Tuesday, January 8, 2013

KANISA LA AJABU LINALOPINGA BIBLIA TAKATIFU LATUA TANZANIA

Kanisa hilo ambalo linajulikana kwa jina la The Pool of Siloam lililoko Mbezi- Makonde, Kinondoni, Dar es Salaam linafanya ibada zake Jumanne badala ya Jumapili wakiamini ndivyo Neno la Mungu linavyotaka.

Jambo lingine ambalo linachagiza u-ajabu wa kanisa hio…

KANISA lingine la ajabu limegunduliwa Bongo ambapo linafanya ibada zake kwa utofauti mkubwa na makanisa yaliyozoeleka na wengi, Uwazi limechimbua.
                        

Kanisa la The Pool of Siloam lililoko Mbezi- Makonde, Kinondoni, Dar es Salaam.
Kanisa hilo ambalo linajulikana kwa jina la The Pool of Siloam lililoko Mbezi- Makonde, Kinondoni, Dar es Salaam linafanya ibada zake Jumanne badala ya Jumapili wakiamini ndivyo Neno la Mungu linavyotaka.
Jambo lingine ambalo linachagiza u-ajabu wa kanisa hio ni kupinga jina la Biblia Takatifu. Muumini mgeni anayefika kwenye kanisa hilo hulazimika kukabidhi Biblia yake kwa uongozi ambapo wao hutoa ‘kava’ ya nje yenye jina la Biblia na kuweka kava nyeupe yenye maandishi ya Kitabu Cha Bwana.
Kama vile hayo hayatoshi, kanisa hilo linaamini siku za mwezi ni 28 na si 29, 30 au 31. Wanasema Mungu alipanga hivyo na ndiyo maana  aliwapa hata wanawake mzunguko wa siku 28 kuingia katika hedhi.
                               
“Kinachotuingiza kwenye majira halisi ya Mungu ni kufuta tarehe 29, 30 na 31 za Julius Kaisari katika kila mwezi wa kalenda ya Gregori kwa mamlaka ya Mungu wa Majeshi ili kuondoa uovu ulioambatana na tarehe hizo za ziada kwenye miezi 12 ya mwaka,” alisema muumini mmoja kanisani hapo.
Uchunguzi unaonesha kuwa, kuanzia mwaka 2008 kanisa hilo lilichapisha kitabu ambacho kinaonesha kuwa mwanzo wa mwaka si Januari bali ni Machi (wao huita Abib au Aviv). Na mwisho wa mwaka si Desemba, bali ni Februari (wao huita Adari).
                       
Waumini wakiendelea na ibada ndani ya kanisa la The Pool of Siloam.
Kwa ugunduzi wao huo, kuanzia mwaka 2008 kanisa hilo hawafanyi ibada ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Bwana Yesu Desemba 25, yaani Krismasi kama madhehebu mengine ya Kikristo kwa vile wanaamini Yesu alizaliwa Februari 28.
Uwazi lilipata nafasi ya kupenya hadi ndani ya kanisa hilo ambalo limejengwa kisasa na kukutana na kiongozi mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Daudi Elia ambaye alisema kuwa makanisa  mengi hayafanyi kama ambavyo Mungu ameagiza.
Aidha, Daudi alimtaja kiongozi mkuu wa kanisa hilo kuwa ni Mchungaji Elia Amu wa Pili Mungu wa Majeshi Mtume na Nabii wa kizazi cha nne na akabainisha kuwa, awali alikuwa akifanya kazi Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco) kama  mhandisi.
“Aliacha kazi ya uhandisi na kuanza kumtumikia Mungu wa kweli kuanzia mwaka 2003, kazi  ambayo amekuwa akiifanya hadi sasa ambapo kanisa limesimama na kuenea Tanzania nzima na duniani,” alisema Daudi.
                         
...Waumini wakisali ndani ya kanisa hilo la The Pool of Siloam lililoko Mbezi- Makonde.
Aliongeza kuwa, Mungu alimwambia nia ya kumteua afanye kazi za kiroho ni kuvunja misingi mibovu ya kumuabudu na kuiweka inayofaa.
Mchungaji huyo ambaye alikuwa akiongea kwa niaba ya kiongozi mkuu, alisema kanisa hilo limekuwa na maagizo ya kweli ambayo  Mungu aliagiza yafanyike.
Kiongozi huyo akizungumzia namna ya kujiunga na kanisa hilo alisema kuwa, sharti la kwanza ni mtu kubadili jina lake la awali na kupewa lingine ambalo ni matakwa ya Mungu kisha kubatizwa upya.
Alisema kanisa hilo halikubaliani na mambo ya dunia kama vile kuwa na Siku ya Kifua Kikuu, Siku ya Ukoma, Siku ya Ukimwi na kadhalika kwa vile kufanya hivyo ni kwenda kinyume na ufalme wa Mungu.
Hata hivyo, baadhi ya waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kiluteri Tanzania (KKKT) wanaoishi jirani na kanisa hilo walipohojiwa kuhusiana na nyumba hiyo ya ibada walisema wana wasiwasi na nguvu za kishirikina ndiyo zinaratibu mwenendo wao.
                      
                                 Muonekano wa kanisa hilo kwa nje.
“Huwezi kuchana ‘kava’ la Biblia na kukataa jina la Biblia Takatifu kwa sababu kufanya hivyo ni kama uchawi ambao kwa Mungu haufui dafu,” alisema muumini mmoja ambaye alikataa kutaja jina.
Waumini hao walitofautiana na wa Kanisa Katoliki (RC) ambao walisema mambo ya kujadili namba ni mambo ya Freemason.
 “Hawa wanaosema namba za mwezi mwisho tarehe 28 ni mambo ya Freemason. Sisi tunaona hivyo,” alisema muumini mmoja ambaye naye hakutaka jina lake kuandikwa gazetini.
Hivi karibuni gazeti hili liliibua kanisa lingine liitwalo Brotherhood of the Cross and Star la jijini Dar ambalo waumini wake husujudu na kuingia kanisani wakiwa pekupeku huku mabikira wakipewa kipaumbele cha kupelekwa nchini Nigeria, makao makuu ya kanisa hilo.

6 comments:

  1. ENYI WANA TUNAOMTUMAINI MUNGU WETU WA KWELI SASA IMEFIKA WAKATI TUPIGE MAGOTI NA KUFUNGA KWELI YA ROHONI ILI MUNGU AONDOE MAKANISA MACHAFU YOTE YANAYOMAZILILISHA YESU KWA SABABU YA WATU WANAOTAKA MAISHA YAO YA AJABU HUKU WAKILITUMIA JINA LA BWANA YESU!NA TOKA SASA WASHINDWE KWA JINA LA YESU KRISTU WA NAZERETI ALIYE HAI! SHINDWENI ENYI WATUMISHI WA KUZIMU HAMNA MAMLAKA DUNIANI WALA MBINGUNI,DAMU YA YESU IWACHOME!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. SISI WANA WA MUNGU WA KWELI TUMEWAAGIZIA MAJESHI YA MBINGUNI AMBAYO YAMEANZA VITA VYA KUANGAMIZA NGOME YA DINI YA MASHETANI DUNIANI KOTE!MAOMBI YETU MUNGU AMESIKIA KILIO HIKI NA DUA ZETU!HIVYO TUNAISUBIRI SIKU YA BWANA YAJA!

    ReplyDelete
  3. MAONI HAYA YAWEKWE HAZARANI KWANI MABIKIRA HAO WANAOPELEKWA NIGERIA NI KWAMBA WANAENDA KUTOLEWA KAFARA NA WENGINE KUPANDIKIZWA MAROHO MACHAFU AMBAYO HUTUMWA KUIHUBIRI INJILI YA UNGO HUKU WAKITOA MAPEPO KWA JINA LA YESU LAKINI SIVYO NI NGUVU ZA GIZA KUU!HII HUWAPELEKEA WATU KUKIMBILIA KUPONYWA HUKU WAKIPELEKA SADAKA NONO AMBAZO NI KIPATO CHA WAPONYAJI HAO! AJIRA YA KUZIMUUUUUUUUUU!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  4. HIZI NI NYAKATI ZA MWISHO KAMA MAAGIZO YA BWANA WETU YESU ALIVYOSEMA WATAKUJA MANABII WA UONGO WATAKAO LITUMIA JINA LANGU KUFANYA MIUJIZA HIVYO TUWE MAKINI SANA NA TUWEZE KUPAMBANUA NYAKATI KWA KUZUNGUMUZA NA MUNGU ILI TUEPUKANE NA HAO WATUMISHI WA SHETANI WANAOMALIZAI ROHO ZA WATU HUKO KUZIMU! MAANA YAJA SIKU BWANA YESU ATAKANA MBELE YETU KWA SIE ALIETUPONYA KATIKA SHIDA NA MARADHI YETU NA NDIPO ATAKAPOSEMA ENYI KIZAZI CHA NYOKA KISICHOSIKIA TOKENI KWANGU ENDENI JEHANAMU YA MILELE! NDUGU ZANGU AMKENI HARAKA YAKIMBIENI MAKANISA YA MAROHO YA SHETANI KWANI WENGI WETU WAMETEKWA WAKIWA NA UCHU WA MALI NA UTAJIRI BATILI!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! KAMA WEWE UKO NDANI YA KANISA LINALOTILIWA MASHAKA NA HUENDA UMESHAPUMBAZWA NA MAROHO HAYO MABAYA JITAHIDI KUMWITA MUNGU WA UKWELI KATIKA NAFSI YAKO MUELEZE ULIPO NA JIBU ATAKUPATIA MAPEMA TU.SISI TUKAZA BUTI LA MAOMBI KWANI HATUTISHWI NA SHETANI HIVYO MAOMBI YETU YATAKUWA MSAADA WA KUWAKOMBOA NDUGU ZETU WALIOTEKWA NA MILKI YA SHETANI!

    ReplyDelete
  5. ENYI WATUMISHI WA UONGO MNAOTUMIA JINA LA YESU ILI MPATE UMAARUFU MKASAHAU KUWA UMAARUFU NI WA MUNGU TU!OLE KUU IKO MBELE YENU TAKA MSITAKE ATAWAHUKUMU MFALUME WA AMANI BWANA YESU!NYIE ENDELEENI KUKATA MAISHA YA RAHA KW KUJIKUSANYIA SADAKA NA KUJIWEKEA AZINA DUNIA KWA KUWA PUMBAZA WANADUMU WENZENU!POLENI SANA KWA UNAJIMU DUNIA!

    ReplyDelete
  6. WATUMISHI MMEVAA MAVAZI MAZURI YA GHARAMA NA MADHABAHU ZENU MMEZIPAMBA VIZURI SANA KATIKA ULIMWENGU MACHO YA NYAMA YAPENDEZA ILA KWENYE ULIMWENGU WA ROHO WA MUNGU MNATISHA KWANI HUMO KANISANI MNA JOKA KUU NA VIKARAGOSI LUKUKI VIKIAGUA WATU NA MAMBO MENGI YA KUTISHA NA MALANGONI MWA MAKANISA HAO KUMECHIMBIWA MAPEPO YANAYOWAVAA WAUMINI BILA WAO KUJUA TENA WKIDHANI WAKO IBADANI KUMBE WANAINGIA KUZIMU KUTUMIKISHWAAAAAAAAAAAAAAA NA HIYO NDIYO IBADA YA MASHETANI!!!!!!! PESA ZAO ZOTE WAMEPELEKA HUKO HUKU WANAJISIFU WANAMTOLEA MUNGU!JAMANI MUNGU HANA MPANGO NA MATOLEO HAYOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO! POLENI SANA NDUGU ZETU!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete