MCHUNGAJI
wa Kanisa la Glory of God Miracle Center, Peter Rashid Aboubakar
(pichani), ametupiwa skendo kisha yeye mwenyewe akakiri kuoa mwanaume
mwenzake.
Peter ambaye mwenyewe hupenda aitwe mtume, ameshuhudia
mbele ya Uwazi kwamba ni kweli alioa mwanaume lakini ni zama ambazo
alikuwa hajaokoka wala kupata upako wa kuongoza kanisa.
Awali, Uwazi
lilipokea taarifa kutoka kwa vyanzo vyake kwamba Peter na utumishi wa
Mungu wapi na wapi, kwa maana ana rekodi za uchafu, ikiwemo kuishi
kinyumba na mwanaume mwenzake.
Chanzo chetu kilidai kuwa Peter alimuoa mwanaume mwenzake anayeitwa Abdallah Athuman na waliishi wote Ilala, Dar es Salaam.
ALICHOKISEMA MTUME PETER
Mchungaji huyo alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo alijibu: “Kwanza hiyo
siyo skendo. Huyo Abdallah Athuman Hamis, ni kweli nilimuoa, hata kwenye
ushuhuda wangu nimeeleza, kwa hiyo siyo jambo la siri.”
Peter
aliendelea kusema, alitoa ushuhuda mzito kwenye mkanda wa video uliopo
kwenye DVD, akieleza matukio yake mengi aliyowahi kuyafanya kabla
hajaokoka, likiwemo hilo la kuoa mwanaume mwenzake.
“Ndani ya huo
mkanda wa video nimeeleza kwamba kabla sijaokoka nilikuwa mchawi,
nilikuwa na wake wanne. Watatu ni wanawake na mmoja ni mwanaume, tena
kwa sababu nilikuwa nampenda sana, nilimjengea nyumba Ilala,” alisema
Peter na kuongeza:
“Niliishi naye kwa miaka sita. Mwaka 1998
niliachana naye baada ya kuokoka. Kwa hiyo siyo tu kuoa mwanaume, mimi
nilikuwa mchawi kwelikweli wakati sijaokoka.”
KILICHOPO NDANI YA DVD
Timu ya Uwazi, ilitazama mkanda huo wa video na kubaini mambo kadhaa ambayo Peter aliyatolea ushuhuda:
Aliua na kula nyama za watu kwa njia za kichawi.
Alikuwa bosi wa wachawi ukanda wa Afrika Mashariki. Cheo hicho amedai alipewa chini ya bahari na Lucifer (Shetani).
Aliua mke wake wa kwanza na watoto kwa kuwatoa kafara ili atunukiwe mamlaka kwenye himaya ya wachawi.
Chanzo cha kuokoka kwake ni maradhi ya mkewe kupata hedhi isiyo na kikomo.
Alizaliwa kwenye ukoo wa wachawi, akasomea fani hiyo ya ushirikina na kufuzu kwa alama za daraja la juu.
No comments:
Post a Comment