Saturday, June 30, 2012

Sababu 7 za vibinti kushobokea penzi la watu wazima





1. Wanajua kupatiliza wanawake
Katika uchunguzi uliofanyika kwa kuzungumza na baadhi ya wasichana, imeonesha kuwa wengi wao wanapapatikia watu wazima kwa kuwa wanajua namna ya kumpatiliza mwanamke. Wanajua kujali, kubembeleza na kuwafanyia wapenzi wao vitu ambavyo wanavitaka kwa wakati bila longolongo.
Inaelezwa kuwa, watu wazima wanawachukulia wapenzi wao kama watoto hivyo kuchukua nafasi ya kuhakikisha wanakuwa ni wenye furaha wakati wote.
2. Wanajua kuhudumia
Inasemekana kuwa, mtu mzima anapoingia kwenye uhusiano, anakuwa mwenye msimamo unaoweza kufanya mambo yakaenda kama alivyopanga. Akisema anakupenda anamaanisha kweli na atakuwa tayari kwa gharama yoyote kuhakikisha uhusiano au ndoa inadumu.
Linapokuja suala la fedha, watu wazima wanaonekana si wabahiri. Wanajua kuhudumia ili mradi tu wapewe penzi lenye ujazo unaostahili. Hapa ndipo panapowagusa wengi.
Katika wasichana 10 niliowauliza sababu za baadhi yao kupenda watu wazima, 9 walisema ‘wazee’ siyo bahiri na wanajua kuhudumia na kumfanya mwanamke aishi maisha ya raha mustarehe tofauti na vijana ambao mwanzo wanaweza kuanza kwa kujifanya wanajua kuhudumia lakini baadaye wanageuka kuwa ‘marioo’.
3. Wanajiamini
Asilimia kubwa ya wanawake ulimwenguni kote wanapenda kuwa na wapenzi/waume wenye msimamo na wanaojiamini. Hata hivyo inaonesha kuwa, watu wazima ni wenye msimamo na wanajiamini zaidi kuliko vijana na ndiyo sababu ya baadhi ya wasichana kuwashobokea.
4. Wamepevuka
Watu wazima ni watu waliopevuka kiakili na kimwili hivyo wana uwezo wa kuwafanya wapenzi wao nao wakapevuka kadiri siku zinavyokwenda. Ndiyo maana baadhi yao wakishaolewa au kuwa kimapenzi na watu wazima wanabadilika katika maamuzi. Hicho ni kitu kinachowafanya baadhi yao kupenda kuwa na watu wazima.
5. Wameshafanya makosa mengi, wamejifunza
Mtu mzima ni lazima atakuwa amepitia uhusiano na watu wengi. Atakuwa amepata uzoefu mkubwa kwani atakuwa amefanya makosa mengi na kupitia hayo atakuwa amejifunza, hawezi kuyarudia.
Kwa maana hiyo mwanaume mwenye umri umri mkubwa akiingia kwenye uhusiano na kabinti ni vigumu kukakwaza, kila atakalotaka kulifanya ambalo atahisi atamkosea ni rahisi kuliacha hivyo kumfanya msichana aliyeingia kwenye uhusiano naye kutopokea samahani za kila mara kwa mara.
6. Hawaigizi
Ni kweli wapo watu wazima wale tunaowaita mafataki ambao wanapomtokea binti mdogo lengo lao si kuoa bali ni kuonja penzi kisha huingia mitini.
Hata hivyo, uchunguzi unaonesha watu wazima wengi wanajua kupenda na wanaposema hivyo wanamaanisha kweli, hawaingizi sanaa na ndiyo maana ni wepesi wa kuhudumia, kubembeleza na kuchukua nafasi ya ‘ubaba’. Hicho kinawafanya wasichana wengi kukimbilia huko.
7. Hawana wivu wa kijinga
Wapo ambao wana wivu kweli lakini uchunguzi unaonesha kuwa, watu wazima wengi hasa wale walio kwenye uhusiano hawana wivu wa kijinga unaoweza kuwa kero.
Hawana tabia ya kupiga simu kila mara na kuuliza uko wapi, hawana maswali kama vile; ‘yule uliyekuwa unaongea naye ni nani’, kwa kifupi watu wazima wakipata kile wanachokitaka hawana ile kumfuatilia mtu licha ya kwamba wakibaini wanamegewa wanaumia sana na ni wepesi wa kuchukua maamuzi magumu.

No comments:

Post a Comment