Davies
Mosha
“HII sasa ni kufuru!” Hivi ndivyo utakavyoweza kusema kwa Davies
Mosha ambaye ni makamu mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Yanga, ambaye
nafasi yake kwa sasa klabuni hapo inashikiliwa na Clement Sanga.
Kwa tafsiri ya haraka, yawezekana Mosha anaweza kuwa ndiye kiongozi pekee wa soka nchini kumiliki gari la kifahari na lenye gharama kubwa aina ya Lamborghini kama ambalo linamilikiwa na mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney.

Gari
analomiliki Mosha ambalo lina rangi ya njano, linaaminika kuwa miongoni
mwa magari yenye thamani kubwa siyo tu Tanzania na Afrika, bali duniani
kote, kwani hata siku Rooney alipolinunua wenzake wengi hawakutegemea,
siyo kwa sababu hana fedha, ila kwa kuwa hakuwa mtu wa matumizi ya
magari yenye thamani kubwa kama hilo.
Mosha ameliambia Championi Ijumaa kuwa anamiliki magari kadhaa ya kifahari kwa matumizi yake binafsi na familia yake.
Mosha ameliambia Championi Ijumaa kuwa anamiliki magari kadhaa ya kifahari kwa matumizi yake binafsi na familia yake.
Yafuatayo
ni maelezo kuhusiana na gari hilo la kifahari kwa kuanzia kiwango cha
mafuta na usumbufu anaoupata akiwa katika mizunguko yake.
Ameinunua kwa bei gani?
“Kutokana na ubora wa gari hili, nililazimika kutoa shilingi bilioni
moja kwa ajili ya kulinunua, kama unavyojua ni fedha nyingi, nimenunua
kwa mapenzi yangu.
Alipolinunua
“Hili gari kaniuzia mtoto wa Bakhresa (Yusuph), baada ya kufikia makubaliano kati yake na mimi, aliniuzia Julai 2011.
Spidi ya gari
“Hili gari kasi yake ya mwisho ni 360, ni kasi kali na inatosha kwa matumizi yangu binafsi.
Matumizi ya mafuta
“Matumizi ni ya kawaida wala siyo ya kuogopesha sana, inategemea na umbali utakaotembea.
Usumbufu anaoupata
“Usumbufu mkubwa ninaoupata kiukweli, nikiwa naendesha barabarani,
madereva wengine wanalishangaa sana, hali inayosababisha kutokea ajali
au msuguano mara kadhaa.
“Hivi karibuni dereva mmoja aliigonga sehemu ya tairi la nyuma kushoto kutokana na kuishangaa, ilikuwa maeneo ya Masaki hapahapa Dar es Salaam.
“Hivi karibuni dereva mmoja aliigonga sehemu ya tairi la nyuma kushoto kutokana na kuishangaa, ilikuwa maeneo ya Masaki hapahapa Dar es Salaam.
“Matengenezo
yake yaligharimu pauni 20,000 (zaidi ya shilingi milioni 50), hali
iliyosababisha niwe makini nikiwa naendesha,” anasema Mosha.
No comments:
Post a Comment