Wednesday, October 3, 2012

Wachina wanaongoza kwa matukio ila hili limetia fora


WAHIFADHI MWILI WA KIJANA WAO MIAKA 6 KWENYE JOKOFU NCHINI CHINA

 

Tian Xueming akiangalia mwili wa kijana wake katika jokofu.

Nyumba ya Tian Xueming.
NI miaka sita sasa tangu familia ya Tian Xueming raia wa nchini China ianze kuhifadhi mwili wa kijana wao kwenye jokofu.
Mwaka 2006, familia hiyo ilimpoteza kijana wao aliyefariki kwa ugonjwa wa leukemia. Tian Xueming mzazi wa kijana huyo aliamua kuuhifadhi mwili wa kijana wake katika jokofu. Kila mara wanapomkumbuka kijana wao, Tian na mkewe wanakwenda kimyakimya katika jokofu na kuuangalia mwili wa kijana huyo. Tim anasema kuwa "kijana wangu katika jokofu anaonekana kama alivyokuwa enzi za uhai wake. Mwanangu bado yupo pamoja nasi mpaka leo."
Miaka 15 iliyopita, familia ya Tian Xueming ilimpoteza pia binti yao aliyefariki kwa ugonjwa wa moyo. Miaka sita baadaye kijana wao naye akafariki kwa leukemia.


No comments:

Post a Comment