Friday, June 15, 2012

Dully Sykes aonyesha dharau live XXL ya Clouds FM

 Dully akiwa katika picha
Nachelea kusema kuwa wanakuwa wanalewa ama sifa au vijisenti ambavyo wanakuwa wamevipata na kusau mashabiki ndio wamewafanya wawe na umaarufu walionao na si tu mashabiki bali vyombo vya habari ndio vimewafikisha hapo walipo.
Binafsi nimekerwa sana na kitendo cha mwanamuziki Dully Sykes kukosa adabu akiwa si tu studio bali akiwa Live kwenye kipindi ambacho mashabiki wake wengi wanamsikiliza. Ndani ya wiki moja msanii huyu ameweza mara mbili kukosa adabu tena kwenye radio moja hiyo hiyo.
Wiki iliyopita akiwa live kwenye kipindi cha XXL Dully Sykes alimjibu fyongo mtangazaji Adam Mchomvu wa kipindi hicho mwanzo nilidhani ilikuwa utani lakini Dully alisisitiza kuwa hawezi kuongea na mtu mchafu kama Adam Mchomvu, “siwezi kuongea na mtu mchafu kama wewe angalia mi nywele yako…. mi naongea na Boss wako biashara si mtu mchafu kama wewe” alisema Dully. Baada ya kuangalia kipindi kile kesho yake kupitia Nyuma ya Lensi kupitia Clouds TV nikaona jinsi ile ilivyomuumiza Adam Mchomvu na alivyokuwa akitulizwa asiendelee kujibishana na Dully kiasi alivua headphones na kukaa pembeni.
Kumbuka Dully alikuwa akifanya mahojiano juu ya wimbo wake mpya ambao ameutoa kwa kumshirikisha Mwana FA. Baaada ya Single hiyo inayokwenda kwa jina la Ameen kupigwa hewani watu wakaanza kusema kuwa Single hiyo imefanyiwa sampling kutoka kwenye wimbo mmoja wa huko Jamaica. Hii ilimpelekea Gossip Cop wa Clouds fm kuruka hewani na kumuuliza kwanza Mwana FA juu ya hiyo ambaye alikiri kwa kiasi fulani midundo imefanana lakini alisema ailizwe Dully Sykes ambaye naye baada ya kupigiwa badala ya kujibu alionyesha kukerwa na swali hilo inawezekana style ya kuulizia ya Gossip Cop lakini Dully alimjibu kuwa haongei na mashoga na kumuonya asipige tena.

No comments:

Post a Comment