Serikali ya Scotland imetangaza kwamba itaruhusu ndoa za watu wa jinsia moja.
Hii inamaanisha kuwa Scotland inakuwa jimbo la kwanza la uingereza kutangaza sheria kama hiyo.
Naibu
waziri mkuu wa Scotland Bi Nicola Sturgeon amesema hatua hiyo ni ya
maana sana na inastahili hasa kwa vile serikali yake inayoheshimu usawa
wa kijinsia.
Huenda Scotland ikajitokeza kuwa sehemu ya
kwanza ya Uingereza kukubali ndoa za watu wa jinsia moja baada ya
serikali ya SNP kutangaza mipango ya mabadiliko hayo.
Mawaziri wamesema kua muswada huo utajadiliwa
mapema ikiashiria kua sherehe za kwanza huenda zikafanyika mwanzoni mwa
mwaka 2015.
Viongozi wa kisiasa, mashirika yanayowania usawa na makundi ya imani yamefurahia hatua hio.
Hata hivyo ndoa ya jinsia moja inapingwa vikali na kanisa katoliki pamoja na Kanisa la Scotland.
ndoa ya jinsia moja
Tangazo hilo lilifanywa kufuatia mashauriano ya serikali yaliyopokea majibu kutoka kwa watu 77,508.
Sheria ya Scotaland kwa Wapendanao wa wanaoishi
pamoja wanaweza kuingia wenzi lakini serikali imesisitiza kua hapana
taasisi yoyote ya kidini inayolazimishwa kuendesha sherehe za kufunga
ndoa.
Serikali ya Scotland imesema kua itashirikiana
na Mawaziri wengine Uingereza kuona kubadili sheria zinazowalinda watu
mashuhuri wasichukuliwe hatua endapo watakataa kukemea au kukashifu ndoa
za watu wa jinsia moja.
Waziri kiongozi wa Scotland, Nicola Sturgeon,
alisema kua bado tuna amini Scotland iliyo na usawa na ndio sababu
tunaendelea na mipango ya kuendesha ndoa za watu wa jinsia moja -tuna
amini uwamuzi huu ndiyo jambo sawa.
No comments:
Post a Comment