Mbaya imetokea Mbeya mmoja afariki Hapo hapo na Majeruhi 7

Lori lakubeba kifusi cha mawe aina ya Skania Namba T 525ACP  Mali ya Bhanji , lililo katika breki na kushindwa kusimama katika Mteremko wa Nzovwe na kuenda kugonga Gari aina ya Prado ambapo Dereva wa Gari hilo dogo alifariki hapo hapo.

LAMAR AKANUSHA KUTOA RUSHWA


Produza na mmilikiwa studio maarufu ya muziki Bongo, Fishcrub, Lamar Niekamp amekanusha tetesi za kutoa rushwa kwa baadhi ya watangazaji na ma-Dj wa vituo vya redio nchini kwa lengo la kupewa chapuo kwa nyimbo zilizopita kwenye mikono yake.

Sunday, July 15, 2012

Moyo wa huruma huwa chanzo cha usaliti katika Mapenzi

 
TUMEKUTANA tena kujuzana machache kuhusu maisha yetu ya kila siku. Sasa hivi kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja, limekuwa jambo la kawaida, ndoa zimeingia katika migogoro mingi, nyingine kutokana na mdudu huyu ‘kukosa uaminifu’.
Kona hii kama kawaida imefanya uchunguzi wa kina na kugundua sababu kubwa ya uhusiano mwingi kuwa na migogoro ni kukosa uaminifu. Nitamzungumzia mwanamke ambaye ndiye aliye kwenye hatari kubwa katika mapenzi.
Moyo wa huruma umekuwa tatizo kwa wanawake wengi ambao wamo ndani ya uhusiano unaowafanya wajidhalilishe kwa huruma yao.