Tuesday, September 25, 2012

Mama Rwakatare na Dk. Cheni Presha juu

Nyumba ya Dk. Cheni.
Nyumba ya Mama Rwakatare.

SAKATA la kutangazwa kubomolewa kwa majumba yao kwa sababu tofauti, Mchungaji wa Kanisa la Assembles of God Mikocheni B ‘Milima ya Moto’ la jijini Dar es Salaam, Dk. Getrude Pangalile Rwakatare na staa wa filamu za Kibongo, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’, sasa presha zao juu.
Kwa upande wa Mama Rwakatare, mjengo wake wa bei chafu aliouzindua hivi karibuni uliopo Mbezi Beach, Dar utavunjwa kwa madai kwamba umejengwa kinyume cha sheria za mazingira kwani upo katika maeneo ya kando mwa mito ya Mbezi Beach, Mndumbwe na eneo maalum la hifadhi ya miti adimu ya Mikoko.


Kwa mujibu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), baadhi ya majumba katika maeneo hayo yameshabomolewa katika oparesheni iliyohusisha Wizara ya Maliasili na Utalii na kusimamiwa na Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) cha Jeshi la Polisi, lakini jumba la Mama Rwakatare ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM) liliachwa kutokana na kuwapo zuio la mahakama lililofunguliwa na mchungaji huyo.
Kwa upande wake Dokta Cheni, naye presha ipo juu kufuatia jumba lake la kifahari lililopo Vingunguti, Dar kutaka kubomolewa ili kupitisha upanuzi wa reli.
Kwa mujibu wa Dk. Cheni ni kweli presha ilimpanda aliposikia nyumba yake itabomolewa lakini akaweka wazi kuwa, si kwa sababu ya kupitisha njia ya treni bali kuna mwekezaji anayelitaka eneo hilo hivyo serikali imemwambia awalipe ndipo afanye zoezi hilo la ubomoaji.

No comments:

Post a Comment