Tuesday, July 17, 2012

Shilole chupuchupu kuvuliwa nguo barabarani

 Zuwena Mohamed ‘Shilole’.


MSANII wa filamu na muziki wa Pwani, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ameponea chupuchupu kuvuliwa nguo barabarani maeneo ya Darajani mjini zanzibar baada ya kukatiza mitaa ya sokoni akiwa katupia kigauni kifupi ajabu.

Bongowood ilimshuhudia Shilole akiwa na wanenguaji wake akipigiwa kelele na wanaume waliotaka kumkamata wamvue kisha wamlambe viboko hivyo akalazimika kukimbilia dukani akanunua dela na kulivaa juu ya kigauni cha kihasara alichokuwa amekitinga.

1 comment:

  1. Heko wanaume wa Zenji maana huo mtindo wa kuvaa nguo fupi umezidi kwa akina dada mastar. hili liwe fundisho kwa akina dada kama huyu

    ReplyDelete